Ccm ni sawa na mti uliooza kiini -- mzee butiku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm ni sawa na mti uliooza kiini -- mzee butiku

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FUSO, Oct 20, 2011.

 1. F

  FUSO JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,867
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  Wakuu,

  Wote tunamjua Mzee Butiku, yaani kila nikifikiria hii statement yake aliyotoa wakati wa majumuisho ya kumuenzi baba wa taifa kweli mimi nabaki hoi bin taabani.

  Kweli mambo yamefikia pabaya namna hii ndani ya chama hiki kikongwe?, CCM wanalazimika kuzifanyika kazi kauli kama hizi, vinginevyo ndugu zangu maji ndiyo yamezidi unga. Wote mnajua kwamba bila kiini (moyo) hata kama ni mtu lazima ukate roho sasa Mzee Butiku kaona mbali kwamba CCM inaelekea KUZIMU muda si mrefu.

  Angesema haya mtu mwingine ambaye si MZITO, wana CCM wangekejeli na kusema akapimwe akili huyo, lakini mpaka sasa bado hatujasikia upande mwengine ukifafanua kauli hii. Binafsi nampongeza Mzee wetu, kweli sisi wananchi hasa Vijana tumeipokea kauli hii kwa matumaini mapya ya mustakabali wa taifa letu.

  Hongera Mzee kuweka mambo Hadharani na Mungu akujaze na akupe maisha marefu. Ukweli unauma lakini ni muda sasa wa sisi watanzania kuungana pamoja kukaa chini, kuweka uzalendo mbele na kuangalia mustakabali wa taifa letu hasa tunapoelekea kusherekea miaka 50 ya uhuru wa nchi yetu ya Tanganyika.
   
Loading...