MchunguZI
JF-Expert Member
- Jun 14, 2008
- 4,009
- 2,171
Narejea maneno haya kwa hali mpya ya sasa. Kwa hali ilivyo sasa kundi la Cartel limekuwa kubwa. Mahakama hazitendi haki, zinashirikiana na waharifu. Polisi hawatendi haki, vituo vimekuwa ni sehemu ya kuokota maiti. Mawaziri ni wezi wanashirikiana na watendaji na wanalindwa hadi Ikulu.
Tunaelekea hali ya Kolombia ambapo Waharifu walikuwa wanafadhili hadi mtu kuwa rais, IGP, CDF na wataalamu wote muhimu ktk nchi.
Je Tanzania tutaendelea kama nchi?
Kwa wale munaofahamu jinsi Cali cartel walivyokuwa wakifanya kazi halamu ya cocaine nchini Colombia ni rahisi kulinganisha mambo yanayofanywa na CCM na kikundi kama hicho. Cocaine iliwahusisha hata wanasiasa, akiwemo Rais Ernesto Samper.
Binafsi siioni tofauti kati ya Cali Cartel na CCM. Ni chama kinachoishi kwa kutumia mbinu chafu. Sasa wanauza ardhi, wanavuna madini, wanabeba pesa za serikali kifisadi, nk. Kwa ujumla sioni tena biashara halali inayofanywa na CCM kuingiza kipato cha kuwawezesha kulipa mishahara ya wenyeviti na makatibu kila Wilaya na bado wakapata pesa za chaguzi ndogo na kununua magari na sasa waingie uchaguzi mkuu.
Taasisi zote za serikali hupata pesa pungufu ya zile zilizopangwa na Bunge kila mwaka lakini hakuna anayeuliza sehemu isiyokuja huenda wapi. Inasikika ni kwenye chama. Yaonekana Bajeti yetu inahudumia serikali mbili, Serikali halisi na hii ya CCM. CCM ni Cartel wa hatari sana! Cali cartel iliangushwa kwa msaada wa America. CCM iko Jeshini, iko polisi, iko mahakamani, na kwa ujumla kila katibu Mkuu wa Wizara lazima awe na kadi ya chama ndo maana wengine walianza kutangaza niya ya kugombea wakiwa bado ni makatibu wakuu. Nani ataiangusha? Nchi gani ya nje itakayoweza kutusaidia kuiondoa wakati tunasifiwa tumetulia na tuna amani?