CCM tuone soni, huku ni kujiharibia

CCM tuone soni, huku ni kujiharibia

Kuna watu wametuharibia chama, nasikitika sana, ila sikipendi kilivyo kwa sasa,mpaka kioshwe kiwe safi
 
Mnapozidi kuwekeza nguvu zenu kumtukana Lowasa ndipo wananchi wanaongeza nguvu kuichukia CCM.
Na mmesahau kuwa wananchi wa sasa si wale wa enzi za TaNU.
 
Wananchi Ukweli Ccm Hawaitaki Hasa Hii Style Mfano Kukatana Ndiyo Imeuwa Chama Siasa Chafu Halafu Wanatumia Pesa Kuchafua Upinzani Wakati

Vijana Wengi Ni Makachero Siri Zao Zinavuja Daily
 
Pole mzee tupatupa. Chama chako ndo kinatupwa sasa.
Angalia tu usije kuwa nabii wa chama chako kwa hilo jina lako
 
Siwezi kuvumilia jambo hili. Nami nasema hata kama wasikilizaji hawatakuwepo. Nasema ukweli ili uniweke huru. CCM inafanya siasa za maigizo, ulaghai na usanii. Hii si CCM tuliyoizoea. Hii si CCM yetu ya miaka ya Nyerere, Mwinyi na hata Mkapa. CCM hii inategemea zaidi propaganda kuliko ukweli. Inategemea vihoja badala ya hoja za haja. Kutwakucha, CCM imetingwa na propaganda. Tunapotea na kupoteza. Hakika hatutashinda uchaguzi huu na mwingine wowote kwa mipasho, kejeli, ulaghai na uzushi. Nianze na mgombea wetu wa Urais: Dr. John P. Magufuli. Ameahidi kuanzisha Mahakama ya Kupambana na rushwa na ufisadi. Kwakweli anashangaza na kudharau sheria zilizopo. Mahakama zipo. Sheria zipo. Majaji na mahakimu wapo. Tatizo utayari. Utayari wa kuwaburuza wahusika mahakamani. Ndani ya CCM na Serikali zake haupo. Afadhali angeahidi utayari tu. Si sheria wala mahakama. Halafu, kunafanywa kila mbinu na nguvu kuwaaminisha watanzania kuwa UKAWA/CHADEMA ni mafisadi kwakuwa wanao akina Lowassa, Masha na Sumaye. Imesemwa kuwa kwa kuwapokea hao,CHADEMA imehamisha choo kukipeleka chumbani. Ni kweli kuwa Lowassa, Sumaye na Masha, hata kama kweli ni mafisadi, ndiyo pekee ndani ya CCM na hivyo kuhama kwao ni kuhamisha choo chote? Inang'ang'aniwa kashfa ya Richmond, vipi kuhusu kashfa nyingine kama EPA na Escrow? Ifike mahali, CCM kama chama kinachopigania kutetea dola, kiache usanii na ulaghai. Siasa za sasa ni za kisasa na si kisasi. Kuendelea kujisafisha kisanii wakati huu wa uchaguzi ni usanii uliotukuka. Haufai wakati huu. Kama ni ufisadi, CCM ndiyo mama yake. Nasema hivi kwakuwa wala rushwa na mafisadi ni watu wenye mamlaka Serikalini. Nao ni makada wa CCM. Wao ndiyo waliozaliwa,kulelewa na kukua humo. Wapo wengi tu. Ni aibu kusingizia kuwa sasa wametoka na wamekwenda CHADEMA/UKAWA. Aibu sana. Kama kampeni hizi za Urais,Ubunge na Udiwani zinalenga kupata ushindi kwa kusafisha chama kutoka rushwa na ufisadi,CCM itakwama na haitatoboza. Kama tunalenga kutetea dola kwa hoja na kuonesha mafanikio ya kichama kwa utawala uliopita,tutafanikiwa. Tuache usanii! Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Mzee Tupatupa umeacha pia ile kauli ama agenda kuu ya wagombea wa CCM imempendekeza mwanamke ili akawe mshauri mkuu wa mambo ya wanawake. Swali hapa ndugu zangu mambo mengine ya maendeleo kwa jamii makamu wa rais kumba hatafanya kama ilivyo kwenye katiba?
 
Na je hatuoni kuwa hapa CCM imepotoka jamani kwa makamu wa rais kuwa mshauri wa mambo ya wanawake tuuuu? Mie nilidhani ni msaidizi wa rais
 
Masaburi akili yako iko matakoni. Eti huyo ni Dr? Wa falsafa au wa mifugo? kweli Taifa limepotea. Au ndio wa kienyeji kama Dr. Manyau.
 
Mzee Tupatupa, kilicho mwondoa Lowasa ccm siyo jitihada za chama kajisafisha bali matokeo ya siasa za makundi, pale JK alipo jiunga na kundi moja wapo na kuamua kulibeba. Kusinge kuwa na makundi , kuna uwezekano mkubwa Lowasa angekuwa ni mgombea uraisi kupitia ccm pamoja na kushiriki kwake ktk Richmond.
 
Mzee Tupatupa, inaelekea CCM hakuna waunda mikakati wenye akili kiasi nkwamba mbinu za kitoto kama zomeazomea kwa kulipa vijana, kuhonga waliokosa nafasi za uongozi kama Lipumba na Slaa. Kwa wenye akili leo kutumia ahadi na usanii kama wa akina Slaa siamini kama CCM inaonyesha ukomavu wa kuwa madarakani kwa miongo yote hii
 
Siwezi kuvumilia jambo hili. Nami nasema hata kama wasikilizaji hawatakuwepo. Nasema ukweli ili uniweke huru. CCM inafanya siasa za maigizo, ulaghai na usanii. Hii si CCM tuliyoizoea. Hii si CCM yetu ya miaka ya Nyerere, Mwinyi na hata Mkapa. CCM hii inategemea zaidi propaganda kuliko ukweli. Inategemea vihoja badala ya hoja za haja. Kutwakucha, CCM imetingwa na propaganda. Tunapotea na kupoteza.

Hakika hatutashinda uchaguzi huu na mwingine wowote kwa mipasho, kejeli, ulaghai na uzushi. Nianze na mgombea wetu wa Urais: Dr. John P. Magufuli. Ameahidi kuanzisha Mahakama ya Kupambana na rushwa na ufisadi. Kwakweli anashangaza na kudharau sheria zilizopo. Mahakama zipo. Sheria zipo. Majaji na mahakimu wapo. Tatizo utayari. Utayari wa kuwaburuza wahusika mahakamani. Ndani ya CCM na Serikali zake haupo. Afadhali angeahidi utayari tu. Si sheria wala mahakama.

Halafu, kunafanywa kila mbinu na nguvu kuwaaminisha watanzania kuwa UKAWA/CHADEMA ni mafisadi kwakuwa wanao akina Lowassa, Masha na Sumaye. Imesemwa kuwa kwa kuwapokea hao,CHADEMA imehamisha choo kukipeleka chumbani. Ni kweli kuwa Lowassa, Sumaye na Masha, hata kama kweli ni mafisadi, ndiyo pekee ndani ya CCM na hivyo kuhama kwao ni kuhamisha choo chote? Inang'ang'aniwa kashfa ya Richmond, vipi kuhusu kashfa nyingine kama EPA na Escrow?

Ifike mahali, CCM kama chama kinachopigania kutetea dola, kiache usanii na ulaghai. Siasa za sasa ni za kisasa na si kisasi. Kuendelea kujisafisha kisanii wakati huu wa uchaguzi ni usanii uliotukuka. Haufai wakati huu. Kama ni ufisadi, CCM ndiyo mama yake. Nasema hivi kwakuwa wala rushwa na mafisadi ni watu wenye mamlaka Serikalini. Nao ni makada wa CCM. Wao ndiyo waliozaliwa,kulelewa na kukua humo. Wapo wengi tu. Ni aibu kusingizia kuwa sasa wametoka na wamekwenda CHADEMA/UKAWA. Aibu sana.

Kama kampeni hizi za Urais,Ubunge na Udiwani zinalenga kupata ushindi kwa kusafisha chama kutoka rushwa na ufisadi,CCM itakwama na haitatoboza. Kama tunalenga kutetea dola kwa hoja na kuonesha mafanikio ya kichama kwa utawala uliopita,tutafanikiwa.

Tuache usanii!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Kwa hali ilivyo sasa kwa siasa za kupazana matope zimepita ni kumwaga Sera ili watanzania wapate matumaini lakini hakuna ukawa wanamwaga Sera tu mnampa wakati mgumu MAGUFULI yaani muhuni yeyote akiwa na neno anaongea tu ashakum so matusi je yule kipofu anaeipigia kampeni ccm atanifundisha nini wakati yeye haoni na kuona ni kuamini
 
usanii wao waendelee nao wanadhani wapiga kura ni walewale kama wa 2005 walioahidiwa maisha bora kwa kila mtu...usanii wa kufananisha mabadiliko yaliyotokea libya na tunayotaka watanzania ni usanii, kuvalisha vijana wa mtaani t-shirt za chadema , kujenga hospital ya rufaa kila mkoa ni usanii,

ni kweli tunaitaka ccm ijikite kuelezea uongo wake wa maisha bora kwa kila mtanzania iliuahidi mwaka 2005 badala ya kuhamisha hoja kutoka ile ya msingi. WAPIGA KURA MBUMBUMBU WAMEPUNGUA SANA KWA KIFAO NA WAMEIBUKA DIGITALI AMBAO HAWANJUI YUSUFU
 
Back
Top Bottom