wilcoxon
JF-Expert Member
- Jun 25, 2017
- 1,094
- 2,831
Mpaka sasa ni dhahiri kuwa katiba mpya inayotakiwa kulinda rasilimali za nchi haizuiliki na wala halipaswi kuwa ombi tena, mikataba yote inayohusu rasilimali za nchi ijadiliwe bungeni tena 'live' kabla ya kusainiwa, kwa jinsi ripoti mbalimbali zinavyoibua uozo mbalimbali wa huko nyuma ni makosa makubwa kuamini na kumkabidhi mtu mmoja au wawili mamlaka ya kufanya maamuzi makubwa ktk wizara ambayo yanaweza kuligharimu taifa.
Hatujui atakayefuata baada ya Magufuli, hivyo katika mazingira ya aina hiyo, ambayo viongozi wengi siyo waaminifu, njia pekee ya kuwadhibiti ni kuboresha mfumo wa kuwabana, kuwashauri na kuwaelekeza kabla hawajafanya maamuzi makubwa kama kusaini mikataba gizani kwa niaba ya taifa, hapo ndipo kuna tatizo kubwa ktk mikataba ya nchi hii maana huko gizani lolote hutokea.
Hata wawekezaji wa kimataifa wanapenda mikataba ya gizani kama ule mkataba wa buzwagi uliosainiwa na Karamagi kule Marekani, maana ktk giza ndipo hawa wawekezaji hutumia mwanya huo kupenyeza vifungu vinavyowalinda.
[HASHTAG]#CCMMpya[/HASHTAG] inatakiwa ianze kuwekeza nguvu ktk hili eneo ikiwa ni mpango wa muda mrefu wa kuijenga Tanzania mpya. Binafsi ripoti ya leo kuhusu madini ya Tanzanite imenisikitisha sana.
Magoiga SN (huyu ni kada mtiifu wa chama cha mapinduzi)