CCM sijikanyage, mnaongoza kwa kukiuka katiba yenu.

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,109
2,000
Mnalilia suala la kuchaguliwa kwa Mh Msigwa kuiongoza kanda ya Nyada za juu kusini kunawahusu nini? Mnataka kulazimisha wachaguliwe mnaowataka ninyi ili ya nyuma yajirudie sio? CHADEMA ni makini zaidi ya mjuavyo ninyi endeleeni kupotosha. Kamwe hutuwezi kuweka watu ambao mna maslahi nanyi, haiwezekani. Mkiona mtu aetenguliwa mjua kuna tatizo.


2015, kwenye kura za maoni kule DODOMA mbona ninyi wenyewe mlilia baadhi ya makubwa wenu kuingia na wagombea wao mifukoni? Hilo hamkuliona? Mbona aliyekubalika na wengi mlimkata? Kama ilikua ni kwa maslahi maana ya CCM basis na msigwa nae kachaguliwa kwa maslahi mapana ya chama tena kwa kura nyingi.

Mkiambiwa ninyi ni waongo na wasahaulifu mnasema kua wapinzani ni wakorofi,ya watu mnayadandiaje? Yanawahusu ninyi? Wenyeviti wangapi wa CCM wa mikoa wanabebwa bebwa tena tunaona kabisa. Mh Msigwa kapita kwa kura nyingi kuliko zilizomkataa.Mnakuza mambo hata kwa kitu kidogo ambacho hata kwenu hakini maslahi yeyote zaidi ya kupotea muda tu.
 

Ongata

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
525
1,000
Waambie,hawajui mwakani kuna njaa nchi nzima badala ya kutunza hela kuwanunulia wale waliowapa tisheti zile za korijo chakula wameakalia chadema,wamehama kwa Lema na Ben sasa wako kwa Mbowe watu wa hovyo kweli,wakati kuwapa mkopo kumewashinda
 

Kingsharon92

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
6,707
2,000
Kwa hiyo sasa hivi mnaishi kuenenda na ccm wanachofanya ama kweli usilolijua litakusumbua iwapo hutathubu kulifanyia kazi
 

simon mato

JF-Expert Member
Sep 27, 2015
926
500
Msikimbie kuunga unga hizi viumbea mjibu maswali mliyopewa!!! Mnajinasibu kuwa wanademokrasia je ni kweli hiyoo demokrasia mnaipractise ndani ya chama au "MNAABUDU SANAMU YA MTU"???

Kwahyo P. Ole Sosopi ni amekuwa msaliti anatumiwa na CCM ndio maana kakatwa siku ya uchaguzi??
Usikimbilie kuandika huaro kama hii JF chukua mda wako fikiria kwa makini uje na majibu yanayoridhisha!!!
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,930
2,000
Tena kuna tofauti kubwa katika vyama hivi. Ukiona uongozi wa juu wa ccm unashinikiza uongozi kwa mtu fulani ujue sio kwa maslahi ya chama bali katika kulinda maslahi ya wachache ndani yake.
Tofauti na Chadema ni kuwa, wanachama wanaweza kumtaka sana mtu fulani aliyewashawishi kuwa anawafaa lakini uongozi wa juu ukatumia veto kuweka mwingine, basi ukiona hivyo inteligensia ya chama imegundua ushawishi wa mtu huyo anayependwa na wanachama ni kwa vile hawamjui kuwa nyuma yake wapo kina nani. Wengi wao nyuma yao wako wanaccm wenye malengo mabaya na Chadema hivyo wanataka aingie ili avuruge au wanamjua kuwa ni dhaifu hawezi kuwapa shida.
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,777
2,000
Toka lini panya anamshauri paka, ccm ni ukoo wa panya tu wasubiri kuliwa maana hakuna namna
 

Iceman 3D

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
20,629
2,000
Ikiwa demokrasia ni somo basi CCM wanapata 3℅ CDM 13%, sasa ni ujinga kujisifu kumzidi mwenye 3% kwa kuwa wewe una 13% unasahau kuwa wote mna F, you guys are still worse in democracy within your party, na kujilinganisha na CCM hakuwasaidii.
Wakati mna fanya kazi kubwa ya kutuonesha kuwa CCM ni mbaya mna shindwa kazi ndogo ya kutuonesha kuwa CDM ni nzuri.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom