CCM ndio iliyoleta umaskini Tanzania

CCM ndio iliyoleta umaskini Tanzania

ntemintale

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2016
Posts
956
Reaction score
1,878
Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndicho chama kongwe barani Afrika kilichosababisha umaskini kwa wananchi wengi nchini Tanzania. Sababu ni hizi:-

1. Elimu/maarifa/stadi duni kwa wananchi. Hivyo kuwafanya washindwe kuyamudu maisha na mazingira yao.

2. Huduma duni za afya, nguvu kazi inapotea kwa vifo.

3. Ukosefu wa maji safi na salama, kunazorotesha afya za wananchi na kusababisha magonjwa mbalimbali, kwani 70% ya mwili wa binadamu ni maji.

4. Ukosefu wa vyanzo bora vya umeme (mgao). Hivyo kushusha jitihada za wananchi kuzalisha mali.

5. Miundo mbinu duni ya barabara kwa wananchi wengi ambao 80% wanaishi vijijini. Usafirishaji wa bidhaa, mazao na watu umezoroteshwa.

6. Kilimo duni cha jembe la mkono, kunakopelekea uhaba wa chakula na kushuka kwa kilimo biashara.

7. Ukosefu wa demokrasia ya kweli, yenye kuruhusu uhuru wa mawazo na habari, ambavyo ni njia muafaka ya kukuza ubunifu na kupashana habari. Uchakachuaji wa chaguzi mbali mbali na kupelekea kupata viongozi wabovu (dhaifu na madikteta)

8. Rushwa, Ufisadi na kujichotea pesa kienyeji bila idhini ya bunge, kisha kuzipeleka kusikostahili, kama kujenga international airport kijijini, ili hali kuna uhaba wa madawa hospitali.

CCM Mungu anawaona.
 
Huko nyuma tulifundishwa kuwa " ili tuendelee tunahitaji mambo manne, watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora" toka wakati huo mpaka sasa hatujaendelea. Tumekwamishwa wapi? Watujibu
 
Huko nyuma tulifundishwa kuwa " ili tuendelee tunahitaji mambo manne, watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora" toka wakati huo mpaka sasa hatujaendelea. Tumekwamishwa wapi? Watujibu
Tena watufafanulie haswaaa
 
Huko nyuma tulifundishwa kuwa " ili tuendelee tunahitaji mambo manne, watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora" toka wakati huo mpaka sasa hatujaendelea. Tumekwamishwa wapi? Watujibu
Sema wewe hujaendelea na Jiulize binafsi kwa nini hujaendelea?
 
Sema wewe hujaendelea na Jiulize binafsi kwa nini hujaendelea?
Tuendelee kama nchi. Labda hukusomea Tanzania ama huenda wewe ni mnyarwanda. Vinginevyo watanzania wote wanalijua somo hilo lilihusu maendeleo ya taifa na si maendeleo ya mtu mmoja mmoja.
 
Yeye sio mbinafsi Wa kujiangalia yeye
Na wakati tunafundishwa mbinu hizo za maendeleo taifa lilituonya kuachana na ubinafsi, ndiyo maana kulianzishwa na vijiji vya ujamaa, maduka ya ushirika nk. Kila mtanzania alijua hivyo. Ukiona mtu analazimisha ubinafsi kwenye jambo hilo ni mgeni Tanzania. Huenda ni wale waliokimbia vita kwenye nchi zao na kujipatia urai Tanzania bila kujua vipaumbele vya Taifa
 
Na ukienda huko vijijini ndio utasema watanzani kweli wanataabika na ccm yao

Swissme
 
Back
Top Bottom