CCM Tusishangilie Bunge lijalo kukosa wapinzani

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
714
1,137
Kwa mwenendo wa siasa za sasa za Tanzania, kuna uwezekano mkubwa sana bunge lijalo likawa halina wabunge kabisa wa upinzani au wakawemo wachache sana.

Ni kweli awamu hii ya JPM imefanya makubwa sana, lakini kuna baadhi ya wana CCM wangependa kuona bungeni kukiwa na wabunge wa CCM pekee.

Hii itakuwa hasara kubwa sana kwa taifa,.pamoja na maendeleo tunayoyaona kuna mkono kidogo wa wapinzani kwani wakati wanainanga serikali ya CCM kushindwa kununua ngege, ufisadi katika miradi ya umeme wa dharura, wafanyakazi hewa hoja nyingi zilikuwa zikitolewa na wapinzani.

Lakini pia kuna wabunge wengi wa CCM kazi yao ni kusofia tu bila kutoa maoni na mwongozo wa nini kifanyike. Wabunge wengi wa CCM wanaogopa kuikosoa serikali wakiogopa chama kuwashughulikia.

Na wengine wanaogopa kuikosoa serikali wakitarajia kuteuliwa kuwa mawaziri na manaibu mawaziri.

Ni kutokana na hilo bado tunawahitaji sana baadhi ya wapinzani wenye mwelekeo wa kuipa changamoto serikali na kuyafanyia maboresho maisha ya Watanzania.

Kuna baadhi ya wabunge wa CCM ni mzigo kwa chama na serikali. CCM tukiwa peke yetu bunge lijalo itakuwa ni majanga na tutashindwa kuisaidia Tanzania yetu.
 
Hakuna jinsi.Bunge lijao ni 100 % chama tawala.

Je hi itakuwa ni kwa matakwa ya wapiga kura au kwa matakwa ya NEC?
 
Yanaweza kuwa matakwa ya wapiga kura lakini itarudisha.maendeleo nyuma
Hakuna jinsi.Bunge lijao ni 100 % chama tawala.

Je hi itakuwa ni kwa matakwa ya wapiga kura au kwa matakwa ya NEC?
 
Sawa upande flani ila unakosea kitu. jpm amefanya maovu makubwa mno na ubadhirifu mkubwa ila anatumia nguvu kuficha kama alivyofanya kuficha corona na kusema imekwisha, wewe unaamini corona imekwisha na unaona sawa kuficha takwimu? Ndivyo anavyoficha upotevu wa matrilioni na hakuna mtu anaweza kusema kitu. Tupo pabaya haijawahi kutokea.
 
Kuna mijitu mipumbavu itakuja hapa na kusema upinzani hauna maana, subiri tu utaiyona.
 
Back
Top Bottom