CCM Pambalama!

Hoja nimeipenda, nitairudia kuchangia lakini naomba kwanza nianze na huu wimbo. Mbona mmebadilisha maneno yake? Kwa kumbukumbu yangu huu wimbo ni wa kichaga, niliwasikia sana wakiuimba enzi tuko Moshi (wakati huo CCM ilikuwa na miaka miwili tu!). Enzi hizo watumishi wa serikali walikuwa wanalazimika kujiunga na mgambo ili wapate cheo kwenye CCM, tulikuwa tunawasikia wakiimba huu wimbo pale uwanja wa shule ya Msingi Muungano ambayo ilikuwa nyuma ya ofisi za RDD wa Moshi:

CCM kyaambalama kocheenyi,
CCM kyaambalama kocheenyi,
CCM kyaambalama kocheenyi CCM eeeh,
Kocheenyi CCM kyaambalama kocheenyi!

Sikuwahi kusumbuka kutaka kujua maana yake wakati huo, lakini kwa kuwa mmenikumbusha naomba wachaga walioko kwenye forum hii wanipe tafsiri yake.

Kithuku,

Miye nilisikia kwenye Mbiu za Mikoa, Asilia Salamu na vipindi vingine vilivyopiga muziki wa kilugha (kikabila). Sijui asili yake ni kabila gani wala maana yake. Nilivyouimba hapa ni jinsi nilivyojitahidi kukumbuka.

Lakini nia kubwa haikuwa kuimba wimbo, bali ni kuijadili CCM ambayo ilisifika enzi zileeee...na sasa unanuka uvundo na uozo!
 
Fukuto la fukuta, moshi wafoka, mapovu yanamwagika, CCM imefika njia panda! Ama isuke au inyoe!

Hili vurugu la Richmond, likizingirwa na BOT EPA, BOT CIS, BOT Minara, Rada, Kiwira, Buzwagi na moto kutoka Upinzani, unafanya mambo kadhaa tujiandee kutokea.
  1. Wabunge ambao si mtandao, wenye uchungu wa kweli wa CCM, kuendelea kusulubisha viongozi wao na Serikali yao iwe wazi. Hawa wabunge, mwokozi wao na nguzo yao ni Wastaafu Malecela, Kawawa, Mwinyi, Salim na Msuya. Huku wako hawa walioshupalia RDC;-Mwakyembe, Kilango-Malecela, Seleli, Kimaro, n.k.
  2. Team Mkapa; huku ni wale wajanja wa Che-Nkapa ambao bado wanatibu majeruhi ya mchakato wa kugombea Urais 2005 na kunyang'anywa tonge la Hatamu za Chama. Hapa kuna Mang'ula, Ngwilizi, Kigoda, Kinana, Warioba na Ruhinda. Katika kundi hili, pia wapo wale waliotajirika na mradi wa Ujasirimali Ikulu; Yona, Mramba, Mgonja, Mkono n.k.
  3. Mtandao; Kundi hili lina majeruhi wengi kutokana na kuvunjwa kwa baraza la mwazirina mwegemeo wa kashfa za ufisadi kuwa kwenye shingo zao. Kundi hili, limegawanyika katika sura mbili;
    1. Team Kikwete ambayo wamebakia Makamba, Chiligati, Membe, Migiro, Karume
    2. Team Rostwassa(Rostam/Lowassa); Karamagi, Msabaha, Nchimbi, Apson, Meghji, Kamala, Diallo, Chenge,
  4. Wasiofungamana lakini wana nguvu na ni tishio; Pinda, Mwandosya, Sumaye, Balali, Salmin, Magufuli, Msekwa na Sitta.
Kutokana na kuwepo makundi haya makubwa na utata unaotambaa angani hasa baada ya Lowassa kuangushwa na minong'ono kuwa naye Lowassa ana ushahidi wa kujikosha, linalobakia kwetu watazamaji ni kupima upepo na kuomba dua wapigane na wagawanyike ili tujue nani ni kwa manufaa ya Taifa na nani ni mnyonyaji.

Nanukuu baadhi ya mambo ambayo yanaashiria kuwa huko CCM si salama, na hata kama wakitoka nje ya ukumbi wakiwa wamekumbatiana, tusiwaamini.

Rev kishoka...lazima uanzishe thread kila ukisoma gazeti linakuvutia? si lazima kila mtu aanzishe thread...hata hujui ipi muhim...take time kusoma walichoweka wenzako, then weka mchango na sources zako.

Pia Muhimu kuweka the whole story? au http link inatosha..mnajaza space bila mpango ktk JF.

Hivi ndivyo ilivyo JF , mbona munatutisha sisi Junior member , kwa nini mtu asitoe mawazo yake - la muhimu ni kuchangia hoja na sio kukandia thread za mwenzako.
 
Team Kikwete ambayo wamebakia Makamba, Chiligati, Membe, Migiro, Karume
Team Rostwassa(Rostam/Lowassa); Karamagi, Msabaha, Nchimbi, Apson, Meghji, Kamala, Diallo, Chenge,
Wasiofungamana lakini wana nguvu na ni tishio; Pinda, Mwandosya, Sumaye, Balali, Salmin, Magufuli, Msekwa na Sitta.

Mkuu wangu Rev,

Maneno mazito hayo, Sitta ni mtandao haswa, ila tamaa za urais ndio zinamponza, ccm is ok maana sasa the brass ndio wenye power wakiitumia idara, muungwana ndiye aliyeko matatani maana akifanya mchezo the brass wanaweza kumuweka mkuchika 2010, otherwise, ya kwako ni great analysis!
 
Kama Marmo atajaribu kudhibiti Hoja basi itakuwa anaimaliza CCM.Maana kila Mbunge sasa anasema kila kitu mezani na hivyo itakuwa rahisi kuchambuliwa .Wakishimdwa Upinzani utaleta hoja na wakiona iko moto watairudia lakini wananchi si wajinga .Labda wafanye kwa kuzima TV na Radio lakini sasa Wapinzani watakuja kwenye Public domain kama walivyo fanya na hapo again CCM will be on defensive .
 
Mwalimu Nyerere alisema, upinzani makini utatokea CCM, je utabiri wa mambo ya nyakati unatimia?

Ikiwa wanatoana macho wenyewe huku Bungeni, je Upinzani uko wapi kujitwalia jimbo la Kiteto?

Tusipoangalia, Upinzani utakufa kifo cha "Mende" kwa CCM mpya kuzaliwa ambayo ni ya Wazawa.

Jiandaeni CCM Wazawa dhidi ya CCM Mafisadi, pia jiandaeni kusikia Ukolimbalization kwa baadhi ya majina makubwa katika hizi kashfa ili kukinusuru chama!
 
Mkuu wangu Rev,

Maneno mazito hayo, Sitta ni mtandao haswa, ila tamaa za urais ndio zinamponza, ccm is ok maana sasa the brass ndio wenye power wakiitumia idara, muungwana ndiye aliyeko matatani maana akifanya mchezo the brass wanaweza kumuweka mkuchika 2010, otherwise, ya kwako ni great analysis!

Sitta ni flip flopper call him mtandao maslahi huyu jamaa ni smart lawyer kila wakati anapima upepo unapovuma halafu ndio anafanya maamuzi, si umeona kwenye tume ya Mwakyembe alikuwa anapiga huku na huku. Lowasa amesema wazi Sitta alimnong'oneza kama ana "ushahidi" wowote wakati tume ya Mwakyembe inaendelea na kazi.

Hii yote ni ktk kuhakikisha kuwa usije ukaniona m-baya mbele ya safari incase plot ya kumng'oa EL inge fail...

Same applies wakati wa kesi ya Mengi V Malima alipoona kibao kinam-badilikia haraka aka aply "busara zangu"

Watu kama Sitta ni hatari sana wanauma na kupulizia...
 
Yanayotokea sasa hivi ni ushahidi tosha kuwa CCM kunaungua, lakini tunaoumia ni sisi!
 
Back
Top Bottom