mgeni wenu
JF-Expert Member
- Jan 2, 2012
- 3,664
- 1,730
Wana JF kama mlivyoona baada ya CHADEMA kuleta wabunge wake makini Arumeru na kumwaga CHECHE katika ufunguzi,Leo wabunge wa CCM wamefurika mjini hapa kwa ajili ya Kujibu mapigo,Guest na Hoteli zote zimejaa Mji umechangamka Bia na nyama choma zinanyweka huku kukiwa na Mkesha wa Taarabu usiku kucha katika viwanja ambavyo CCM watafanyia Mkutano,Tyr Mzee mkapa kaingia na kupokelewa na Chiligati na Mwigulu,wabunge wa CCM wanazunguka kila kona ya mji wa USA na Leganga katika baa huku wakiwanunulia vijana Viroba na bia kama njia za Ushawishi kesho kuja Mkutanoni,Huku wasanii wa khanga Moko wakitegemewa kutoa burudani jukwaani
Wabunge wengine wamekwenda kulala Arusha Mjini baada ya Hotel zote kujaa na kubaki Guest House ambazo siyo hadhi yao,na ndizo walizopo Wabunge wa CHADEMA na baadhi ya waandishi wa Habari.
Kesho nitakuwa katika mikutano kadhaa ya wagombea na kuleta habari kamili
Nikiripoti kutoka Arumeru ni mimi mgeni wenu wa Jamii forums