CCM wachota mamilioni ya kampeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wachota mamilioni ya kampeni

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by nyabhingi, Oct 19, 2010.

 1. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  35,000,000/= zimechotwa kutoka kila mkoa kwa kisingizio cha pesa ya kusimamia mitihani ya form 4..

  Kawaida fedha zinazopelekwa kwenye taasisi cheki zake hufungwa (closed cheques) yaani lazima zilipwe kwenye akaunti husika lakini hizi zilichukuliwa kama masurfu maalum(special imprest), kwa uzoefu wangu kazini sijawahi hata mwaka mmoja usalama wa taifa wakapewa kiasi hiki cha fedha na kwa kukiuka kanuni za fedha.

  Fedha hizo zilichotwa mwezi Septemba ka ushirikiano mkubwa wa katibu mkuu hazina na wafanyakazi wa juu wa hazina,ndiyo maana fedha za matumizi mengine (other charges) za mwezi wa tisa ama hazikuwepo au zilikuwepo kidogo sana mawizarani,tawala za mikoa, halmashauri na taasisi nyingine za serikali, other charges hutumika kulipa per diem, stationeries, matengenezo na mengineyo..

  Fanya hesabu:

  35,000,000*(mikoa 26) = 910,000,000..

  Ukijumlisha na zilizopigwa wizarani na kwenye halmashauri....jibu lake ni ufisadi wa kutisha....kwa mpango huu Salma na Ridiwani na Kikwete mwenyewe hata wakitumia rocket kwenye kampeni zitagharamiwa kwa kodi yako.

  NIAMINI NIYASEMAYO SABABU NIPO KARIBU SANA NA NINAYOYASEMA.....

  [​IMG][​IMG][​IMG]
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  UUUUIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIiii eeeh mungu tuepushe na familia hiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Hii nashindwa kuchangia manake source sina uhakika nayo, hawachelewi kusema chadema tunazusha!
   
 4. Y

  Yetu Macho JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Michezo yao hiyo ila yote yana mwisho

  Peopleeeeeees...
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Leta ushahidi hapa sio mahali pa maneno yasiyo na ushahidi maana unasema uko karibu na chanzo cha habari hii. Basi tufanyie hisani uje na data. Au sema ni tetesi tujue. Hata hivyo kuna watakaoanza kuzifanyia kazi
   
 6. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Makampuni pia yamepewa agizo
  La kupeleka some millions kwa ajili ya kampeni za ccm. Mnaninyonya pesa zangu mnanilipa kijani barabarani...mna laana nyie watu.mwisho wenu utakuwa mbaya sana
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hata wachote sh ngapi safari yao imekwisha fika mwaka huu watu wanaangalia nani mgombea makini hawatazami nani anapaka poda usoni
   
 8. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Uwiiiiiii twafa.
   
 9. M

  Miruko Senior Member

  #9
  Oct 19, 2010
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 173
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Hizo sh milioni 900 ni sawa na fedha zilizodaiwa kuchangwa hivi karibuni kwa maelezo kuwa ni za kusaidia kampeni Singida;

  Habari yenyewqe ndiyo hii:

  CCM yachangisha Sh mil 900 za kampeni

  Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 11th October 2010 @ 07:36 Imesomwa na watu: 175; Jumla ya maoni: 1

  MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete ameongoza harambee ya kuchangia kampeni za majimbo na kata mkoani Singida, ambapo Sh milioni 900.4 zilipatikana.

  Katika harambee hiyo iliyofanyika juzi usiku jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete aliwaagiza wanachama wa chama hicho kushiriki ipasavyo kuchangia chama chao kupata ushindi Oktoba 31 mwaka huu.

  “CCM itaendelea kuifanya nchi iwe na amani na utulivu ikishinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, na yote haya tutafanya kwa Kasi zaidi, ari zaidi na nguvu zaidi.

  Tupeni ridhaa tuendelee kuongoza Dola muone haya,” alijinadi mgombea huyo wa urais.

  Kuhusu michango ya fedha za kampeni, Mwenyekiti huyo wa CCM aliwataka wanachama wenye uwezo mzuri kifedha, kuchangia chama chao kwani ada pekee haitoshi kuifanya CCM kumudu gharama mbalimbali zikiwemo za uchaguzi.

  “Wanachama wanategemewa sana kutoa michango ambayo ni ada ya uanachama ambayo hata hivyo haitoshi kufanikisha gharama mbalimbali, hivyo ni lazima wenye uwezo zaidi wajitolee ili kufanikisha ushindi kwa chama chetu.

  “Kura za urais zinapatikana katika kila kata na jimbo, ni vizuri mikoa mingine nako wafanye harambee kama hizi ili tupate fedha zaidi za kufanikisha kampeni,” alisema mgombea huyo wa urais wa kwa tiketi ya CCM.

  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Joram Allute alisema katika hafla hiyo kwamba wamelazimika kuitisha harambee hiyo, kwa kuwa wanaihitajika fedha zaidi kukiwezesha chama hicho kufanya kampeni na kupata ushindi wa kishindo mkoani Singida.

  “Tuna tatizo la upungufu wa rasilimali fedha katika kampeni kwa ajili ya ununuzi wa vifa, ukodishaji magari, mafuta na vitu vingine vinavyotakiwa katika kampeni ndio maana tumeitisha harambee hii,” alisema Allute.

  Baadhi ya waliohudhuria harambee hiyo ni Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM, John Chiligati, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya harambee hiyo pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Vifaa ya CCM Taifa, Mama Zakhia Meghji.
   
Loading...