CCM tuwaamini kwa lipi?

CCM tuwaamini kwa lipi?

DIZZO MTAWALA

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2015
Posts
240
Reaction score
769
CCM kila ikifanya maamuzi yake inauhadaaa umma kuwa kutakuwa na mabadiliko kumbe washaiba.

Walipoleta sera ya ubinafsishaji tuliwapinga kwann mnagawa Mali za umma kama sadaka matokeo yake viwanda vilikufa uchumi ukadorora wakatupachika majina mabaya kwamba tunatumika viko wapi viwanda kama mwatex general tayre tanganyika pekers•

Wakatuhadaa tena uchumi wetu utapaa kwa kuuza madini yetu wakatunga sheria za kutunyanganya mali ya madini kwa hati ya dharura leo yamebaki Mashimo tu sio Geita, nyamongo ,mererani wala shinyanga kote umasikini umetamalaki Tundu lisu akapinga wakamuweka ndani akaibua ya bulyakulu watu walivyokufa wakasema anatumika na mabeberu huku wao wakiwapa mabeberu madini yetu.

Haikuishia hapo wakasema sasa uchumi wetu utabadilishwa na gesi watani zangu wa mtwara wakakiona cha mtema kuni watu walipopinga wakatupachika majina ya kutumiwa na mabeberu huku mabeberu wakichukua gesi yetu kilaaini.

Leo kichekesho zaidi wamekopa trillion moja kuboresha bandari kabla hata hajakaa sawa wameigawa bureee tena Milele yaani ccm ni janga kabisaa.

CCM hata mkituita majina Yoyote muitavyo nyinyi mmevuka level ya wizi yaaani mna mna medali ya ujambazi.
 
Back
Top Bottom