Niliwahi kuandika thrd hii siku za nyuma nikiamini kabisa kwamba ndani ya CCM hakuna anayeweza kusema itabadirika. Hali tuliyo nayo inazidi kudhihirisha maandishi yangu maana kwa vitendo tunavyoviona vikifanyika ndani ya chama au na vigogo wa chama sina sababu ya kusema CCM ni chama cha siasa. Chama tawala kinacholinda na kusimamia malipo ya DOWANS, 'adui' wa nchi, aliyeshitaki alipwe.
Sasa tena tunaona eti UVCCM wakijifanya wako upande mwingine wa chama. Hizi ni mbwembwe ili kuonyesha kwamba hayo ya DOWANS hayawahusu CCM. Mwenyekiti wao, Kikwete, yuko wapi???
Naomba niirejee meseji yangu kwa wakati huu.
Kwa wale munaofahamu jinsi Cali cartel walivyokuwa wakifanya kazi halamu ya cocaine nchini Colombia ni rahisi kulinganisha mambo yanayofanywa na CCM na kikundi kama hicho. Cocaine iliwahusisha hata wanasiasa, akiwemo Rais Ernesto Samper.
Binafsi siioni tofauti kati ya Cali Cartel na CCM. Ni chama kinachoishi kwa kutumia mbinu chafu. Sasa wanauza ardhi, wanavuna madini, wanabeba pesa za serikali kifisadi, nk. Kwa ujumla sioni tena biashara halali inayofanywa na CCM kuingiza kipato cha kuwawezesha kulipa mishahara ya wenyeviti na makatibu kila Wilaya na bado wakapata pesa za chaguzi ndogo na kununua magari na sasa waingie uchaguzi mkuu.
Taasisi zote za serikali hupata pesa pungufu ya zile zilizopangwa na Bunge kila mwaka lakini hakuna anayeuliza sehemu isiyokuja huenda wapi. Inasikika ni kwenye chama. Yaonekana Bajeti yetu inahudumia serikali mbili, Serikali halisi na hii ya CCM.
CCM ni Cartel wa hatari sana!
Cali cartel iliangushwa kwa msaada wa America. CCM iko Jeshini, iko polisi, iko mahakamani, na kwa ujumla kila katibu Mkuu wa Wizara lazima awe na kadi ya chama ndo maana wengine walianza kutangaza niya ya kugombea wakiwa bado ni makatibu wakuu. Nani ataiangusha? Nchi gani ya nje itakayoweza kutusaidia kuiondoa wakati tunasifiwa tumetulia na tuna amani?