funguotatu
Member
- Jul 13, 2012
- 85
- 11
Kwa muda mrefu mimi ni mpenzi wa JF kwa sababu mbalimbali lakini muhimu ni mbili. Kwanza nafahamu kuwa JF kuna baadhi ya watu ambao ni wachambuzi wazuri wa mambo lukuki. Wapo wasomi wa kupindukia, wapo waliosoma wastani na wapo waliosoma kidogo. Sababu ya pili ya kuipenda JF ni kwamba inataarifa nyingi motomoto. Hata hivyo, kuna kitu ambacho nadhani kina walakini. Sina hakika lakini wachambuzi nijuzeni, nimeperuzi nyororo/uzi nyingi kuhusu CCM na zile za CDM. Maoni yangu ni kwamba wachambuzi mahiri wenye hoja zenye mashiko hugeuka ghafla na kuvaa vyeo vya makatibu wenezi na propaganda wa vyama hivyo vikuu.
Ikifika hapo huwa hawajali hoja bali ushabiki na hata matusi ya nguoni. Kinachonishangaza ni kwamba wachambuzi wenye hulka hizo ni walewale na hawakosi kutetea chama wanachokipigania japo mada inaweza kuwa ina ukweli na inaweza kutumika kuvijenga vyama hivyo iwapo kasoro hiyo itarekebishwa. Mara nyingi nimesoma kauli kuwa baadhi ya wachambuzi hao huwa wanalipwa kufanya kazi hiyo. Ninachouliza ni kwamba, Hawa watu wanaogeuza JF uwanja wa propaganda za vyama vyao huwa wanailipa JF? Pili, mchambuzi mahiri kugeuka shabiki hakukuondolei sifa yako ya uchambuzi? Naomba kutoa hoja.