CCM Rukwa yataka Kanisa litubu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Rukwa yataka Kanisa litubu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 29, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280

  CCM Rukwa yataka Kanisa litubu

  Imeandikwa na Peti Siyame, Sumbawanga; Tarehe: 28th December 2010 @ 23:53

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Rukwa, kimewataka baadhi ya viongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga walioonesha kushabikia baadhi ya vyama vya siasa wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu, wasitumie nafasi ya Kanisa hilo kuwatenga na kuwawekea pingamizi waumini wao, hasa wanaCCM.

  Rai hiyo ilitolewa juzi usiku mjini hapa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete katika hotuba yake kwenye hafla ya kuwapongeza Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini kwa tiketi ya CCM, Aeshy Hilaly na Meya wa Manispaa hiyo, Samweli Kisabwite, kwa kuchaguliwa kushika nafasi hizo.

  Kauli ya Mwenyekiti huyo inatokana na mgongano wa kiimani unaolihusisha Kanisa hilo na baadhi ya waumini wao ambao wengi wao ni wanaCCM, uliochochewa na kile Kanisa hilo kinachoeleza kauli za kufuru dhidi ya Utatu Mtakatifu wakati wa Uchaguzi Mkuu, likidai baadhi ya wagombea walikufuru imani ya Kanisa hilo kwa kujifananisha na Yesu Kristo mwana wa Mungu katika dhana ya mafiga matatu.

  “Kwa kuwa makanisani ni mchanganyiko wa waumini wenye itikadi za vyama mbalimbali vya siasa na wale ambao hawana itikadi hizo, bila shaka wapo baadhi ya viongozi wa kanisa wa ngazi mbalimbali ambao wana itikadi za vyama ambapo wengine walikuwa mawakala wa vyama vyao wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita.

  “Nashauri watu wa namna hiyo wasitumie nafasi zao za Kanisa kuwatenga na kuwawekea pingamizi zisizokuwa na msingi wa itikadi ya vyama vyao na hasa kwa wanaCCM wanaotaka kujipatanisha na kanisa lao,” alifafanua Mwenyekiti Matete.

  Alisisitiza kuwa kutengwa kwa baadhi ya waumini na kanisa hilo na wengine kuwekewa pingamizi, lisitafsiriwe kuwa ni fimbo ya kudhoofisha nyoyo za wanaCCM na mashabiki wao, kiasi wakashindwa kujiunga na CCM kwa hofu ya kutengwa au kuwekewa pingamizi, kwani chama kitaendelea kujengwa na kuwa imara.

  “Bahati mbaya Kanisa Katoliki liliingia kwenye mgogoro na baadhi ya waumini wake, ili tuendelee kuwa na amani, nawaomba kuliacha kanisa na waumini wake…sisi ambao si waumini wa kanisa hilo ni vizuri tukanyamaza ili tusichochee uchochezi.

  Wahenga walisema ya Ngoswe mwachie ngoswe mwenyewe,” alisema.

  Aidha, alitumia fursa hiyo kuwaonya baadhi ya watu wanaowanyang’anya na kuwapora wanachama wa CCM wanapowakuta mitaani wakiwa wamevaa mavazi ya chama hicho, akisema vitendo hivyo vinaashiria uvunjifu wa amani na mshikamano uliokuwepo tangu zamani.

  Naye Mbunge wa zamani wa Jimbo la Nkasi, Posian Nyami alitumia vifungu vya Biblia Takatifu juu ya msamaha na kuondoa makundi huku Mbunge Hilaly akitaka kutoangalia uzuri wa jalada la kitabu kabla ya kusoma.

  Akizungumza hivi karibuni na vyombo mbalimbali vya habari mjini hapa, Wakili wa Kiaskofu; kwanza alikiri kutengwa na kuwekewa pingamizi baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki jimboni hapa, kwa kuwatenga wanaodaiwa kuisaliti imani yao kwa kufanya kwa kukufuru utatu mtakatifu na kukashifu msalaba.

  Hata hivyo, Kasisi huyo alipinga shutuma zinazotolewa dhidi ya kanisa hilo kwa madai kuwa limewatenga na kuweka pingamizi sababu ya itikadi za siasa kwa kukipigia kura chama tawala au sababu za udini.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280
  Hivi hawa wakosefu hawaoni waombe msamaha tu yaishe badala ya kutingisha kiberiti na kanisa...................vinginevyo waanzishe kanisa lao..........
   
 3. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hivi kutengwa na kanisa kumehusianishwa vipi na CCM? Hivi watu wengine mbona wanatumia vibaya majukwaa yao?
   
 4. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu soma post ya iliyotangulia, inayosome hivi " waumin wa RC watubu" hapo ndipo utaona udini wa waziwazi. najua thread ilikuwa ndefu lakini jitahidi kuspear some time ili uisome yote then will understand. (Niukweli usio na kificho kuwa kanisa lilipigia kampeni chadema, hatusemi slaa kwani yeye alikuwa hahubiri udini ila makasisi wa kanisa ndo tatizo kwenye hilo sakata.
   
 5. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,737
  Likes Received: 3,170
  Trophy Points: 280
  Waombe msamaha wa nini bana kwani wao nani?? CCM ianze kutubu kabla makanisa hajaanza kutubu. Hiviiiiiiiiiii mbuzi zinafugwa wapi wajameni na Kondoo jee naomba kujuzwa kwa hili.
   
 6. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #6
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kumbe kanisa ni nani hasa??? Kwi!! kwi!! kwi! kwi!

  CCM peleka hizo siasa zako za UCHAKACHUAJI huko kwingineko majukuani na wala si hapa kwetu, kwi kwi kwi!!! Hata siku moja 'Jumba la Baba yangu aliye juu mbinguni haliwezi kugeuzwa PANGO LA WANYANG'ANYI. Kwi kwi kwi

  Na shangaa wala haujiulizi hata maaskofu wala hana ubavu kuniingilia katika hili maana huku kanisani ndiko pekee sehemu ambako FISADI mwenye mamilioni na masikini wote ni wamoja, cheo kimoja cha uumini na mtoto wa Baba yangu juu mbinguni basi.

  Pesa hainunui kila kitu ndugu CCM, kwi kwi kwi!!!
   
 7. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo Hilaly kweli anajua kiaarab au aliangalia jalada tu. Kwa hiyo ndani ya Biblia Takatifu anasema ni hovyo au mimi sikumwelewa? Nafikiri amezidi kutukana dini yetu!
   
 8. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nilisoma posting fulani humu iliyonakili gazeti lililomnukuu Mwenyekiti wa CCM. jamani mwenyekiti huyu wa leo ni yuleyule wa huko nyuma aliekiri kukufuru?
   
 9. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #9
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ngekewa, wakati mwingine unapochangia wala hauhitaji kuuchota MKEKA MZIMA MZIMA kama alivyoitandika mtoa mada wa awali. Au sio bro?? Kumbuka kuna wale wanaofuatilia mambo ya JF kwa simu za viganjani tu.
   
 10. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,171
  Likes Received: 1,900
  Trophy Points: 280
  Kama una ushahidi kwamba kanisa katoliki limeifanyia kampeni CDM na ni kinyume cha sheria fanya upes4 wende mahakamani ili waadhibiwe kwa kosa hilo Zaidi ya hapo Wewe ni muongo na unacho fanya ni propaganda au chuki binafsi kwa kanisa katoliki kwa sababu na maslahi yaliyo sirini mwako KWA TAARIFA KWAKO UNACHOFANYA UNAPIGA KONZI NCHA YA MKUKI!
   
 11. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #11
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Hakuna wa kuomba msamaha, Huo ni upuuuuuzi
   
 12. comson

  comson JF-Expert Member

  #12
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kwanza sisiem ni wajinga ila sio wote na wale wenye mawazo ya kuwa kanisa lilipigia kampeni CDM...without evidence hauna right ya kuspeak....if u hav strong evidence nenda mahakamani...... Kanisa la roma halina mambo ya kubabaisha bwana.... Ucfananishe katoliki na getruder rwakatale....

  Ushindwe kabisa na ulaaniwe wewe unayekashifu kanisa kwa maslahi ya mafisadi....
   
 13. comson

  comson JF-Expert Member

  #13
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Huyu hilaly na matete wamelaaniwa kabisa hawa kwanza kuona wanachama wa sisiem wanaonewa ni uongo uliokithiri na kuvuka mipaka hawakumbuki biharamulo waliwafanyia nn CDM..... Halafu ukienda kinyume na kanisa utatengwa tu uclete siasa kwenye dini bwana.... Toa hoja strong na acha ushabiki kwa sisiem tucwe kama mafalisayo........
   
 14. Sisimizi

  Sisimizi JF-Expert Member

  #14
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Msimamo wa kanisa katoliki kuhusu kupinga ubadhilifu ndani ya nchi na taifa letu, unaeleweka, na hauna kifisho. Kama itaonekana mtu anahusisha CDM na Katoliki, basi huyo anaipa credit CDM kwa kuwa msimamo wao ni kupinga ufisadi waziwazi jambo ambalo Kanisa Katoliki lilifanya siku nyingi hata kabla ya pilika pilika za uchaguzi mkuu. Nadhani, mwenyekiti w CCM Rukwa alikuwa anatafuta publicity, kwa mgongo wa kanisa. Niwahakikishie waamuni wa Katoliki ambao wanafikiri masuala ya kiroho yanaweza yakasafishwa majukwaani, tena majukwaa ya kisiasa, wanajipotezea muda na kujipalilia laana bure.

  Wasipotii amri ya kanisa kwa unyenyekevu wajue rohoni wamepoteza.
   
 15. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #15
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  imekula kwao go church go church go!!!!

  hilo ndio kanisa RC!!! hakuna kuchakachua!!! kama wanaweza wakae huko huko wanakotaka..au watafute dini yao nyengine!

  keep it on RC kiboko cha mafisadi!
   
 16. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #16
  Dec 30, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  CCM wao ndiyo watubu kwa kutuibia kura waTZ.
   
Loading...