GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,100
Moja ya dhana katika ulimwengu wa Vihatarishi wanasema" It is easy to manage Risk than Crisis, Management of crisis ni gharama kubwa sana, kwa lugha ya isiyo rasmi wanasema si rahisi kulizuia janga kwani Janga tayari limetokea lakini ni rahisi kutatua au kuzuia vitu ambavyo vinaweza pelekea kwenye janga
Wananchi wengi wa Tanzania tayari ni Janga au crisis wanalala na kuamka wanafikiri umaskini wao au utajiri wa wengine umesababishwa na ccm Kama chama hilo sio kweli kabisa, Wananchi wenyewe wamejisababishia umaskini wa fikra tangu uhuru
Watanzania wengi Baada ya uhuru walijenga fikra Sasa mkoloni alitutumikisha sana ni muda wa kupumzika, na kweli walipumzika wakisubiri serikali mpya ilete maendeleo kwenye familia zao, Nani asiyejua jinsi Nyerere Rais alipopita maeneo ya Njombe na Ruvuma akitishia watu lazima walime sana mahindi baada ya kugundua wanabweteka tu ,kuna kipindi watu walifanaya kazi za shamba kuogopa ma DC na wakuu wa mikoa ,Je hili ni kosa la ccm ?
Nani asiyejua hulka ya watanzania kuchangia ngoma na harusi badala ya kushikamana kuchangia baadhi ya watoto wapate elimu ,Ni jambo la kawaida kusikia sherehe imegharimu milioni 20 Huku Bi harusi na Bwana harusi wanatoka koo zenye umaskini uliotopea na koo yenye watoto wengi wasiosoma, Hili ni kosa la ccm ?
Leo hii miaka mingi imepita tangu uhuru, kimezaliwa kizazi kipya kabisa cha 1990's ambacho Ndio kimemaliza shule na vyuo kwenye ulimwengu wa technology, kizazi hiki kimesoma kwenye ulimwengu wa You tube, Facebook na WhatsApp, Nani asiyejua jinsi hawa vijana wanatumia kuanika maungo yao na kujadili mambo ya betting tu, Je umaskini wa hawa watoto na watoto wao baadae ni kosa la ccm ?
Miaka hii ya kuanzia 2005 to 2010.enzi za Kikwete nani asiyejua mzunguko wa pesa ulivyokuwa mkubwa na watu wengi waliamua kuacha kazi na kufanya biashara wakiamini kazi ni utumwa ,Wakati wazungu mtu hufanaya kazi zaidi ya tano au kumi bila kudharau kazi mojawapo, Fikra kuwa kazi moja ni zuri kuliko nyingine imewafanya vijana kutokuwa na msimamo na msingi imara leo anafunga hiki kesho anaanza kile, Nani asiyejua vijana hufuata upepo wakisikia matikiti yamezaa sana mwaka huu basi wote mwakani watalima matikiti na kuacha kazi moja, Hili kosa la kufuata upepo ni kosa la ccm ?
Kuendekeza siasa za majitaka na uchama ,kujadili Viongozi masaa 24 siku saba kwa week badala ya kufanya kazi Ndio agenda ya kuelekea 2020.Nani asiyejua wanaojadiliwa wana miradi na maendeleo ya kutupwa, Makosa kama haya yaliletwa na ccm ?
Wananchi lazima watambue maendeleo yao yanaletwa na wao wenyewe kwa kubadili fikra zao binafsi, Hata siku moja ccm haikuwahi msababishia mtu umaskini tangu kuanzishwa kwake
Sisi wananchi ndio tumeisababishia ccm umaskini Jaribu kuangalia wanaojiuzulu ubunge ili ccm iingie gharama, Jaribu kuangalia sauti za Komu na kubenea wakipanga uhuni ili serikali na chama viingie gharama
Tutatoa povu lakini maisha yako yapo mikononi mwako mwenyewe binafsi, Chama kipo pale Kama holistic structure tu
Maswali ya kujiuliza :
Je, Taratibu na kanuni tulizonazo Kuna siku zitabadilika au ni wananchi wenyewe wabadili fikra zao ili wakifanye chama kilete maendeleo, na sio kukisubiri kiwaletee maendeleo
Ni nani anayeeneza sera na Itikadi kwa miaka hii karibuni, Je si ni vijana wenzenu mliowaunga mkono leo mnawaona mwiba na wasaliti, Hata siku moja maendeleo hayaletwi na chama bali watu hufanya chama kilete maendeleo
Hitimisho :
Kusubiri chama kilete maendeleo hakuna tofauti na kumchukua mbuzi beberu kumuweka angalie UEFA champions league ataona mnampotezea muda wa kula nyasi