kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 16,998
- 16,645
Ni njaa tu na faida binafsi zinazowafanya watu wahame kutoka chama hiki na kwenda chama kile.
Ukweli ni kwamba vyama vya siasa ni kama madhehebu ya dini na club za mpira waumini wake ni vigumu sana kuhama dini moja kwenda dini nyingine, dhehebu moja kwenda dhehebu lingine na kutoka club moja (Simba, Man Ukwenda club nyinge (Yanga, Arsenal).
Hata kama utatoa hela nyingi kumpa mwanachama na shabiki wa Yanga ahamie Simba atahama kiwiliwili tu lakini moyo na imani yake itabakia Yanga tu.
Miaka 25 ya uwepo wa vyama vingi nchini umesababisha nchi kugawanyika katika makundi wawili ya wananchi wenye imani kubwa na CCM na wale wenye imani kubwa sana na vyama vya upinzani na ukubwa wa makundi haya unazidi kukua kila siku kadiri siku zinavyoongezeka. Hivyo wako watu wenye imani na CCM hata kama iwe inafanya wizuri au inaboronga, na wako wale wasioipenda CCM hata kama itafanya mambo mazuri sana.
Watu wa aina hii mioyo yao itabaki CCM au upinzani siku zote na mara zote, litoke jua au inyeshe mvua. Watu wa aina hii hata kama wakihama chama watahama viwiliwili tu lakini mioyo yao itabakia upande ule wanaouamini. Hali kama hii inawapata hata wachezaji wenye mapenzi na club fulani za michezo.
Ni njaa, umaskini, utajiri, hasira, hamaki, visasi na maslahi binafsi vitasababisha watu wa aina hii wahamie upande mwingine na sivinginevyo. Kama wakishafanisha haja zao ama itatokea kushindwa kufanisha haja zao kule waliko hamia basi ni rahisi kurejea kwenye club zao wanazozipenda na kuziamini.
Hivyo mwanasiasa anayehamia ni hatari sana kumuamini 100% kwenye mipango yenu ya chama, maana nirahisi kurejea alikotoka na siri za chama kama akikumbana na changamoto hata zile ndogondogo tu.
Ninawashauri vyama vya siasa kuwa hata siku moja wasikubali kuwapokea wanachama wanaohamia na kuwajumuisha kwenye mipango yao ya ndani kabisa, iko siku watalia.
Vyama vya upinzani wanachama na mashabiki wenu wa kweli kweli kabisa ni wale wenye umri wa miaka chini 30 ambao walikuwa watoto wadogo wakati vyama vya upinzani vinazaliwa nchini na wale waliozaliwa ndani ya siasa za vyama vingi, hawa hawajawahi kuwa wanachama wala shabiki wa CCM. Wekezeni zaidi kwenye kundi hilo ambalo wengi wao ni wanafunzi bado na wachache wanajitegemea. Hawa wako royal kwenye upande wanatakao uamini.
Ni makosa makubwa sana vyama vya upinzani kuwategemea watu aina ya Mh. Lowassa, Sumaaye, Mashinji, Lwamwai, Msindai, Kingunge rip, Lyatonga, nk ambao maisha yao yote walikuwa CCM, yaani hapo ni sawa na kumwambia Mzee Mwina Kaduguda ahamie Yanga na Mzee Akilimali rip ahamie Simba.
Wanaohama vyama ni watu wenye mioyo miepesi kwelikweli, wenye uchu kwelikweli, wanaoweza kufanya lolote kwa manufaa yao, watu hawa ni hatari sana kuwaamini ndani ya vyama vya siasa. Hawa watakujakuwa vyanzo na sababu muhimu za vyama husika kugawanyika na kufa kabisa kwasababu yao.
CCM tuwaogope watu hawa kama ukoma, ni opportunistic hawa, angalieni nyendo zao kila saa na kila dakika maana hawana uvumilivu wala vifua vipana.