VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Siwezi kuvumilia jambo hili. Nami nasema hata kama wasikilizaji hawatakuwepo. Nasema ukweli ili uniweke huru. CCM inafanya siasa za maigizo, ulaghai na usanii. Hii si CCM tuliyoizoea. Hii si CCM yetu ya miaka ya Nyerere, Mwinyi na hata Mkapa. CCM hii inategemea zaidi propaganda kuliko ukweli. Inategemea vihoja badala ya hoja za haja. Kutwakucha, CCM imetingwa na propaganda. Tunapotea na kupoteza.
Hakika hatutashinda uchaguzi huu na mwingine wowote kwa mipasho, kejeli, ulaghai na uzushi. Nianze na mgombea wetu wa Urais: Dr. John P. Magufuli. Ameahidi kuanzisha Mahakama ya Kupambana na rushwa na ufisadi. Kwakweli anashangaza na kudharau sheria zilizopo. Mahakama zipo. Sheria zipo. Majaji na mahakimu wapo. Tatizo utayari. Utayari wa kuwaburuza wahusika mahakamani. Ndani ya CCM na Serikali zake haupo. Afadhali angeahidi utayari tu. Si sheria wala mahakama.
Halafu, kunafanywa kila mbinu na nguvu kuwaaminisha watanzania kuwa UKAWA/CHADEMA ni mafisadi kwakuwa wanao akina Lowassa, Masha na Sumaye. Imesemwa kuwa kwa kuwapokea hao,CHADEMA imehamisha choo kukipeleka chumbani. Ni kweli kuwa Lowassa, Sumaye na Masha, hata kama kweli ni mafisadi, ndiyo pekee ndani ya CCM na hivyo kuhama kwao ni kuhamisha choo chote? Inang'ang'aniwa kashfa ya Richmond, vipi kuhusu kashfa nyingine kama EPA na Escrow?
Ifike mahali, CCM kama chama kinachopigania kutetea dola, kiache usanii na ulaghai. Siasa za sasa ni za kisasa na si kisasi. Kuendelea kujisafisha kisanii wakati huu wa uchaguzi ni usanii uliotukuka. Haufai wakati huu. Kama ni ufisadi, CCM ndiyo mama yake. Nasema hivi kwakuwa wala rushwa na mafisadi ni watu wenye mamlaka Serikalini. Nao ni makada wa CCM. Wao ndiyo waliozaliwa,kulelewa na kukua humo. Wapo wengi tu. Ni aibu kusingizia kuwa sasa wametoka na wamekwenda CHADEMA/UKAWA. Aibu sana.
Kama kampeni hizi za Urais,Ubunge na Udiwani zinalenga kupata ushindi kwa kusafisha chama kutoka rushwa na ufisadi,CCM itakwama na haitatoboza. Kama tunalenga kutetea dola kwa hoja na kuonesha mafanikio ya kichama kwa utawala uliopita,tutafanikiwa.
Tuache usanii!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam