CCM waanza? Magamba yaanzia kwa dagaa

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Kilumbe Ng'enda amevuliwa Ukatibu wa Mkoa wa Dar es Salaam (CCM) kwa kosa la kutenda maamuzi binafsi kinyume na maamuzi ya vikao halali vya chama.

Taarifa tulizo nazo zinazidi kueleza kuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar naye yupo kwenye hatihati. Nyeti nyingine zinadai kuwa kutokana na EL kujaza watu wake Dodoma ili wafanye fujo basi huenda yeye na Chenge wakaachwa na maamuzi yakatolewa ghafla baada ya mkutano huko Dodoma.

Nape kasema nafasi hiyo imeondolewa mikononi mwa Ng'enda na atapangiwa nafasi nyingine (wanaendelea kubebana???)
 
Mwee! Kweli ccm kwisha yani wanaogopa mapapa wanamuonea dagaa wavue gamba waone kazi chenge kasema mkimwaga mboga yeye ugali.
 
Haki ya nani walah hii inaweza kunkata utumbo. Mungu yapishilie mbali yasitokee.
 
Chama cha Mapinduzi bwana! Huwa hawana dharura eh!? Kwa nini hawakumtoa mara tu baada ya uchaguzi? Wapo slow mno...na huu u-slow slow ndiyo unaowaumiza!
 
What we need in Tanzania is parties with firm political structure ,clearly defined views and stand not group of political LovePeddlers(which is what we presently have on ground).

Sijui ni kwa nini CCM wanashindwa kutoa maamuzi sahihi bila kupendelea upande wowote at the same time wanaadhimisha miaka zaidi ya 34 tangu chama hicho kizaliwe.

Presently, Chadema seems to be the only prepared and ready to rule as political party with a determined and tested patriot who can lead the people in the nation building of a New Tanzania in the leadership of Africa among other nations in the 21st century.
 
Hahahaaaa...wanatumia ile kanuni kwamba ukitaka kuanza kuhesabu anza na 0,1,2,3,4.....etc kwahiyo watafika tuu kwa walengwa wa juu muda sii mrefu.Yangu majicho maana kama ni uoga wa maamuzi magumu kweli wanao...Na EL mwenyewe aliwashauri wakati fulani wawe na uwezo wa kufanya maamuzi magumu lakin wapi wanashindwa kuitumia hiyo kauli kumtekelezea yeye mwenyewe aliyewashauri kumwonyesha kwamba wanaweza fanya maamuzi magumu hata kumvua NYANGUMI.:smash:
 
mimi nilijua wanakata mibuyu kumbe wanafyeka matawi tuuu!!!

Kweli wezi wanaogopana sana!!!
 
Kikwete naye ang'olewe kwenye kiti cha Mwenyekiti wa chama taifa kwa kutenda kosa la kufuga wezi!
 
Idd Azan huyo,unajua jk anamkubali sana na alipeleka malalamiko yake buku zima lote madhambi ya kilumbe.
 
Maajabu sana. Mapapa makubwa yanaogopana. Yanaangaliana kama majogoo lakini hakuna wa kumrukia mwenzake. Hayo sio magamba yaliyopigiwa chapuo la nguvu mikoa karibu yote!!! Wavueni magamba hao mapapa tuwaone. Mmekwisha ninyi....
 
Back
Top Bottom