CCM ni ma-genius wa Siasa!

Hiki Chama kitaendelea kutawala Tanzania kwa miaka mingi sana ijayo na sababu ni kwamba CCM inaelewa Siasa za Dunia kuliko siajabu Chama chochote kile barani Afrika kama siyo sehemu kubwa ya Dunia!

Kwa mfano CCM imekuwa madarakani kwa miaka mingi sana ukilinganisha na Vyama vingine, lkn tofauti na vyama vya nchi nyingine kama vile ZANU-PF, KANU au sijui MPLA -Angola &Co. ambapo kwenye hizo Nchi unaweza kuita Viongozi wao Madikteta na hoja yako kuuzika kwa maana wanaongozwa na Kiongozi mmoja miaka yote, lkn hapa Tanzania kwetu huwezi kuita Udikteta kwa maana ndani ya CCM ni demokrasia pure, kwamba Uongozi una ukomo hivyo basi kila baada ya miaka 10 huja Kiongozi mpya, na hii ndo Janja kubwa ya CCM, hapa ndipo genius ya CCM ilipo!

Hivyo basi tofauti na Syria, Libya au sijui Kongo ambapo ilikuwa rahisi kujenga hoja ya Udikteta na kupata sapoti ktk nje hapa kwetu huwezi kupata sapoti kwa maana kila kitu kiko wazi na watu wa nje hawawezi kuikubali hoja ya Udikteta Tanzania kwa maana hakuna Kiongozi Dikteta kwa maana halisi ya neno na ndo maana ni ngumu sana Upinzani kuishinda CCM ndani na nje ya Nchi!

Na sasa kama hiyo haitoshi CCM inabadilika kuendana na muda sasa kuna damu mpya watu kama H.Pole pole ambao wana mawazo mapya jinsi ya kuijenga na kuiboresha CCM, the old guard imeeenda, fikiria tu mtu kama Nape Nnauye nani alijua kama baada ya miaka 5 angemaliza muda wake na kupisha wengine? Nipe mfano wa Chama kinachofanya hivyo hapa TZ au hata nje ya mipaka yetu, ndo maana hata watu kama akina Kingunge walifikiri wako juu ya Chama kwa kutishia kujitoa, wamejitoa lkn hakuna hata kilichobadilika ni kama hata hawajafanya kitu, na hii imewezekana tu kwa sababu ya mfumo mzuri wa CCM waliojiwekea ambao ndio unaowafanya waendeelee kuwepo, hivyo basi ni ngumu sana kwa Upinzani kuweza kuishinda CCM si kwa kura au hata kwa hila tu labda kujaribu kupata sapoti nje ya nchi kwa maana CCM iko vizuri na ina demokrasia kubwa!
Nina fikiri haujui kwanini ccm inatawala kwa miaka mingi.Hivyo inaoneka jinsi ulivyo na uwezo mdogo wa siasa za hapa Tanzania.Elewa hivyi kuanzia leo.Ni rahisi sana kuwatawala watu wengi wasio na elimu.Elimu ndio msingi wakujitambua,hivyo basi wananzania waliowengi hawana elimu. Hawajitambui wanadanganyika kirahisi.Miaka 55 sasa tangu tupate uhuru bado vyuo vikuu havifiki hata kumi !!!!!!!.halafu unajidanganya kwamba ccm ina magenius wa siasa!!!! Wewe ni mmoja wao wasiojitambua au upo ccm kwa maslahi yako binafsi .Maranyingi huwa nafikiria serikali inafanya makusudi kutowekeza katika elimu ,hasa elimu ya juu ili iweze kututawala kwa miaka mingi. Serikali inatakiwa ijenge vyuo vikuu vingi kama inataka tanzania iendelee. Nina pendekeza kila bajeti ya mwaka kuwe na mioango ya kujenga chuo kikuu mkoa na mkoa. Serikali inatakiwa nguvu zake nyingi ielekeze katika elimu. Elimu ndio msingi wa kila kitu.
 
Back
Top Bottom