CCM ni ile ile, hakuna kimpya

CCM ni ile ile, hakuna kimpya

Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2020
Posts
5,595
Reaction score
14,054
CCM imekuwa madarakani kwa takribani miaka 50 shida ambazo watanzania wanazo ni zilezile chini ya utawala wa CCM.

Imefika wakati viongozi ambao ndio dira ya taifa kutoa majina ya ajabu kwa wananchi wake kuona kwamba ndo sifa kuu ya wao kupata ushawishi wa kisiasa nacha ajabu ni kuwa wananchi wenyewe wamekubali kuitwa majina hayo hayo uku wakijihisi ni ufahari kuitwa hivyo "Wanyonge" Na wanyonge hawa ndo wamekuwa wakitapeliwa pesa zao na utawala wa CCM mfano ni wakulima wa korosho.

Na sifa za hawa wanyonge ambao ni mazao ya utawala wa CCM ndo umefanya wawepo wamekuwa na mawazo ya kimaskini ya kutaka kuona kila aliye nacho apoteze ili awe kama wao ila sio wao kufanya juhudi kupata ili wawe kama kundi la walio nacho.

Ndio maana kuna kiongozi alikuwa anawaambia wananchi wake kuwa nchi yao ni tajiri hivyo watembee kifua mbele na wakati huo huo anajiita Rais wa Wanyonge na mpaka anapoteza maisha kawaacha wanyonge bado wakiwa katika hali ile ile uku wakilia badala ya kutumia akili zao kutoka kwenye unyonge.

Unyonge ni ishara ya kujidharau, ujinga, kuwaza kimasikini, uvivu, majungu, fitina, uoga nk na hawa wanyonge ndo mtaji wa CCM kubaki kuendelea kutawala maana ni "wapupaze na uwatawale"

CCM imekuwa ikitembea na matumaini hewa kwa watanzania ndio maana maadui watatu ambao Baba wa taifa aliwataja wako pale pale miaka kenda rudi ni wimbo ule ule Umaskini,ujinga na Maradhi.

CCM ni chama chenye mfumo wa kulindana ndio maana wezi wakubwa wa mali za umma wako bado mitaani wakila kuku kwa mrija kabisa bila wasiwasi na bado pesa za Watanzania wavuja jasho zikiendelea kuwatunza kama viongozi wastaafu.

Watanzania sasa wameonekana kuwa na matumaini makubwa baada ya kuingia kwa awamu ya 6, uku wakisahau kuwa Chama ni kile kile mifumo ni ile ile hakuna kipya ni suala la muda tu.

CCM ni sawa na ukoo wa Panya.
 
Nyereere alifanikiwa sana 100% kuishikanisha Dola na CCM

Yaani CCM ndio Polis, Majesh, Usalama n.k

Kuiondoa CCM madarakan nisawa umeondoa Dola n.k. Kazi ambayo ni Ngumu mnooooo mnooooooo.
 
Maendeleo ya kweli na ya dhati yatapatikana Tanzania siku CCM ikiondoka madarakani.
 
CCM Hawafai ni Ile ile MIJAMBAZI. Watu ni wale wale. Tabia ni zile zile ..Mijizi ile ile so Daaah!...CCM mbona Unatutesa.....Mungu bado Haujatusaidia na Hawajakuelewa ebu...Tusaidie...Watesi bado wale....Washauri wa Korona bado ni credible wanaendelea kushine..Maana wap juu tena Juu...Ohooo Sir God Mbona hawajajua wewe ni Mungu.
 
Swali linabaki ni nani atakayeiondoa sasa?
 
Naona mmeanza rasmi kumpiga Mama vita sasa.
 
Wengi hawalifahamu hilo
Nyereere alifanikiwa sana 100% kuishikanisha Dola na CCM

Yaan CCM ndio Polis, Majesh, Usalama n.k .

Kuiondoa CCM madarakan nisawa umeondoa Dola n.k.. Kazi ambayo ni Ngumu mnooooo mnooooooo.
 
Maendeleo ya kweli na ya dhati yatapatikana Tanzania siku CCM ikiondoka madarakani.
Hahah! Mkuu hapo ndy umepotea kbs, kwa mfano ni chama gani cha upinzani kinachoweza kuongoza dolla. Binafsi kuna cha upinzani nilianza kukiamini lakini kitendo cha kumchukua mtu alikatwa chama tawala na kumtambulisha kuwa ndy mgombea wao kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 ilinifanya nikose imani kabisa na hivi vyama vya upinzani.

Kwa ufupi sio kwenye chama tawala pamoja na kwenye vyama vya upinzani, bado tuna Changamoto kubwa ya uzalendo kwenye maslai ya Taifa letu.
 
CCM imekuwa madarakani kwa takribani miaka 50 shida ambazo watanzania wanazo ni zilezile chini ya utawala wa CCM.

Imefika wakati viongozi ambao ndio dira ya taifa kutoa majina ya ajabu kwa wananchi wake kuona kwamba ndo sifa kuu ya wao kupata ushawishi wa kisiasa nacha ajabu ni kuwa wananchi wenyewe wamekubali kuitwa majina hayo hayo uku wakijihisi ni ufahari kuitwa hivyo "Wanyonge" Na wanyonge hawa ndo wamekuwa wakitapeliwa pesa zao na utawala wa CCM mfano ni wakulima wa korosho.

Na sifa za hawa wanyonge ambao ni mazao ya utawala wa CCM ndo umefanya wawepo wamekuwa na mawazo ya kimaskini ya kutaka kuona kila aliye nacho apoteze ili awe kama wao ila sio wao kufanya juhudi kupata ili wawe kama kundi la walio nacho.

Ndio maana kuna kiongozi alikuwa anawaambia wananchi wake kuwa nchi yao ni tajiri hivyo watembee kifua mbele na wakati huo huo anajiita Rais wa Wanyonge na mpaka anapoteza maisha kawaacha wanyonge bado wakiwa katika hali ile ile uku wakilia badala ya kutumia akili zao kutoka kwenye unyonge.

Unyonge ni ishara ya kujidharau,ujinga,kuwaza kimasikini,uvivu,majungu,fitina,uoga nk na hawa wanyonge ndo mtaji wa CCM kubaki kuendelea kutawala maana ni "wapupaze na uwatawale"

CCM imekuwa ikitembea na matumaini hewa kwa watanzania ndio maana maadui watatu ambao Baba wa taifa aliwataja wako pale pale miaka kenda rudi ni wimbo ule ule Umaskini,ujinga na Maradhi.

CCM ni chama chenye mfumo wa kulindana ndio maana wezi wakubwa wa mali za umma wako bado mitaani wakila kuku kwa mrija kabisa bila wasiwasi na bado pesa za watanzania wavuja jasho zikiendelea kuwatunza kama viongozi wastaafu.

Watanzania sasa wameonekana kuwa na matumaini makubwa baada ya kuingia kwa awamu ya 6,uku wakisahau kuwa Chama ni kile kile mifumo ni ile ile hakuna kipya ni suala la muda tu.

CCM ni sawa na ukoo wa Panya.
Changamoto si chama tawala wala vyama vya upinzani, Changamoto kubwa ni wazalendo wa kweli wenye kupigania maslai ya Taifa. Karibu vyama vyote hapa nchini vina hiyo changamoto, hata kwenye hivyo vyama vya upinzani bado ni walewale hakuna kipya..
 
Nyereere alifanikiwa sana 100% kuishikanisha Dola na CCM

Yaan CCM ndio Polis, Majesh, Usalama n.k .

Kuiondoa CCM madarakan nisawa umeondoa Dola n.k.. Kazi ambayo ni Ngumu mnooooo mnooooooo.
Mkuu "hakuna marefu yasiyokuwa na ncha"
 
Hahah! Mkuu hapo ndy umepotea kbs, kwa mfano ni chama gani cha upinzani kinachoweza kuongoza dolla. Binafsi kuna cha upinzani nilianza kukiamini lakini kitendo cha kumchukua mtu alikatwa chama tawala na kumtambulisha kuwa ndy mgombea wao kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 ilinifanya nikose imani kabisa na hivi vyama vya upinzani.

Kwa ufupi sio kwenye chama tawala pamoja na kwenye vyama vya upinzani, bado tuna Changamoto kubwa ya uzalendo kwenye maslai ya Taifa letu.
Toka mfumo wa vyama vingi umeanza kungekuwa na uwanja sawa wa kufanya siasa kwa vya vyote hali ingekuwaje, kwenye siasa sawa hata ccm ingeweza leo kuwa chama cha upinzani. Hata wenyewe CCM wakipasuana na kushindwa kulindana chama kikavunjika itakuwa poa sana. Leo taifa inatimiza miaka zaidi ya 50 huduma za CT scan na MRI ni Dar na Mwanza tu, Moshi na Mbeya sina uhakika.
 
Uko sahihi, binafsi naangalia hii Changamoto ya utawala hasa kwenye hizi nchi zetu ya kiafrika kama janga la kitaifa. Yaani kwamba si vyama tawala wala vya upinzani bado uzalendo imekua ni changamoto kubwa.

Kikubwa ni kila mtu atangulize maslai ya Taifa kwa nafasi aliyokua nayo. Kwa hii nchi yetu bado naona wapinzani wanasafari ndefu kuchukua dolla na hii ni kutokana na wap wenyewe kukosa uzalendo wa kweli.

NB: Mimi si shabiki wa chama chochote ni mpenda maendeleo.
 
CCM imekuwa madarakani kwa takribani miaka 50 shida ambazo watanzania wanazo ni zilezile chini ya utawala wa CCM.

Imefika wakati viongozi ambao ndio dira ya taifa kutoa majina ya ajabu kwa wananchi wake kuona kwamba ndo sifa kuu ya wao kupata ushawishi wa kisiasa nacha ajabu ni kuwa wananchi wenyewe wamekubali kuitwa majina hayo hayo uku wakijihisi ni ufahari kuitwa hivyo "Wanyonge" Na wanyonge hawa ndo wamekuwa wakitapeliwa pesa zao na utawala wa CCM mfano ni wakulima wa korosho.

Na sifa za hawa wanyonge ambao ni mazao ya utawala wa CCM ndo umefanya wawepo wamekuwa na mawazo ya kimaskini ya kutaka kuona kila aliye nacho apoteze ili awe kama wao ila sio wao kufanya juhudi kupata ili wawe kama kundi la walio nacho.

Ndio maana kuna kiongozi alikuwa anawaambia wananchi wake kuwa nchi yao ni tajiri hivyo watembee kifua mbele na wakati huo huo anajiita Rais wa Wanyonge na mpaka anapoteza maisha kawaacha wanyonge bado wakiwa katika hali ile ile uku wakilia badala ya kutumia akili zao kutoka kwenye unyonge.

Unyonge ni ishara ya kujidharau,ujinga,kuwaza kimasikini,uvivu,majungu,fitina,uoga nk na hawa wanyonge ndo mtaji wa CCM kubaki kuendelea kutawala maana ni "wapupaze na uwatawale"

CCM imekuwa ikitembea na matumaini hewa kwa watanzania ndio maana maadui watatu ambao Baba wa taifa aliwataja wako pale pale miaka kenda rudi ni wimbo ule ule Umaskini,ujinga na Maradhi.

CCM ni chama chenye mfumo wa kulindana ndio maana wezi wakubwa wa mali za umma wako bado mitaani wakila kuku kwa mrija kabisa bila wasiwasi na bado pesa za watanzania wavuja jasho zikiendelea kuwatunza kama viongozi wastaafu.

Watanzania sasa wameonekana kuwa na matumaini makubwa baada ya kuingia kwa awamu ya 6,uku wakisahau kuwa Chama ni kile kile mifumo ni ile ile hakuna kipya ni suala la muda tu.

CCM ni sawa na ukoo wa Panya.
Na ndo imekufanya uwe na elimu ya kuja kuiponda usisahau hilo
 
Kikubwa ni kila mtu atangulize maslai ya Taifa kwa nafasi aliyokua nayo. Kwa hii nchi yetu bado naona wapinzani wanasafari ndefu kuchukua dolla na hii ni kutokana na wap wenyewe kukosa uzalendo wa kweli.
Naamini watanzania wote ni wazalendo, ila uzalendo wao unategemea anaewaongoza. Rais akiwa mzalendo kwa vitendo, hakuna kubagua, kulindana, anaweka maslahi ya Taifa mbele chama nyuma, unaheshimu katiba. Ndani ya miaka 10 tunaingia Nchi za Dunia ya 2 bila kuambiwa na wazungu, maana popote utakapokuwa mabadiliko ya kimaendeleo na kiuchumi yatakugusa moja kwa moja. Hakuna nchi rahisi kuongoza kama Tanzania, anagalia jinsi JPM alivyotuburuza hakuna aliyekuwa anakohoa.
 
Sasa huo uzalendo wa kweli kwa upande wa upinzani bado nina mashaka nao. Kwangu mimi naona bado wana deni la kwa namna gani wafanye ili niridhike kua sasa wanaweza kuongoza nchi na kunisahaulishe yale waliyoyafanya mwaka 2015 kwenye uteuzi wa mgombea wao wa nafasi ya urais.

Binafsi nina imani nao tu kwenye nafasi za ubunge na nyingine za chini. Lakini kwenye kuongoza nchi bado hua nahisi wanaweza kurudisha nyuma hata haya maendeleo tuliyonayo.

NB: Kuongoza nchi kama Tanzania sio kitu rahisi, kumbuka hata Mh.Magu alipigwa sana mawe wakati wa uongozi wake na hii ilitokana na mapenzi pamoja n.a. uzalendo aliokua nao kwenye nchi yake..
 
Nani aliweza kumpinga JPM na akabaki salama? Kina nani hao waliokuwa wanapinga uongozi wake na kwanini?
 
Nyereere alifanikiwa sana 100% kuishikanisha Dola na CCM

Yaani CCM ndio Polis, Majesh, Usalama n.k

Kuiondoa CCM madarakan nisawa umeondoa Dola n.k. Kazi ambayo ni Ngumu mnooooo mnooooooo.
Ipo siku itang'oka tu. Hata kwa mtutu wa bunduki itang'oka tu. Hakuna lenye mwanzo, likakisa kuwa na mwisho.
 
Back
Top Bottom