CCM ndio kila kitu, wengine ni watapia mlo tu, ndio ukweli

CCM ndio kila kitu, wengine ni watapia mlo tu, ndio ukweli

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
2,175
Reaction score
4,180
Chama cha Watanzania ni CCM, tulieni, Watanzania walio wengi ,na hawa wachache ni wa vyama vingine ambavyo zaid vipo kikanda au kiukoo mfano, wapemba wachaga na kadhalika.

Ifahamike inaposemwa kiukoo au kiukabila usiangalie viongozi zaidi angalia wafuasi na viongozi wao, wengi wanakuwa kutoka pembe moja ya nchi hizi.

CCM itaiongoza Tanzania kwa miaka mingi sana inayokuja pengine nyote au sote itakuwa tumeshaiwacha dunia ,hivyo tuendelee kuchapa kazi na kuachana na tamaa na maneno ya uchochezi na kuleta mifarakano, vyama vilivyopo kama nilivyosema kwanza havina wafuasi wa kweli,wananchi wa Tanzania sio watu wa fujo fujo ni mihemkoa ya kuchangamsha tu likipita limepita.

Ona kule, wafuasi wa Bob wayne, Raila unaweza kusema kule kuna wananchi wenye tabia za uthubutu na sio kwa Tanzania, WaTanzania ni wapenda amani sana sana kuliko maelezo, hivi vyama vichache ,eti sera za ubwabwa, pana siasa hapo ?

Vyama havidai tume ya uchaguzi mpaka uchaguzi kesho, mna wazimu ? Si mnalidanganya kundi lenu na wafuasi wenu tu, ili miradi yenu ifanikiwe.

Tunaona CCM tunavyoimarisha umoja baina ya wananchi, sasa waTanzania walio wengi wameanza kuona mwangaza wa Uongozi waliokuwa na tunu nao kwa miaka mingi na vyama vile vimebaki na wenyeviti na meza tu huku uraiani wanazidi kukimbiwa na kuhofiwa kama virusi vya corona..
 
Nje ya mamlaka ya dola CCM nayo ni hopeless tu tena zaidi ya hao wengine. CCM ni portion ya jamii ileile inayotoa wenye itikadi nyengine za kisiasa, kwahiyo utofauti wao ni mdogo sana kama watawekwa kwenye nazingira sawia ya kufanyia siasa zao.
 
vyama vya ukanda na ukabila ,wasahau kushika dola kwenye hili taifa. chadema ni kimoja wapo,ukabila na ukanda umewajaa.hiki ni chama!!au kampuni ya ukoo!!!
 
Sio Mitano tena ni milele kabisa tafadhali.

Uchumi wa kati.

Nchi hii ni tajiri sana.

Au nasema uongo ndugu zangu.

Unaijua vieite wewe?

Viongozi wote wa CCM tunatembelea mavieitee.
IMG_20210112_150518.jpg
IMG_20210101_160453.jpg
 
Wapinzani wamefika hapa walipofika leo baada ya kuokota wavuta bangi, wanywa gongo, wapiga ndole, mateja nk kuwa wafuasi wao. Ndio maana kila unapofanyika uchaguzi wanaangukia pua, maana hao sio wapigaji kura
 
We fikiria kama Mwamakula alikuwa ndio mshauri wa yule mbelgiji,!

Hakuna kama ccm, hawa wengine ni wapiga debe tu
 
Bado nafikiria ni nani aliyeipigia kura CCM maana wengi hawaitaki ata tuanze kufuatilia comments za CCM ni chache sana
Hata Lisu alipokuwa anaona coments za kwa kigogo, akija hapa jf kina mmawia wanahanikiza kwa comnts zao basi akajiona tayari rais.
 
We fikiria kama Mwamakula alikuwa ndio mshauri wa yule mbelgiji,!

Hakuna kama ccm, hawa wengine ni wapiga debe tu
kama hao wengine sio tishio, ni kwann mkatumia nguvu kuubwa uchaguzi mkuu hadi kulazimika kuubaka ili mshinde?!

kwakuwa mungu wa chato kafanya makubwa si hata kampeni asingefanya apate kura zote kwakuwa wadanganyika walimuelewa sana?!.
 
Mmebaki wenyewe uwanjani lakini bado hamjiamini, mnawawaza wapinzani wa nini tena? Tunahitaji maendeleo ambayo mlituambia kuwa wapinzani ndio walikuwa wanayachelewesha
 
CCM hawahawa wanaosema kuwa kukataa social distancing ni suala sahihi litakalotupeleka sehemu sahihi?
0210210165643.jpg
 
Onako Kajinga aka


CCM iwe kila kitu itumie mbinu za kishenzi namna hii??

Wasomi wote ndan ya CCM wamekua maboyaaa sababu ya Tumbo

Nikionaga mtu anaishabikia CCM hata kama kasoma, najua kabisa hili kichwan hamna kitu,

Lina elimu ya kusoma kwa kukesha na kuloweka miguu na kubebwa, lkn uhalisia unabaki palepale kua Bongo lake lina uozo.
 
Ukweli mchungu ,na ndio sioni ajabu wengine wanaanza kutoa maneno ya ufezuli, huwezi kudai tume huru uchaguzi kesho,ni kuwadanganya watu ionekane ukishindwa kura zimeibwa,walewale waliokamata masanduku ya kura walewale wameingia bungeni,Alima Ndee uyu alikuwa kinara wa kukamata walizoziita kura za bandia au sijui za wizi leo yuko wapi,sasa akikurupuka huko aliko na kusema zile drama zote zilitayarishwa na chama mtasemaje ? bado bado sana wajamaa,kuongoza nchi sio lelemama na mipango na njama za kutunga kutafuta huruma kwa mabeberu,inatakiwa mjitoe na zaidi mkubalike huku mitaani jambo ambalo hamjalifikia,zaidi mnakuwa na kuonekana kumejaa kutokana na wafuata burudani.

Mmeona uchaguzi huu tuliowapiga na chini juzi,mikutano ya CCM haikutumia nguvu nyingi kutoa hotuba majukwaani zaidi walitoa burudani kwa wananchi wa Tanzania .

Naamini mtaelewa tu CCM tutaiongoza nchi hii kwa karne zingine zinazokuja,hivi vyama ni kama makundi ya nzige yanakuja na kupita.
 
kama hao wengine sio tishio, ni kwann mkatumia nguvu kuubwa uchaguzi mkuu hadi kulazimika kuubaka ili mshinde?!

kwakuwa mungu wa chato kafanya makubwa si hata kampeni asingefanya apate kura zote kwakuwa wadanganyika walimuelewa sana?!.
Nani kaiba? Una ushahidi wa kuibiwa? Uliibiwa kura ngapi?
 
Wapinzani wamefika hapa walipofika leo baada ya kuokota wavuta bangi, wanywa gongo, wapiga ndole, mateja nk kuwa wafuasi wao. Ndio maana kila unapofanyika uchaguzi wanaangukia pua, maana hao sio wapigaji kura
Therefore Watanzania>6million waliompigia kura Mh.Lissu ni wanywa gongo na bangi¿ Hivyo vitu haramu vinafanyika serikali ikiwa likizoni?Uzembe wa Sirro,Muroto,Mambokale au???
 
Back
Top Bottom