CCM ni waongo

Ole

JF-Expert Member
Dec 16, 2006
2,157
971
Chama Cha Mapinduzi kwa mara nyingine kinawahadaa walipa kodi kwa kusema kwamba viongozi Mafisadi waliojikita ndani ya chama hicho na kukifadhili wataachia ngazi walizonazo na kukiacha chama hicho kuwa safi. Je, huu ndio utawala wa sheria ambao chama hiki kinahubiri?

Ikumbukwe kwamba kashfa ambazo RA, Chenge pamoja na EL zinawakabili ni kubwa sana za kuhujumu uchumi wa nchi. Sheria za kuwaadhibu zipo, Je ni kwa nini hazichukuliwi ili tufahamu zipi ni mbivu? Je, JK anaogopa kwamba na yeye ataingia kwenye huo mtego? Inawezekana vipi watu wakwapue pesa za walipa kodi na wasiwe na adhabu yoyote? Je tumefika mahali ambapo sheria za nchi zinatembezwa mfukoni kama pesa? Inawezekana vipi JK akatembea kifua mbele wakati anashindwa kulinda katiba ambayo aliapa kwamba atailinda?

RA, EL, Chenge na wafuasi wao lazima wachukuliwe hatua zinazostahili bila kuwaonea aibu kwa sababu tukiwaonea aibu hawa itabidi tuwaonee aibu wanaoiba kuku pamoja na heleni.
 
Ole umesema ukweli..
ile dhambi iliyo kuu ndiyo wameifumbia macho huku wakidanganya kwa msemo wao wa kujivua gamba.
 
huyo jk ameacha taifa hili linaangamia, mpaka hapa tulipo.
Je hakujua maovu hayo yaliyokuwa yanafanywa na wanachama wa chama chake na chizi makamba.
Je ataweza kufidia hasara ambazo taifa limepata kwa ufisadi wa chama chake.
Jk ni mnafiki mkubwa tena hatari kuwa naye kama rais rahisi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom