GuDume
JF-Expert Member
- Jan 18, 2015
- 6,651
- 14,318
Nikikaa nawaza sana. Nikitizama tulipotoka mpaka hapa tulipo naona hakuna uwiano. CCM ikiwa Tanu ilitusaidia kupata Uhuru chini ya Nyerere.ilifanya kazi yake miaka hiyo ikakamilika. Ilitubeba kama punda abebavyo mizigo. Miaka zaidi ya 50 sasa CCM imechoka sana. Imechoka kuliko. Kama Punda mzee. Miguu yote imekufa huyu punda anaishi tu kwa kudra za sijui nani. Ila hana faida tena kijamii,kiuchumi na kisiasa.
umewah mwona kuku aliyekatwa kichwa halafu akaachiwa aruke? huruka akijigonga huko na huko pasipo uelekeo mpaka roho yake itakapomtoka. huwa haoni anapoelekea hukimbia au kuruka uelekeo wowote asijue pa kwenda.
Ilianza safari yake miaka mingi kwa sera na kauli mbiu mbalimbali ambazo mpaka leo hakuna ambacho kimeonekana kikiwa na uhai katika vyote. imekuwa ikienda kwa kupapasa. ikienda pasipo kuwa na uelekeo N ahapa Marehem Horace Kolimba ndipo aliposema CCM imepoteza uelekeo. Imekuwa kama Tanga lisilo na nahodha baharini. laenda kilikokotwa na Upepo huko na huko kulingana na Upepo unakoelekea. Halina mwongozaji. na ndo maana tunaona chama hiki kinaongozwa kuendana na Utashi wa Rais aliyeko madarakani.
akija rais akasema sasa kila mtu achume ajilie vyake watu watachuma na rais huyo watakavyo na mwishowe atamaliza muda wake wakiwa yeye na washirika wake wameibia wananchi hawa maskini kwa kiwango kikubwa sana. atapumzika kwa amani kabisa nchi hapa na kokote atakapo.
akija mwingine ambaye yeye kichwa chake anakijua mwenyewe naye ataendesha nchi kwa imani yake yeye na mtizamo wake yeye mwenyewe. naye ataongoza kwa miaka yake 10 kama jeshi la mtu mmoja au kikundi flan cha makomandoo. akimaliza ataondoka na kupumzika kwa amani kabisa. CCM imapoteza muelekeo.
Wapinzani. hawa wamekuwa kama mbwa koko... mbwa huyu anabwekea hata kivuli... mbwa huyu anabwekea hata ndege wanaoruka angani. mbwa koko huyu anabweka usingizini. lakini si mkali ni koko anabweka huku mkia akiwa ameuweka katikat ya miguu yake. huamini? leama yupo ndani mpaka leo kwa inachosemwa amri ya mkuu ingawa aliyethibitisha hilo mpaka sasa kuwa ni amri ya nani. ben saanane hafahamiki yupo wapi mpaka leo hii. lakini hamna anayezungumza watu wamepigwa ganzi. kuna miili ilionekana imeharibika huko mto ruvu ikasemwa ni miili ya wakimbizi. tukajiuliza utaratibu wa ku mutilate wakimbizi umeanza lini? hatukupewa jibu na ben saanane hafaahimiki yu wapi.aliowatumikia nao wamepigwa ganzi.
suala la lugumi suluhisho lake lilikuwa tu ni kwa kitwanga kujiuzuru na kuishia hapo? je hakukuwa na jambo lingine kubwa zaidi la kuwawajibisha wahusika?baada ya kitwanga kufukuzwa kazi likawa limeisha. wapinzani walikuwa wanabwekea kivuli.
madawa ya kulevya. tunadhana hapa hili liwe vita dhidi ya makonda...wapinzani wanabwekea kivuli. hili wapinzani walipaswa waliteke walifanye ni ajenda yao kwa namna yao ya kisomi na kufuata taratibu. na si kuhamishia vita kwa makonda ambaye ilishaonekana alishindwa kabla ya kuanza. badala yake wapinzani na wabunge kwa ujumla wakaanza kucheza ngoma yenye midundo ile ile ya makonda kwa maneno tofauti tu.ikawa ni vita dhidi ya makonda. utajiri wake, mahusiano yake, vyeti vyake n.k. hapa wapinzani walitoka kwenye reli. na kwa sasa hilo jambo limeisha isha. alitakwa amepatikana na igizo litaendelea wiki ijayo.
wananchi wa kawaida tusio na vyama ndio tunaopata shida. wenye vyama akili zao hazifanyi kazi kabisa. wanapofikiri wanafikiri kichama, wanapoongea wanaongea kichama, wanapotembea wanatembea kichama, wanapokula wanakula kichama, wanapowaza wanawaza kichama, wanapoandika wanaandika kichama.
waliobali na pure mind ni wachache, wengi wameshakuwa corrupt. ukimkosoa mtu watasema ni kwa kuwa ni chama x na wao wanapomkosoa mtu ni kwa vile ni chama y . nchi inaangamia.inakosa watu wenye free mind. si wanasiasa si wasomi. wote wanawaza kwa mtizamo kengeufu.
nimenena yangu ni zamu yako nawe kusema au kunibwatukia.