Wadau CCM sasa imeamua kuimaliza CHADEMA.Habari za wabunge wake walioshindwa kwenda mahakamani kupinga ushindi wa wabunge wa CHADEMA si habari njema hata kidogo.Mahakama yetu kama inavyofahamika si huru sana.Rejea hukumu ya mgombea binafsi.Kwa taarifa tu ni kwamba mpaka sasa zaidi ya nusu ya wabunge wa CHADEMA wamepingwa mahakamani.Kiongozi wa upinzani bungeni MBOWE amepingwa,Ndesamburo amepingwa,Lema amepingwa,MR TWO amepingwa,HALIMA MDEE amepingwa na wengineo wengi.Huu unaoenekana ni mkakati maalum wa kuitumia mahakama kuwavua ubunge.Wanajamii tujadili hili na tuwape ushauri viongozi wetu wa CHADEMA wafanyeje?????