CCM ni sikio la kufa - Halisikii dawa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM ni sikio la kufa - Halisikii dawa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chigwiyemisi, Apr 4, 2012.

 1. Chigwiyemisi

  Chigwiyemisi JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 531
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwa jinsi mambo yanavyoendelea ndani na nje ya CCM naamini kwa dhati kabisa kwamba chama hiki sasa kinajinoa kuwa chama cha upinzani na kuwaachia CDM hatamu zote. Nasema CCM ni sawa na sikio la kufa ambalo kamwe halisikii dawa kwa sababu chama hiki kina bahati ya kupata mawazo, ushauri, maoni na mbinu mbali mbali za kukinusuru lakini labda kwa kutoelewa au kwa makusudi kabisa kimekataa kubadilika na kubaki na mambo yake ya mwaka 47 katika dunia ya leo. Kimeshindwa kutumia fursa zote za kubadilika na sasa nadhani safari yake imefikia ukingoni! Naamini pia inawezekana laana kubwa inawakabili na Mungu ameamua kutunusuru waja wake na chama hiki dharimu.... Hebu fikiria kama sio laana;

  1. Inawezekana vipi wakakaa, wakajadiliana na kutafakari kwa kina wakaona kuwa Wasira, Lusinde (matusi) na Mwigulu wanaweza kuwa wapiga kampeni wa kukipatia ushindi! kama sio laana ni nini?
  2. Inawezekana vipi kumrudisha Mkapa kufunga kampeni baada ya kufanya madudu namna ile kwenye ufunguzi! Busara na maono yao yako wapi? Sikio la kufa .........
  3. Inawezekana vipi Lusinde akaongea Masaburi day 1, day 2, day 3 na kuendelea bila kumkanya wala kumtimua? Hawakuona? Je ni laana au sikio la kufa?
  4. Inawezekanaje Wasira (mausingizi) akadanganya kuwa Nasari hana baraka za wazazi wake, wazazi wakakanusha kisha akadanganya kwamba Dr. Slaa alikula fedha za kanisa, kanisa likakanusha lakini wao wakaendelea kumuamini hadi mwisho bila kumtimua wala kumkanya! Ni hujuma, laana au ndo sikio la kufa?
  5. Wakati yote hayo hapo juu yanafanyika hawakuwa wanakaa na kutathmini hatima ya chama chao? Mwenyekiti wao alikuwa anajulishwa mwenendo wa kampeni?

  R.I.P CCM
   
Loading...