CCM sasa kuiangamiza CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM sasa kuiangamiza CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Dec 30, 2010.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Wadau CCM sasa imeamua kuimaliza CHADEMA.Habari za wabunge wake walioshindwa kwenda mahakamani kupinga ushindi wa wabunge wa CHADEMA si habari njema hata kidogo.Mahakama yetu kama inavyofahamika si huru sana.Rejea hukumu ya mgombea binafsi.Kwa taarifa tu ni kwamba mpaka sasa zaidi ya nusu ya wabunge wa CHADEMA wamepingwa mahakamani.Kiongozi wa upinzani bungeni MBOWE amepingwa,Ndesamburo amepingwa,Lema amepingwa,MR TWO amepingwa,HALIMA MDEE amepingwa na wengineo wengi.Huu unaoenekana ni mkakati maalum wa kuitumia mahakama kuwavua ubunge.Wanajamii tujadili hili na tuwape ushauri viongozi wetu wa CHADEMA wafanyeje?????
   
 2. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #2
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wape muda hao CCM, kwa nini CHADEMA wawe na wasiwasi wakati wapigakura wako upande wao??
   
 3. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,876
  Trophy Points: 280
  Hata Dr. Slaa alipingwa mahakamani mwaka 2005, lakini alishinda kesi. Waache waende wakarudishe kodi zetu kwenye gharama za kesi.
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Dec 30, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,593
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Topic nzuri mkuu,

  Kupinga ni siasa tu, umesahau ngumi za utotoni ukishindwa unakimbilia kuuma!

  mimi naona hao wana-CCM wanatapatapa tu

  However, is high time kwa viongozi wa CDMkuwa kitu kimoja, na kuleta 'chachandu' za kisiasa kuwapa taarifa hao mahakimu kuwa CDM ni ya wananchi. Tatizo ni kuwa ndani ya CDM hivi sasa (japo hawataki tuseme) ni wabinafsi na vimi-gogoro vya kitoto toto tu na vya mwaka 47 vikiongozwa na Slaa, silent killer wa chadema, ambaye walidhani angefaa kuwa rais. Slaa ameshindwa kuweka bifu lake na wivu wake mfukoni yeye kila kukicha anawaza jinsi gani ya kushindana na baadhi ya watu fulani ndani ya CDM, ana chuki sna huyu mtu na persnally hafai kwenye ile position. umri wake, uwezo wake, elimu yake ilitosha kabisa kukijenga chama na hasa kutumia vijana kupeleka CCM mchakamchaka

  For those cases, yes CDM iko kwenye wakati mgumu na members wengi huwa hawaemi haya, huwa wanasubiri matokeo ya kesi kama ilivyo Dowans, wao wakilala na kuamka wanawaza kuwasema watu fulani ndani ya CDM!!!

  WHAT SHOULD BE DONE

  1. Ile stand/ mismamo wa kuwa Slaa alishinda ulitakiwa na unatakiwa utafutiwe ufumbuzi kuendeleza kulisemea hilo! hata kama si kweli!! kwenye siasa no retrat point za eti busara hatutaki kumwaga damu ni za kijinga, CCM kila siku wanamwaga damu tu

  2. Nimesema chachandu za kisiasa, to digress those cases is easier kama CDM itatafuta kupata attention ya wananchi kwa namna nyingine kulingana na hali ya kisiasa,nimesikia kuna maandamano ya kupinga bei ya umeme..thats excellent we should be having many similar dances, wakati mwingine matokeo ya kesi yanaendana sana na wananchi wanatakaje sio physics ile!!

  3. Weekeni occasion moja kuonyesha kuwa nyie ni kitu kimoja na mna lengo moja na sio wengine wafanyabiashara

  4. Tengenezeni uwezekano wa kibusara ku-reconciliate na vyama pinzani, hata kama mioyoni mwenu mmeishawa-ignore at least kitawapa ahueni. Ni kweli kampeni za Halima mdee hazikuwa na ki-busara sana hasa kuporomosha matusi kwa Mbatia, hata kama mtatetea hiyo ilikuwa wazi na haikuwa na ulazima as far as those campaigns concerned! what for hata kama Mbatia ni mgomvi!! same issue za matusi tulizisikia live kwenye TV!! Slaa shahidi!

  5. I will always tell you, politics is all about games and the winner smiles

  I believe CCM hawawezi kushinda hizi kesi, na ikitokea ni disaster na kutotokea kwa hilo ni CDM kujipanga tu

  mtoa hoja, kila issue huwa inamaliziwa mahakamani!! CDM haitaki kujenga huu utamaduni na inaleta maswali mengi kwa watu wachache !!
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Peoples Power hata wakienda mahakamani, sisi hatuitaki CCM full stop. Katiba ibadilishwe, iandikwe MPYA, 2015 CCM BYE BYE!!!!
   
 6. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Usiwe na wasiwasi wapiga kura tupo imara!CHADEMA itaendelea kushinda tu!!
   
 7. F2S

  F2S JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2010
  Joined: Feb 16, 2008
  Messages: 216
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mafisadi watatumia nafasi hizo kuihonga mahakama kama kawaida yao since pesa wanayo na nyingine inaingia kupitia hukumu ya Dowans. This can happen yaani CDM kikapoteza viti Bungeni. Yatakuwa maigizo. My Stand ni kwamba vyama vya upinzani shirikianeni na wananchi ili kwa pamoja tuondoe ufisadi then haki itapatikana kwani kwa ufisadi uko juuu ya sheria hapa bongo. Balali alikuwa pronounced dead ili tu sheria isishike mkondo wake na mpaka leo yule ni mzima anakula kuku ughaibuni. Kesi chungu nzima zinapindishwa kuwapa ushindi mafisadi inauma sana. Nafikiri maandamano ni njia pekee ambayo wananchi kwa pamoja tutakuwa tuaonesha hisia zetu ktk mambo haya yanayotuumiza na kukosa imani na Serikali. Maana ukisubiri uchaguzi wa 2015 mambo yatakuwa haya haya au saana kama Ivory cost uchaguzi utachakachuliwa tu hata hii 2010 hawakushinda asilani ni mpango mzima wa usalama wa Taifa tu. Huwa nashangaa eti tuiachie mahakama itatoa maamuzi kwani wao miungu hawahongeki tena ndo wanaoongoza kwa rushwa. Hata Mungu atatuchoka sasa na kutuondolea amani kwa mtindo huu maana hata nchi zilizopigana wao kwa wao ni mambo haya haya ya kudhulumu the majority. Inauma sana
   
 8. N

  Nonda JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Huu ushauri ni mzuri pia ni kwa manufaa yao wakiupokea na kuutekeleza.

  Hapa JF tegemea kurushiwa madongo.
  watu wanaona chama cha upinzani ni kimoja tu....au waki-rephrase watasema Chama cha upinzani cha kweli.

  Upinzani una safari ndefu!!1
   
 9. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #9
  Dec 30, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Si mtakumbuka Makamba aliwaambia wale wote walioshindwa wakate rufaa chama kitasaidia!? Hata kama wameshindwa kihalali?
  Halafu hizi kesi zitachukua miaka 3-4 au hata mitano kama zingine,vinginevyo mmmh.
   
 10. semango

  semango JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mfa maji...................!
   
 11. s

  smz JF-Expert Member

  #11
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM hawataki kushindana, wanataka waachiwe dola milele. Makamba huwezi kuamrish eti wale wote walioshinwa kwenye nafasi zao waende mahakamani, na ccm itawasaidia!! Maana yake nini??

  Inawezekana kabisa wapo wenye sababu za msingi za kwenda mahakamani, waache waende. Lakini kusema wote waende kwa amri ya Makamba, hiyo siyo sahihi. Wanataka mlundikano wa kesi zisizo na msing kwenye mahakama zetu na mwisho wa siku wachakachue. Let's wait and see. Maana Makamba anaonekana ndo kila kitu, Mwanasheria yeye, Katibu mkuu yeye
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Dec 30, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kumekucha
   
 13. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #13
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Kama CDM watafanya yaliyotarajiwa na wananchi katika kipindi hiki hadi hapo hukumu zitakapotolewa hapana shaka wananchi watawarudishia majimbo hayo hata kama wabunge wa sasa watazuiliwa na mahakama kutetea nafasi zao.

  Huu uvundo tunaousikia ndani ya CDM kila kukicha si wimbo mzuri saaana. Pengine Waberoya kaja na wazo jema kwamba wafanye jambo kuonyesha umma kuwa wao ni wamoja kuliko wakati wowote ili kuwin support ya watanzania.
  Niliwahi kusikia kuwa Rais wa 3 wa URT hakuwa in good terms na wife wake lakini iliwalazimu kuonekana kitu kimoja machoni pa watanzania. Nadhani CDM wanapaswa kujua kwamba wana wajibu wa kuwaunganisha watanzania. Kuwa chama kikuu cha upinzani si swala la kujivunia au sifa fulani bali ni ishara ya wajibu mkuu.
  Nyerere alipata kusema uRais ni mzigo kama ambavyo kuwa chama chenye kubeba tumaini jipya ilivyo mzigo mkubwa!!!!!!
   
 14. L

  Lapton2005 Member

  #14
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo marope anampango wa kulipafaini kwa kila kesi na hapo kunufaisha chadema na yeye mwenyemwe kutildoliwa. Mjadala mlefu wanini. Wapigakura ndio sisi tuliowachagua hao wabunge tajwa. Hakuna cha taratibu hapa ni nguvu ya watu ndio muamuzi, Mh rais alithibitisha haya katika ufunguzi wa bunge. "Wengine waliwasahau watu wao, wamepata hasira na kuwaadhibu kwa kura". Yaani hawa ni wakina gbagbo wanaotaka wao wawe viongozi milele. Watz sasa mabadiriko ni lazima.
   
Loading...