CCM ng'ang'anieni madaraka kama KANU muue chama

Feb 18, 2019
50
532
CCM mna option 1 ya kuhakikisha chama hakifi. Kubalini kushindwa ili mkajipange upya na kwa uhakika haitawachukua muda mrefu mtarudi kwenye hatamu za nchi hii. Asiyekubali kushindwa si mshindani na kushindwa si kufeli.

Ama laa, ng'ang'anieni madaraka muue chama kama KANU ya Kenya. Ukweli mchungu ambao hamna budi kukubaliana nao ni kwamba hamtatawala milele, hata mfanye mazuri yapi hamuwezi. Hii ni kutokana na human nature ya kuwa na chachu ya kubadili ladha, yani ni kitu ambacho kipo ndani ya damu ya wanadamu.

Ukiachana na makandokando yenu ya uongozi wa nchi hii ni ukweli kwamba automatic watu wanahitaji kuona mabadiliko kwenye uongozi wa nchi hii hata kama mngekuwa mmefanya mazuri yapi, its human desire. Na hii desire ipo kwenye peak kwa sasa hivyo hamuwezi kuizuia.

Ukweli ni kwamba kwa mizizi mliyonayo hamna haja ya kuwa na wasiwasi ya kesho yenu katika uongozi wa nchi hii. Kubalini kuachia madaraka kwa amani ili msiichafue nchi kwani hamtachukua muda mrefu kurudi madarakani.

Siasa ni sayansi inayohitaji mahesabu ya mbali. Kwa hali ya sasa mkijaribu kulazimisha mtakuwa mnajichimbia kaburi wenyewe. Pigeni mahesabu vizuri ya kesho yenu itakuwaje kabla hamjaamua kulazimisha nyie tuu ndio muongoze hii nchi kwa miaka nenda rudi wakati umefika muda wa kustep pembeni ili mkajipange upya.

Wakati ni ukuta, huwezi kuuvunja kwa kutumia ngumi.

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom