CCM - the Tanzanian's Grand Old Party (GOP)

President Elect

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
689
208
CCM ndio chama kikubwa na kikongwe zaidi nchini Tanzania - Grand Old Party (GOP).

Je CCM imefeli katika kuzikonga nyoyo za wananchi wetu wazalendo wa Taifa hili? Kama jibu ni 'ndio', basi uongozi wa juu una wajibu wa kulijua hilo na kurekebisha hali ya mwamko wa siasa ili kugusa dhamira na matakwa ya wananchi, huku wakifahamu wananchi wanataka nini.

Kama jibu ni 'sio', basi isibweteke, bali iongeze juhudi zaidi katika kulinda mafanikio yaliyoletwa na CCM kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa letu la Tanzania.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi!
 
change123

Member
Oct 8, 2010
65
23
Jibu ni NDIYO, CCM wanafahamu sana matakwa ya wananchi, lakini kutokana na ubinafsi na ufisadi
uliokidhiri wamefunga macho na masikio. Viongozi karibu wote wa ngazi za juu ni mafisadi
hakuna wa kumhukumu mwingine. Inakuwaje kiongozi anatuhuma nzito lakini hawajibiki wala kuwajibishwI?
Uswahiba umezidi, kujivua GAMBA imekuwa ni sawa na '"love story''''.
Chama hiKi kimedhihirisha kwa umma hakiwezi kufanya maamuzi MAGUMU.

Tuombe MUNGU kiporomoke tupate angalau watu/chama chenye taste mpya ya maendeleo. sio CCM wanao
tudanganya bado tuko kwenye mfumo wa UJAMAA NA KUJITEGEMEA, wakati viongozi wake ambao hata hawajawahi
kufanya biashara ya nyanya ni ma-billionare.

KISIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
President Elect

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
689
208
Kuporomoka, kufa, kuvunjika, au kusambaratika kwa CCM ni wazo hasi. Wazo chanya ni CCM kuwa imara zaidi na kusimamia serikali yetu kwa umakini zaidi.

Kubadili uongozi wa juu kabisa; Mwenyekiti wa Taifa, Makamu wake na Katibu Mkuu, ndio njia chanya ya kutuvusha kutoka hapa tulipo.

Kama Thabo Mbeki angeng'ang'ania uenyekiti, serikali ya ANC ingeondolewa madarakani na upinzani, lakini alipomwachia Jacob Zuma, ANC ilipeta kwenye uchaguzi mkuu.

Hivyo basi, endapo JK hataachia uenyekiti wa chama mwaka ujao, CCM itakuwa na hali ngumu sana 2015.

Namsihi sana Mwenyekiti wa CCM Taifa asigombee cheo hicho mwakani, ili tuwe na 'check & balance' kwa serikali yetu.
 
Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,890
2,617
CCM ndio chama kikubwa na kikongwe zaidi nchini Tanzania - Grand Old Party (GOP).

Je CCM imefeli katika kuzikonga nyoyo za wananchi wetu wazalendo wa Taifa hili? Kama jibu ni 'ndio', basi uongozi wa juu una wajibu wa kulijua hilo na kurekebisha hali ya mwamko wa siasa ili kugusa dhamira na matakwa ya wananchi, huku wakifahamu wananchi wanataka nini.

Kama jibu ni 'sio', basi isibweteke, bali iongeze juhudi zaidi katika kulinda mafanikio yaliyoletwa na CCM kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa letu la Tanzania.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi!
.

RED Tafadhali rekebisha, umeanzia kombo. Umetumia kigezo gani kusema ccm ni chama kikubwa Tz? Pili, ni mantiki gani umetumia kukilinganisha na vingine ktk umri i.e. ukongwe....maana kabla ya kuruhusiwa kwa hiana kuanzishwa kwa mfumo wa siasa ya vyama vingi ccm kilikuwa chenyewe tu. Kwa hiyo kutumia neno "ukongwe" maana ya umri sio mahala pake kama hoja ni levelled comparability. Unalinganisha vipi kutokwepo na kuwepo?

Kwa upande mwingine sasa, kuwepo kwa ccm na utawala wao/wake kwa Tz kwa miaka yote 50 kumekuwa ni balaa, janga na mzigo wa kila MTz mpenda haki, amani na maendeleo.

Mafanikio ya ccm ni haba sana, ya kulaghai na ambayo kwa ufupi ni aibu tupu. Wewe jaribu kufikiria rasilimali watu, maliasili na jiografia ya Tz kama vingetumika angalau 10% Tz leo ingekuwa wapi. Muda ambao walipewa (afforded) ni mwingi sana. Jiulize uwe na miaka 50 halafu uitwe mtoto .....je hilo sio tusi na udhalilishaji mkubwa?

Unajua ktk lugha kuna tofauti ya maana & matumizi ya maneno mbalimbali; sasa ccm wao kudumaza hii nchi hukuita amani, utulivu & maendeleo! Yale mambo waliyotuimbisha zamani mashuleni ya maadui wa Taifa ni hadithi maana hao maadu si tu kuwa bado wapo bali wameongezeka wingi na uwezo. ccm walisema ni vita sasa wameshindwa na hao maadui vibaya sana basi wakiri na kujisalimisha.

Fikisha ujumbe kwao kuwa, the only thing we want now is CCM OUT!!!
 
Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
CCM ndio chama kikubwa na kikongwe zaidi nchini Tanzania - Grand Old Party (GOP).

Je CCM imefeli katika kuzikonga nyoyo za wananchi wetu wazalendo wa Taifa hili? Kama jibu ni 'ndio', basi uongozi wa juu una wajibu wa kulijua hilo na kurekebisha hali ya mwamko wa siasa ili kugusa dhamira na matakwa ya wananchi, huku wakifahamu wananchi wanataka nini.

Kama jibu ni 'sio', basi isibweteke, bali iongeze juhudi zaidi katika kulinda mafanikio yaliyoletwa na CCM kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa letu la Tanzania.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi!

Wewe maoni yako ni nini? Si unaishi humu humu nchini?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom