Chama Cha Mapinduzi, CCM kimesema kina uhakika wa kushinda majimbo yote mawili na kufanya vizuri katika kata zenye uchaguzi mdogo kwa uwazi, haki, amani na demokrasia.
Wamejinasibu kuwa rekodi yao ya utendaji ndani ya serikali katika kutatua kero za wananchi, utoaji bora wa huduma za kijamii, kuimarika kwa uwajibikaji serikalini kwa watumishi na watendaji wake kunawapa jeuri ya kuchukua majibo yote.
Wamewataka wananchi kuachana na vyama vya upinzani kwani hata bajeti kuu ya serikali iliyojaa mipango na miradi ya maendeleo katika maeneo yao waliipigia kura ya hapana hivyo hawana bajeti ya kuwaletea maendeleo badala yake waiunge mkono CCM ambayo ndio yenye serikali inayosimamia utekelezaji wa bajeti ya maendeleo.
"Hatuna mashaka, CCM tutashinda mapema tu tena ushindi wa heshima." alisema moja ya viongozi wa chama hicho.