CCM: Tumetumia Sh220mil, CHADEMA 600mil | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM: Tumetumia Sh220mil, CHADEMA 600mil

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mkirua vunjo, Mar 12, 2012.

 1. m

  mkirua vunjo Member

  #1
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]CCM: Tumetumia Sh220mil, Chadema 600mil [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 12 March 2012 09:49 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  Elias Msuya
  CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimetetea matumizi ya Sh220 milioni katika kura ya maoni kumpata mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mashariki, huku kikirejesha tuhuma za matumizi mabaya ya fedha kwa wapinzani.
  Utetezi huo wa CCM ulitolewa jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ambaye alipuuza tuhuma zilizotolewa na Chadema dhidi yao, akisema kuwa hadema ndiyo kimetumia fedha nyingi zaidi.
  Akizindia kampeni katika uchaguzi huo juzi, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema CCM imekiuka sheria na taratibu za matumizi katika mchakato mzima wa uchaguzi, kwa kutumia Sh220 milioni katika hatua hiyo ya awali, tofauti na maelekezo yanayowataka kutumia si zaidi ya Sh80 milioni.
  Mbowe pia alimtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa kutoa tamko juu ya CCM kukiuka Sheria ya Uchaguzi kwa kutumia kiasi hicho kikubwa cha fedha wakati wa mikutano miwili ya kupitisha mgombea wao wa ubunge.
 
“Tunamuomba Tendwa atoe tamko juu ya hili, kwani mkutano wa kwanza wa CCM walikuwa na wajumbe1,034 ambao kila mmoja alilipwa posho ya Sh50,000 na walitumia zaidi ya Sh100 milioni na mkutano wa pili ulikuwa na wajumbe1,044 ambao walitumia zaidi ya Sh120 milioni,” alisema Mbowe.
  Licha ya kukiri matumizi hayo, Nape amekigeuzia kibao chama hicho akisema kuwa kimetumia zaidi ya Sh600 milioni katika kura za maoni zilizowawezeasha kumpata mgombea wao.
  “Mbona wao (Chadema) wametumia zaidi ya Sh600 milioni, hamuwaulizi? Waulizeni Chadema kwa nini watumie fedha zote hizo, siyo kufuatilia tu fedha zetu” alisema Nape bila kufafanua madaia yake.
  Tofauti na madai ya Nape, Mbowe alisema kuwa chama chake kilikuwa na wajumbe 888 na kilitumia kiasi cha Sh6.2 milioni pekee kutokana na usafiri na chakula kwa wajumbe.
  Mchakato wa kumpata mgombea wa CCM, Siyoi Sumari ziligubikwa na mizengwe ambapo licha ya Siyoi kushinda kwa mara ya kwanza, kamati kuu ya CCM iliamuru kuwa uchaguzi huo urudiwe tena ambapo Siyoi alishinda tena.
  Wakati Chadema kilichomsimamisha Joshua Nasari wakizindua kampeni zao juzi, CCM waliomsimamisha Siyoi Sumari wanatarajia kuzindua kampeni zake leo ambapo Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa ndiye atakuwa mgeni.
  Akizungumzia maandalizi ya kampeni zao, Nape alisema kuwa watafunika kampeni za Chadema.
  “Kwa nini tuandikie mate wakati wino upo, nyie mtaona kesho (leo) itakavyokuwa. Tutafunika tu,” alisema Nape.
  Licha ya Chadema na CCM vinavyoonekana kuwa na wafuasi wengi katika jimbo hilo, vyama vingine vilivyosemamisha wagombea ni pamoja na TLP, SAU na UDP.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. only83

  only83 JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana na wewe huyu jamaa anahitaji msaada wa haraka kwa wataalamu wa akili na magonjwa ya akili..hayuko sawa kabisa.
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Mar 12, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Mbona ameshindwa kufafanua CHADEMA walitumiaje hicho kiasi?
  CHADEMA wamefafanua jinsi 220mil zilivyotumika, ukiacha mbali mabilioni ya Lowassa yaliyotumika kumpitisha Siyoi
   
 4. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hivi hapa Jamvini huwa hawafanyi IQ test?
   
 5. Ishina

  Ishina Senior Member

  #5
  Mar 12, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nape amekubali kuwa chama chake cha Magamba kimetumia Sh. 220 milioni, wakati Mwigulu alijibu hapa juzi kuwa Magamba walitumia Sh. 22 milioni...!!:crazy: Naona waanaanza kuweweseka na kila mtu anaibuka kivyake! Leo kwenye uzinduzi wa kampeni tutasikia data zingine tena. :violin:
   
 6. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Duh.. cijawahi kucikia chama cha upinzani kikatumia hela nyingi kiasi hicho kwa uchaguzi mmoja wa ubunge.. Ndo itakuwa leo chama makini kifanye hayo..? Hatutaki kuona magari ya serikali kwenye kampeni..
   
 7. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Mwigulu kaumbuka,Nape kakubali kwamba wametumia mil220 wewe unasema mil22 haaaaaa Jipange upya mwigulu.
   
 8. Jamani mbona si poa

  Jamani mbona si poa Member

  #8
  Mar 12, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndo tunajadili hivyo matumizi makubwa namna hii ya chama chetu.
   
 9. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #9
  Mar 12, 2012
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hahahaaah ni hatari sana huyu dogo, akili yake inawaza kikarumekenge

  [​IMG]
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  must be sick.... anajustify kosa kwa kuassume kosa la mwenzake??

  this guy needs serious medical attention
   
 11. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Ukuwa mwanachama au mshabiki wa CCM lazima utakuwa unapata deterioration of brain cells!!

  No wonder huwa wanatyoa kauli za kupishana
   
 12. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,984
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  kuna ubaya gani ccm ku2mia hela hz? Wakati kina ofisi na magari ambayo ni lazima itumike pesa kuyaendesha, tofauti na cdm ambacho hakina hata ofisi wakati wanapokea ruzuku kutoka serikalini wanazipeleka wapi? Wanagawana wakubwa wao huku wakijidai kuwachangisha wananchi kwa bakuli tena bila risiti c ni wizi wa mchana tena huo? Tunajuwa target yao hawana lolote.
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  soma sheria ya uchaguzi....

  Mnambowa ni jina zuri kwelikweli.... limekaa ki-pemba ki-pemba hivi
   
 14. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Mwigulu is an opportunist dog who eats whatever food crumbles that fall from CCM Table.
  He feeds in lies, his survival depends on how much he lies.
  He knows for sure that he has staffed his bell from ravish hyena fist in Arumeru hosted by CCM, to bend the truth he is down scaling the fiesta.

  Shame on You Mwigulu.   
 15. S

  STIDE JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nauliza tu, wanaoshabikia MAGAMBA wana ubongo wa namna gani ikiwa viongozi wao ndo kama hawa akina Nape na Mzinzi Mwiguru
   
 16. t

  thengoshahimself Member

  #16
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamaa mrembo mmoja ajitokeze mgumu aweke hii toto ndan wapemba mko wap.plz chukua hii toto nzur sana
   
 17. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #17
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Ukubwa wa kichwa si wingi wa akili,akili ni nywele kama wewe unakipara imekula kwako la sivyo azima nywele za kw pan au zivu mkuu
   
 18. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #18
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Wewe lazima utakuwa ****, kama kusoma huwezi hata kusikia napo husikii?? Unahitaji maombi ya ziada? Unajua sheria za uchaguzi ambazo Mwenyekiti wa magamba alisaini kwa Mbwembwe pale magogoni zinasema nini? Kama hujui muulize Nepi
   
 19. Ishina

  Ishina Senior Member

  #19
  Mar 12, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Inavyoonekana HUJUI hata nini unachoongea au ni hoja gani inayojadiliwa hapa...!! upo nje ya mstari - hebu jipange upya ndo uje uchangie hapa:cool2:.
   
 20. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #20
  Mar 12, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0

  CHADEMA wajibu hili kwa kukubali au kukataa na watoe ufafanuzi kwamba fedha zilitumikaje.
   
Loading...