CCM out

Kwa kuwa Lowassa bado ni CCM sisi wapumbavu,malofa na mbumbumbu kura zetu tunampa LOWASSA halafu tutazilinda tuona kama CCM watakwenda kuzichukua katika sanduku la kura.

Walipobugi UKAWA ni pale walipoleta udhaifu na kumkaribisha Lowasa awe mgombea wao, nyie hamjui kuwa mtoto wa nyoka ni nyoka tu?

Shauri yenu, Lowasa CCM damu yule.

Mnachezewa michezo midogo na wala hamgutuki.

Je Mheshimiwa Lowasa angepata tiketi ya kuwa mgombea wa CCM unafikiri angekuja upinzani?

Kwanini UKAWA wasile matunda yao wenyewe kwa wenyewe na kumsimamisha mtu ambae walietoka nae mbali, ina maana upinzani hawajiamini?

Wenzenu watu Wazima walikaa chini wakasuka mipango na mbinu zao, na kweli zinafanya kazi
 

Inaonyesha jinsi ambavyo ndani ya mfumo wa utawala hakuna uhuru wa kutoa mawazo, kwa kuwa watu huishi kwa hofu. Na EL alichagua kuishi kwa 'hekima ya mtu mzima', lakini ndani ya moyo wake alikuwa hamaanishi hicho ulichoonyesha. EL wa kweli ni huyu wa sasa. Anao uhuru kamili wa kuongea kwa utashi wake mkamilifu. Hiyo ni hulka ya biadamu wote. Na hapo alikuwa akitafuta kick ya chama chake kimpe ridhaa ya kupeperusha bendera ya Urais.

Na kama sio busara, nini kingempata angesema kama asemavyo siku hizi, kama sio kuteremshwa jukwaani na kuondolewa kwenye kinyang'anyiro?
 


aisee naona mnatumia kila mbinu ku-justify unafiki na usaliti uliotokea! kwa mfano angechaguliwa kugombea urais kwa tiketi ya ccm angesema haya anayosema?? na mbowe angesema haya anaosema??!!!
 


Unafanya mchezo na pesa??!! Mtu kanunua chama kizima wafanyabiashara za night club wanaweza kukataa pesa?!!
 

aisee naona mnatumia kila mbinu ku-justify unafiki na usaliti uliotokea! kwa mfano angechaguliwa kugombea urais kwa tiketi ya ccm angesema haya anayosema?? na mbowe angesema haya anaosema??!!!

Unafanya mchezo na pesa??!! Mtu kanunua chama kizima wafanyabiashara za night club wanaweza kukataa pesa?!!
Ubarikiwe sana.

Kwa kumalizia na kwa kufunga mjadala nawaacha na swali.

Kila siku wanalalamika kuwa CCM ndio iliosababisha Raia tuwe masikini na blah blah nyingi tu, mara miaka 52 ya Uhuru CCM haijafanya mabadiliko yoyote na wala haijaleta maendeleo yoyote. Na shutuma nyingine nyingi sana ambazo hazina kabisa misingi.

Mtu akifumaniwa na mkewe inalaumiwa CCM, mtu akinyimwa unyumba na mkewe inalaumiwa CCM, mtu akikosa choo(hapati haja) inalaumiwa CCM, na mengine mengi tu.

Na wakumbuke Mheshimiwa Lowasa alikuwa huko huko CCM ambako wanashutumiwa wametusababishia Raia tuwe na maisha mabovu, duni n.k

Swali:-

Ikiwa Mheshimiwa Lowasa hakuweza kufanya mabadiliko yoyote alipokuwa na ndugu zake CCM je atawezaje kufanya hayo mabadiliko mnayoyataka, mnayoyadai akiwa UKAWA?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…