CCM wafunga shule MSATA, Ugomvi watokea


sasa nimekuamini baada ya kuona na mwana JF mwingine kaandika.
hii ni hatari, ila ndivyo nchi yetu ilivyo wala sishangai
 
Kumbe ni huko Chalinze! Watoto watakuwa wamefurahi sana kupata likizo.... Japo sio fair kbs

Haikuwa sawa kuwanyima watoto haki yao ya kupata elimu! kumbuka watoto hao wanazaliwa na wazazi wenye itikadi tofauti za kisiasa.
 
Kamishina waelimu hili linakuhusu hufai kuwa hapo kama ,watoto wetu hawasomi eti kwasababu ya uchaguzi wa ccm.Kwa stail hii ccm mnaua watoto wetu kielimu
 
samani mkuu,nikikomenti
hapa nitakuwa mjinga kuliko hata hao waliowatoa watoto shule kwa ajili
ya manufaa yao binafsi

Mkuu hivi unajua maana ya Mp.um.bavu? Ni mtu anaye faanya jambo isivyo huku akijua sawia kufanya itakiwavyo, hivyo basi huoni wewe unaangukia kwenye up.umba.vu kwa kucoment wakiti hukutaka kufanya hivyo?
 
Hoja zingine sioni kama zinamantiki ni kama za kilevi hivi imejaa uongo na ushabiki wa wazi kabisa.
 
Chadema kwa kuchanganya uongo ipo siku mkikosa la kusema mtatafuna ulimi.
 
hoja zingine sioni kama zinamantiki ni kama za kilevi.
unatumia simu mjengoni? Halafu mkuu ukipata posho hebu ntupie kwnye ile no yangu nkapate hata kitimoto! Kizuri kula na nduguyo mwenzio jk kanitosa bungeni!!!
 
Eneo la shule ?
Hata kama ingekuwa ni Uwanjani as long as ni eneo la shule, siku ya masomo na muda wa masomo, Hakika haikubaliki.
Na matokeo ya Form 4 Shule hii ni kama haya halafu wanakatishwa masomo kisa uteuzi wa RIDHWANI KIKWETE.Pia hii inaonyesha jinsi watu hawa wasivyopenda na kuthamini elimu kwani MWANAASHA ambae alikuwa shule nzuri na ya gharama kubwa(FEZA) aliambulia DV IV

S1968 MSATA SECONDARY SCHOOL

[h=3]DIV-I = 1 DIV-II = 5 DIV-III = 11 DIV-IV = 30 DIV-0 = 46[/h]
 
Chama cha mapindunzi chalinze kimefanya kitendo cha ukandamizaji wa elimu kwa hali ya juu sana baada kumlazimisha mwalimu mkuu wa shule ya secondary msata kufunga shule siku ya leo ili kupisha chama hicho kufanya mkutano mkuu wa uchaguzi wa kura ya maoni ya kupata mgombea ubunge jimbo la chalenze,mbaya zaidi baadhi ya wanafunzi ndio wamekuwa wakiwaudumia hapo shuleni kwa maitaji ya mají na chakula,elimu yetu inadhalilishwa kwa kiwango hiki! Wagombea wa nafasi hiyo ni wanne Ridhiwan Kikwete, Imani Madega, Ramadhan Maneno Na Mwanamama Mkwazu.wadau wa elimu
 
Tutoe shaka za habari yako tupia hata picha 2/3 hasa ya shule, wanafunzi kugawa vinywaji na ya wajumbe kugombea mgao. Hapo hatutakua na shaka na habari hii.
 

Nakumbuka ilishazuiwa kufanya mikatano ya kisiasa katika taasisi za umma. Ikitokea kesho CUF wakenda kuomba nafasi, keshokutwa CHADEMA, siku inayofuata ACT-Tanzania watoto wetu watasoma kweli?
 
umbea mtupu. Baada ya kuanzisha viwanda vya kutengeneza gongo, sasa chadema wana viwanda vya kutengeneza porojo
Mara nyingi CCM wamekuwa wakijibu hoja makini kwa kejeli na mzaha. Ebu angalia hiyo hapo juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…