Elections 2010 CCM wajifunze mazuri ya upinzani

everybody

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
337
103
Unajua Baba akiambiwa na mtoto wake kwamba amekosea huwa inauma na huenda akamgombeza mtoto. LAKINI baada ya hapo hukaa na kutafakari maneno ya mtoto na huenda akauona ukweli ndani yake.

Nawashauri CCM watafakari sera za upinzani na kufanyia kazi zile ambazo zinamanufaa kwa raia wake ingawa kwenye kampeni wamekuwa wakizipinga bila kutafakari. Sasa ndo wakati wa kuchukua nafasi kutafakari.

Ahadi nyingi zilizokuwa zikitolewa na K hazitekelezeki kwa kipindi hiki kifupi cha miaka 5. Ningewashauri waitafakari sera ya elimu na afya bure kwani inatekelezeka na itamnufaisha kila raia. Hivi ni vitu vya msingi na vinachangia kwa kiasi kikubwa kwenye umaskini wa mtanzania.

CCM wasione aibu kujifunza kwa wapinzani na kuyafanyia kazi yaliyo mazuri badala ya kujifanya viburi... Kukubali umekosea ni njia ya kujiongezea busara.

Najua utakuwa na wakati mgumu mheshimiwa K kwa sababu wewe si chaguo la walio wengi. Kwa faida yako jitahidi kutekeleza yale ambayo raia wanayahitaji walau kurudisha imani kwa wananchi waliokata tamaa.

....Inaumaaaaaa......
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom