CCM: Tumejiandaa kushinda Ukonga na Monduli

MASIGA

Senior Member
Aug 29, 2015
130
281
Chama Cha Mapinduzi, CCM kimesema kina uhakika wa kushinda majimbo yote mawili na kufanya vizuri katika kata zenye uchaguzi mdogo kwa uwazi, haki, amani na demokrasia.

Wamejinasibu kuwa rekodi yao ya utendaji ndani ya serikali katika kutatua kero za wananchi, utoaji bora wa huduma za kijamii, kuimarika kwa uwajibikaji serikalini kwa watumishi na watendaji wake kunawapa jeuri ya kuchukua majibo yote.

Wamewataka wananchi kuachana na vyama vya upinzani kwani hata bajeti kuu ya serikali iliyojaa mipango na miradi ya maendeleo katika maeneo yao waliipigia kura ya hapana hivyo hawana bajeti ya kuwaletea maendeleo badala yake waiunge mkono CCM ambayo ndio yenye serikali inayosimamia utekelezaji wa bajeti ya maendeleo.

"Hatuna mashaka, CCM tutashinda mapema tu tena ushindi wa heshima." alisema moja ya viongozi wa chama hicho.
 
Waasisi wa ukaburu hamuwezi kushinda kwa haki kamwe. Serikali yenye bajeti maana yake ni nini? Mbunge anaruhusiwa kuanzisha TRA ya jimbo lake ili aweze kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye jimbo analowakilisha?

Mbunge ni mwakilishi wa interests za wananchi wa jimbo lake. Kama serikali haitaki kurudisha kodi waliyokusanya kwenye maeneo sahihi badala yake wanapanga bajeti ya KIKANDA NA KIKABURU kwanini mbunge alazimike kupiga kura ya ndiyo?

Kununua wabunge tu ni kosa ambalo halitasameheka milele kwa CCM. Badala ya kutumia fedha za kodi zetu kujenga na kukarabati miundombinu hasa jimbo la ukonga mmezitumia kumnunua mbunge kisha mnaenda kuwaambia wananchi mpaka wawachague ndio mkakarabari barabara na kupeleka maji. Mngeacha pia kukusanya kodi wananchi wajiendeleze wenyewe.

CCM ya makaburu haioni aibu kupora hadi fedha za korosho za wananchi maskini na kuzielekeza kwenye ukanda. Japokuwa bado tuna jamii isiyopenda kufikiri na kuhoji, angalau wenye kujielewa wameona wajitenge na huu upuuzi. (Hongera Hawa Ghasia).

CCM ya makaburu.
 
tulijua itashinda hata kabla hamjasema. siyo habari mpya.
 
Tume ya Uchaguzi + Jeshi la Policeccm +Wakurugenzi = CCM 'Ushindi ni lazima.
 
ni kweli watashinda kwa msaada wa polis wa siro na tume ya uchaguzi. wanahangaika kuongeza vutuo vya kupigia kura. ccm kushinda kwa haki ni ngumu.
 
Back
Top Bottom