Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Kuanzia vijana,washabiki na wengineo wa CCM,katika kujenga hoja ni wepesi sana. Inapotokea kuna mjadala wa ana kwa ana unaowajumuisha CCM na wapinzani,utajionea mwenyewe wepesi wa CCM. Mwana-CCM huishia kujitapa kuwa wanapendwa na kukubalika na wataendelea kuongoza. Alijisemea Mch. Msigwa Bungeni 'so what?'.
Ukiona kiongozi wa CCM au mwanachama anaongea 'points' ujue yuko kwenye mimbari ya mkutano wa hadhara iliyozungukwa na polisi na wanafunzi. Points zenyewe zitakuwa kusifu vyombo vya dola,kukejeli wapinzani na kutamba wanapendwa.
Kwenye midahalo au majadiliano yenye mchanganyiko wa wahusika,utauona wazi wepesi wa CCM. Hawachelewi kudai wahuni wamekodiwa kuwazomea. Hivi ukiongea vitu visivyo na tija kwa taifa ndiyo usizomewe.
Katibu Mkuu wa zamani wa CCM Yusuph Makamba alikuwa wa kwanza kuuona wepesi wa CCM. Aliwakataza viongozi kuhudhuria midahalo. Wa pili kuona wepesi ni Mwenyekiti wao wa sasa Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Rais Kikwete aliwaasa wana-CCM kutotegemea vyombo vya dola. Alijua wazi,bila vyombo vya dola,CCM ni wepesi kama unyoya.
Kimsingi,hata mwaka huu mtaji wa CCM utakuwa ujinga,umaskini na maradhi waliyonayo watanzania na si hoja zao. Ngumu kwao kujenga hoja.