Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,410
- 38,702
Sisemi watu wote CCM ni waoga bali wengi wao tena wako wengi hasa ni watu waoga!! Tangu Enzi chama hicho kinaundwa, uundwaji wake ulifanyika kwa maamuzi ya watu wachache (Aboud Jumbe na Nyerere) wanachama wa TANU na ASP walihusishwa baadaye na hasa baada ya makubaliano ya kuhakikisha kwamba neno "Mapinduzi" litakuwemo kwenye jina la chama kipya CCM. Waliokuwepo walikuwa waoga hawakuhoji na wakapandikiza roho ya hofu kwenye chama chao ambayo ipo mpaka leo.
Kwenye CCM viongozi wana "akili nyingi" sana na hawatakiwi kuhojiwa na wanaojaribu kuhoji ni lazima washikishwe adabu. Utaona mtu yule yule ambaye alikuwa anakosolewa kabla ya kuwa na cheo, akipata madaraka inakuwa ni mwiko kukosolewa. Kwenye CCM mambo yanayotokea kwenye vyama vya upinzani hayawezi kutokea ndani ya chama hicho kwa kuwa kimejaa watu waoga!!
Kinachotokea CUF kwa Katibu Mkuu na Mwanachama wao aliyefukuzwa Ibrahimu Lipumba kulumbana hadharani hakiwezi kuvumiliwa ndani ya CCM na mara zote anayeadhibiwa ni yule mwenye cheo kidogo kuliko mwenzake! Tatizo siyo adhabu bali mara zote adhabu zenyewe huwa za kiuonezi na hakuna anayethubu kusema kwama ni uonevu.
Yale ya Jakaya Kikwete kuja na Majina ya wateule wake kwenye kikao cha uteuzi wa Mgombea urais kupitia chama hicho, isingewezekana kwenye vyama vya upinzani, lazima angepingwa kwenye kikao na nje ya kikao na wanachama wenzake. Woga wa wananchama wa CCM umesababisha ionekane kwamba viongozi wa CCM wana akili kuliko wanachama wake wa kawaida.
Wakati Humphrey Polepole akitangaza kwamba Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa "kauli moja" imeunga mkono mapendekezo yote ya Kamati Kuu ya chama hicho, nikajiuliza hicho kikao cha Halmashauri Kuu hakikuwa na wajumbe wenye mawazo tofauti na yale ya Kamati Kuu? Lakini kumbe waliokuwa na mawazo tofauti tayari walikuwa wameshashughulikiwa!!
Hiki chama kilichojaa watu waoga kwa bahati mbaya ndicho kinachoongoza serikali ya nchi yetu, bila shaka na chenyewe kitataka kujenga hofu kwa watanzania wote na wao wakiogope. Hofu ina tabia ya kuambukiza na wanaotaka watu wawe na hofu hulazimisha hofu kutamalaki pale sauti za kuwapinga zinapoongezeka!!