chitambikwa
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,941
- 903
Zitto alipoenda Kigoma kuzindua Leka dutikite alijaza uwanja mara mbili ya hapo na idadi ya watu waliokaa nje ilikuwa ni mara mbili ya waliopata nafasi ya kuingia ndani, ikumbukwe wote unaowaona hapo sio kwamba wamefuata sherehe hizo kuna walienda kmwona Diamond wakidhani ataimba Leka dutikite na zaidi na zaidi unaambiwa mshiko na mabasi vimetembea balaaaa.
Zitto kaandika ktk twitter kuwa wakati anakwenda Kasulu amekutana na mabasi yamejaza magamba yanakwenda Kigoma, sasa hayo ni sehem tu, je, mangapi ambayo yamesafirishwa?
sherehe za miaka 36 ya CCM zafana sana mjini Kigoma leo
Ndugu yangu Do not read too much katika hadhara hiyo kubwa!! Hakuna kitu kinachoweza kupendwa au kuchukiwa na watu wote; kwa wakati wote! na wala hadhara hiyo haiwakilishi asilimia 100 ya wakazi wa Kigoma; la hasha!!!
CCM ina die hards wake; wazee na walalahoi waliokata tamaa; na Vyama mbadala (Sio Upinzani!) vina watu wake hasa kizazi kipya na wasomi.
Sasa basi ukizingatia kwamba life is so boring in Kigoma; hiyo shughuli ilikuwa ni outing of the decade, Kigoma hakuna mpira wa daraja la kwanza, bendi kubwa kubwa haziendi Kigoma mpaka Zitto ahamasishe matamasha! watu wa Kigoma hawajamuona Raisi wao tangu 2010 wakati wa uchaguzi wa kampeni na isitoshe matarajio ya umma kwa JK kumwaga ahadi zisizotekelezeka lukuki ni baadhi ya mambo yanayoweza kuwafanya wanakigoma kufurika uwanja wa tanganyika pasipo manufaa ya kisiasa kwa CCM.
Mkuu hiyo ni hela imetumika kujaza watu hapo kuna Rafiki yangu wa Karibu mhasibu wa ccm amendokezea hii kitu imekula zaidi ya milioni 500
Safi sana!! Jamaa wanalia,, wako tayari kuita nyekundu wakati wanaona kabisa ni kijani. Jamaa wanakimbia kivuli chao! Wao wakijaza mikutano hawakawii kuleta picha hapa,, leo CCM wamejaza Kigoma nongwa! hawa watu hawa! ni wa kuogopa kama ukoma
Kwani ile treni iliyobeba Magamba mengine toka Dar mmeshaisahau! Kama yaliweza kubeba watu kwa treni toka Dar, je kwa mikoa na wilaya za jirani si yatakuwa yamebeba mpaka Mbwa!
nashangaa unashindwa kufikiria kuwa watu wale walijaa kwa sababu ya Diamond, na sio CCM, tulishawahi kufanya sherehe ya siku ya UKIMWI Duniani Kigoma na tulitangaza Comedy watakuwepo, uwanja ulifurika mno mpaka watu wakazuiliwa getini, ina maana walijaa kwa sababu ya mgeni rasmi?
Ndugu yangu Do not read too much katika hadhara hiyo kubwa!! Hakuna kitu kinachoweza kupendwa au kuchukiwa na watu wote; kwa wakati wote! na wala hadhara hiyo haiwakilishi asilimia 100 ya wakazi wa Kigoma; la hasha!!!
CCM ina die hards wake; wazee na walalahoi waliokata tamaa; na Vyama mbadala (Sio Upinzani!) vina watu wake hasa kizazi kipya na wasomi.
Sasa basi ukizingatia kwamba life is so boring in Kigoma; hiyo shughuli ilikuwa ni outing of the decade, Kigoma hakuna mpira wa daraja la kwanza, bendi kubwa kubwa haziendi Kigoma mpaka Zitto ahamasishe matamasha! watu wa Kigoma hawajamuona Raisi wao tangu 2010 wakati wa uchaguzi wa kampeni na isitoshe matarajio ya umma kwa JK kumwaga ahadi zisizotekelezeka lukuki ni baadhi ya mambo yanayoweza kuwafanya wanakigoma kufurika uwanja wa tanganyika pasipo manufaa ya kisiasa kwa CCM.
Kwa Watanzania wengi, picha ni ujumbe kisiasa, na ujumbe chanya au hasi una shadadiwa na UMATI wa watu shiriki katika mikutano ya kisiasa. Hii ya CCM sijui katika fikra hizo inatoa ujumbe gani, hasa ikizingatiwa hiyo ni "ngome" ya vyama vingine vya kisiasa huku kikiwa 'kimelemewa' na zigo la kiuongozi na kiutawala nchini.
Sina budi kukubaliana na wale wanaopatwa na sindiko la moyo pale matokeo ya chaguzi yanapokuwa vinginevyo kwa kutumia dhana ya UMATI katika siasa za Tanzania.
Kama MAGAMBA walialika Mpaka ngoma kutoka Burundi na huyo Diamond ulitegemea watu wasije kuburudika?? Hawakuja kushabikia CCM ila kuburudika na kuwashangaaa Mafisadi
Kwa Watanzania wengi, picha ni ujumbe kisiasa, na ujumbe chanya au hasi una shadadiwa na UMATI wa watu shiriki katika mikutano ya kisiasa. Hii ya CCM sijui katika fikra hizo inatoa ujumbe gani, hasa ikizingatiwa hiyo ni "ngome" ya vyama vingine vya kisiasa huku kikiwa 'kimelemewa' na zigo la kiuongozi na kiutawala nchini.
Sina budi kukubaliana na wale wanaopatwa na sindiko la moyo pale matokeo ya chaguzi yanapokuwa vinginevyo kwa kutumia dhana ya UMATI katika siasa za Tanzania.
huo umati walikuja kwa ridhaa yao au waliweshwa?