CCM tusilaumiane | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM tusilaumiane

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtaka Haki, Apr 3, 2012.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Napenda kutoa ushauri kwa wana CCM kuwa huu ni wakati ambao tutajilaumu na kuwalaumu wengi baada ya kupoteza jimbo la Arumeru Mashariki. Huku tukituma timu nzito.

  Tunaweza kulaumiana kwa yafuatayo AU KUWALAUMU WAFUATAO.

  1. LUSINDE KWA MATUSI YALIYOPOROMOSHWA MKUTANONI BILA SONI.
  2. MKAPA KUSEMA UONGO ULIOTUGHARIMU kwa kukanushwa na familia NA KUTUFANYA TUSIAMINIKE ( YEYE ZAIDI) KWA MANENO YALIYOFUATA.
  3. WASIRA KUENDELEZA UONGO WA MKAPA NA KUMPONDA SLAA BILA KUJUA ANAOONGEA NAO na hatimaye kanisa kukanusha.
  4. KUTUMAINI WAGANGA WA KIENYEJI NA KUWATUMIA KATIKA KAMPENI KINYUME NA IMANI YA WENGI.
  5.KUMCHUKUA SIOI KWA NGUVU YA PESA BADALA YA SARAKIKYA ALIYEKUWA CHAGUO LA WENGI.
  6. KUMTUMIA LOWASA mwenye tuhuma nyingi za kujibu.
  7.VIONGOZI WA CHAMA KUTOKUKEMEA LUGHA YA MATUSI ILIYOTUMIKA KIASI CHA WATU KUJUA NI UJUMBE WA CCM.
  8.KUWADHARAU WANANCHI KWA KUSEMA AU KUONYESHA HAWAHITAJI SERA BALI VIJEMBE.
  9. WATU WAZIMA WENYE HESHIMA KUNENA UONGO kwa kurudia bila kujali.
  10. SLAA ameaminiwa sana kwa kuwa kila alichokisema dhidi yetu hatimaye ilikuja kugundulika ni ukweli.

  Ni rahisi kulaumiana kwa sababu hizo hapo juu. Lakini ukweli tutulie tuchukue hatua juu ya magamba tuliyoahidi tutayatoa ili turudishe imani iliyopotea. Ni vigumu kuaminisha watu kuwa unaweza kuwasaidia wakati familia yako imekushinda na haina msaada. Kama tumeshindwa kuwachukulia hatua watuhumiwa walioko kwenye chama ni nani atakayeamini kuwa tutaweza kuendelea kuongoza serikali? Hatua yetu hii inaendelea kutoa umaarufu kwa upinzani. Wao wanachangiwa na wananchi sisi tunawahonga wananchi ili watuchague. TUSIPOCHUKUA HATUA BASI TUWE TAYARI KUPOTEZA KILA JIMBO LITAKALOKUWA WAZI NA KILA NAFASI YA UDIWANI. Hatua dhidi ya rushwa, wizi na ubadhirifu ni ya muhimu, Vinginevyo hata sisi wachache tuliobaki tunaondoka.
  Hatuwezi kuona chama kikifa mikononi mwetu huku hakuna hatua inayochukuliwa. Kuogopana hakuwezi kuendelea kuwa asili yetu.

  TUTAFAKARI TUCHUKUE HATUA ZA HAKI NA ZA KWELI AU TUBAKI TUKIENDELEA KUSEMA TUNAVUA GAMBA HUKU MIAKA IKIPITA. We have lost our moral authority. It will be very hard to keep on convincing people to trust us.
   
 2. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Natamani ungeshushwa kwenye kikao cha CCM NEC ukawamwagia haya sijui kama wangekusikia japo umetembea kwenye ukweli asilimia 100%.And for sure CDM is coming naita wacost CCM the hard way they didn't expect for real.
   
 3. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Lazima tulaumiane!!
  Turudishieni chama chetu!!
   
 4. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Ipigwe kura ya kutokuwa na imani na uongozi wa chaama uliopo.
  Unatugharimu.
   
 5. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kulaumiana ni muhimu sana kwetu ccm!
   
 6. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  nimependa pale uliposema "wakati wao wanachangiwa sisi tunawahonga wananchi ili watuchague" nakumbuka wakati kamanda mbowe anatangaza harambee ya kuchangia kampeni siku ya uzinduzi, walipotaja namba fasta nikatuma elf 2, leo najisikia raha mchango wangu umekuwa sehemu ya ushindi, natamani siku moja kamanda atangaze tuchangie kuanzisha tv na radio ya chama, walahi nitachangia kila mwezi hadi siku tunazindua tv na radio zetu.
   
 7. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Chama kimepoteza misingi yake kama walivyosema kina Butiku kwenye kipindi cha Je tutafika?

  Nilishangaa CCM kuibeza CDM "kwa kuwaomba wananchi" kuwasaidia kwa michango kuendesha chama! Hivi leo wangeamka wazee waliofariki miaka ya 1950 akaambiwa TANU iliungana na ASP ikabadilishwa jina. Akaambiwa aangalie matendo ya CCM na CDM halafu aseme kipi kilikuwa TANU, hakika hatasema CCM.

  Wakati wenzao wanajiweka karibu na wananchi (jamaa zao), inashangaza kumsikia mwenezi wa "Chama cha kijamaa", akijisifu kuwa wana ugeni wa wafanyabiasha "mabepari" kutoka Afrika Kusini. Na kuanza kuwacheka wenzao kwa kuwa "masikini".

  Unataka kuwa rafiki wa masikini kwa kujisifia utajiri uliopata kwa jasho la watanzania wote wakati wa chama kimoja!! Haya mambo yanakera, ngoja niishie hapa.
   
 8. g

  glojos88 Member

  #8
  Apr 3, 2012
  Joined: Jul 31, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukweli ni kuwa siku za chama zinahesabika kama hakuna mageuzi makubwa. CHADEMA wakitumia muda huu kuzunguka nchi nzima kitaeleweka. Kwa sababu wkati watu wameshindwa hunyong'onyea na kukosa nguvu. Hivyo this is the right time.
  Pia ni muhimu CHADEMA kutumia muda huu kwani huko MWANZA unyama wa CCM umeeonekana wazi kuwa ndicho chama cha vurugu na hakiitakii mema nchi hii. Kama wawakilishi halali wa wananchi wanaweza kufanyiwa hivyo na hakuna kiongozi anayekemea basi uhalali wa CCM kuongoza uko mashakani kwani hawawezi kuwalinda wananchi wake.

  Kama wameshindwa kuwalinda wawakilishi wa wananchi basi kinahitajika kiachie madaraka.
  Wale mnaotaka uongozi kupitia CCM someni alama za nyakati. Alama ya wakati wa CCM inaonyesha red.
   
 9. M

  MZALAMO JF-Expert Member

  #9
  Apr 3, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 471
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 60
  Ujumbe mzito sana huu kwa chama chako . Wanatakiwa watafakari na wachukue hatua haraka sana la sivyo chama kitawafia mikononi mwao.
   
 10. d

  dada jane JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli ndio inayoweka watu huru. Period!
   
 11. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  "ccm iko imara na itatawala milele" - Nape
   
 12. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #12
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  DEADSTONE LUSHINDWE awajibishwe!
   
 13. Blackman

  Blackman JF-Expert Member

  #13
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 724
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  gamba limelia
   
 14. a

  akelu kungisi Senior Member

  #14
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama thread hii ikisomwa na Mkuu wa kaya pale magogoni na akawa kimya basi kutakuwa na tatizo kubwa zaidi. Thread hiyo imamiliza kila kitu!
   
 15. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #15
  Apr 3, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Mkuu mimi sio Mwanaccm lakini nakubaliana nawe moja kwa moja. CCM hawajaanza matusi leo unakumbuka Bungeni wazusha kuwa Mdee anasagwa na Bulaya, jumlisha na ya kina wasira yapo mengi sana KWA UJUMLA CCM KIMEPOTEZA SIFA YA KUWA CHAMA DOLA. naamini safari ya kuitokomeza CCM imeshaanza kushika kasi. na kwa kifupi CCM haisafishiki labda ibadilishe jina.
   
 16. Micro E coli

  Micro E coli JF-Expert Member

  #16
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Magamba huwa hawasikii wameweka nnta masikioni,sikuzote chama kikitaka kuporomoka mbinu za kukizuia kisiporomoke ndizo hukiporomosha zaidi tizama pesa wanazotumia ccm kwenye kampeni ndizo huwafanya wananchi wakione siochama bora nawao hukichangia kile kisichotoa hela ilikiweze kusimama huu ni mfano mmoja wapo wakuu.
   
 17. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #17
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  CCM has created the seeds of its own destruction.
   
 18. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #18
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  there happened to be greatest empires of all time(mali,songhai empires) and they did fall so to magamba it should act as a wake up call
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ni sahihi kabisa ila siyo kweli kwamba SLAA ni msafi kiasi hicho bali nia ana uwezo wa kwalaghali watanzania waliochoka na CCM na akaonekana kuwa safi, Kashfa zinazomkabili ni nzito sana tena zingine za ukweli kabisa, Watanzania tuna haja ya kutafkari sana kwani kunauwezekano mkubwa sana wa kubadilisha Kanzu Shehe akabaki kuwa yule yule. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Tanzania.
   
 20. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #20
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hii ya kupitisha harambee ya bakuli inaweza kuwa na gharama zake hasa pale wana-Arumeru wa chini kabisa hawataona kile walichokitarajia ndani ya miaka iliyobaki kabla ya uchaguzi wa 2015, ni mtihani kwa NASSARI na Kwa Chama kwa ujumla.
   
Loading...