CCM na siri za miswada ya dharula

CCM na siri za miswada ya dharula

Wabogojo

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
354
Reaction score
87
Habari Wana JF!

Katika hali isiyo ya kawaida Spika wa Bunge leo tena ameahirisha kikao cha Bunge kwa mara nyingine baada ya kufanya hivyo jana. Sababu ya kufanya hivyo ni baada ya Wapiganaji na wawakilishi wa wananchi mle Bungeni kuomba Miongozo na Spika kutupilia mbali maombi ya miongozo ya Upinzani na hivyo kuanzisha sintofahamu kwa kuanza kupiga kelele na huku bila hata AIBU, Mh Simbachawene aliendelea tu kusoma mswaada huo as if yale makelele alikuwa hayasikii.

Kinachoonekana hapa ni kwamba kutakuwa na SIRI nzito inayo wasukuma hawa Wabumge wa CCM na serikali yao kutaka kutaka kupitisha huu mswaada kwa maslahi ya watu wachache badala ya wananchi wote. Na kwa kuwa Wabunge wa UKAWA wameonyesha kuugomea huo Mswaada wa maguta na gesi asilia na vema basi watueleze umma ni nini kilichopo nyuma ya pazia na kufanya mswaada huu pamoja na mingine mitatu kuingizwa Bungeni kwa hati za dharula huku kukiwa hakuna ulazima kihivyo.

Ingekuwa vema sana kama hoja ya Mh Mnyika ingekubaliwa kwa kuweka pembeni moswaada yote na badala yake Bunge lijadili kusuasua kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura ikiwa ni pamoja na mapungufu yake kwa kutumia BVR, lakini pia kagusia suala la uwepo wa Tume huru ya Uchaguzi mboma jambo kama hili nyeti na kwa mstakabali kwa Uchaguzi ulio huru na haki hata halitengenewi mswaada na kuingizwa Bungeni kwa hati ya dharula huku ikizingatiwa kuwa wana siku chache sana za kuwepo bungeni na miezi michache sana kukaribia tarehe ya uchaguzi mkuu hapo Octoba 2015.

My Take:

Mosi, tunaomba UKAWA waueleze UMMA ni nini walicho kiona nyuma ya pazia la CCM juu ya miswaada yao hii ns kama kina harufu ya UFISADI basi ni bora tuelezwa tujue kuliko kuaminishwa kwamba Wabumge wa UKAWA ni watu wa fujo na dharau kwa BUNGE letu TUKUFU.

Pili nataka niwaulize Wabunge wa CCM ni kwa nini mara nyingi wanakuwa against na hoja nyingi zenye maslahi kwa wananchi na badala yake wanakuwa watetezi wa Serikali, hivi wanajua gharama yake? OK tutakutana nao baadaye Octoba 2015.
 
Kwa kweli inasikitisha sana. Kuna haraka gani katika Hili!?
 
Umetiririka vyema mkuu wangetuambia wananchi ni nini kipo nyuma ya pazia
 
Ee Mwenyezi Mungu, Mkuu na mwingi wa Rehema uwaongoze wabunge wetu, wakujue wewe na Haki yako ili taifa letu liendeshwe katika misingi ya haki na amani maana akili za baadhi ya wabunge zinaonekana kufikia mwisho haziwazi tena mema juu ya taifa la Tanzania!
 
oil and gas revenue management act 2015 inatakiwa ipitishwe kwa hati ya dharura kama ilivyoingizwa suala la benk kuu na sarafu 1965 katka orodha ya mambo ya muungano. CCM BAADA ya kuona oil and gas vitatolewa katika muungano na Zanzibar itajitegemea katika hilo wameona njia mbadala ni kudhibiti mapato yote yatakayopatikana kupitia BANK OF TANZANIA NA TRA chini ya wizara ya fedha ya Tanganyika .
hilo ni moja u ya utubo wa miswaada hii nyeti kwa TANZANIA.
 
na kwa NINI mambo haya yaletwe wakati akili zishaelekea kwenye uchanguzi tena kwa HATI YA DHARURA KAMA NI JAMBO HALIKUFAHAMIKA VILE .....kuna viashiria vya ufisadi hapa
 
na kwa NINI mambo haya yaletwe wakati akili zishaelekea kwenye uchanguzi tena kwa HATI YA DHARURA KAMA NI JAMBO HALIKUFAHAMIKA VILE .....kuna viashiria vya ufisadi hapa

Wanajua hilo. Muda huu wabunge wengi wana stress na presha za uchaguzi, wengi hawatasoma muswada. Walitarajia wangepitisha kilaini laini, lakini naona mambo yanakuwa magumu.
 
oil and gas revenue management act 2015 inatakiwa ipitishwe kwa hati ya dharura kama ilivyoingizwa suala la benk kuu na sarafu 1965 katka orodha ya mambo ya muungano. CCM BAADA ya kuona oil and gas vitatolewa katika muungano na Zanzibar itajitegemea katika hilo wameona njia mbadala ni kudhibiti mapato yote yatakayopatikana kupitia BANK OF TANZANIA NA TRA chini ya wizara ya fedha ya Tanganyika .
hilo ni moja u ya utubo wa miswaada hii nyeti kwa TANZANIA.

Kwani Bunge lijalo litakuwa siyo la Tanzania? Wasubiri haraka ya nini, waachie bunge lijalo lije lijadili kwa kina muswada huu siyo kukimbizana kama nchi inataka kupinduliwa! Hata Nhhghulunzinza alisubiri hafanyi haraka hivi!
 
Wanajua hilo. Muda huu wabunge wengi wana stress na presha za uchaguzi, wengi hawatasoma muswada. Walitarajia wangepitisha kilaini laini, lakini naona mambo yanakuwa magumu.

Ni kweli Mkuu, hata Spika jana alisema wazi kwamba tatizo la akina Mnyika na UKAWA kwa ujumla ni kuwa hawaja jiandaa.Sasa kama walikuwa hawajajiandaa hali imekuwa hivyo je wangejiandaa si ndiyo ingekuwa kiama kwa CCM? Big up UKAWA, hakikisheni kinaeleweka.
 
Mama ane semamba makinda watakutoa kafara hawa wana ccm,wakati umebaki na siku 5 tu bunge livunjwe,achana na huo mswada mama yangu
 
nimefurahi sana Leo,miCCM ilijua watu watatka ili yenyewe yaendelee,lkn watu wamekomaa.
 
Ni vyema wanainchi tukaanzisha kampeni ya ''twende bungeni'',,,tuwachape tuu,mbona tunadharaulika kwann?,,so sad,tumelogwa na nan?,,
 
oil and gas revenue management act 2015 inatakiwa ipitishwe kwa hati ya dharura kama ilivyoingizwa suala la benk kuu na sarafu 1965 katka orodha ya mambo ya muungano. CCM BAADA ya kuona oil and gas vitatolewa katika muungano na Zanzibar itajitegemea katika hilo wameona njia mbadala ni kudhibiti mapato yote yatakayopatikana kupitia BANK OF TANZANIA NA TRA chini ya wizara ya fedha ya Tanganyika .
hilo ni moja u ya utubo wa miswaada hii nyeti kwa TANZANIA.

Yap ni kweli siri haswa ni kuinyang'anya zanzibar uwezo wake wa kuchimba mafuta ili mafuta yawe ni ya tanganyika,hebu fikiri wamesubiri baraza la wawakilishi livunjwe ndipo wao wamepeleka hati ya dharura kwenye bunge la tanganyika.
 
Hizi ni njama za kuweka mikataba ya mangungo wa msovero kwa kuwa wao wamemaliza muda wao na wameaga.
 
nimefurahi sana Leo,miCCM ilijua watu watatka ili yenyewe yaendelee,lkn watu wamekomaa.

Bila kukomaa mbele ya majambazi huwezi win vita hiyo! Na silaha yoyote lazima uitumie kushinda! Hiyo zomeazomea pamoja na kuwataja majina eti anaahirisha bunge kwa kuwa wameabuse bunge ni bora iwe hivyo tu!
 
Habari Wana JF!

My Take:

Mosi, tunaomba UKAWA waueleze UMMA ni nini walicho kiona nyuma ya pazia la CCM juu ya miswaada yao hii ns kama kina harufu ya UFISADI basi ni bora tuelezwa tujue kuliko kuaminishwa kwamba Wabumge wa UKAWA ni watu wa fujo na dharau kwa BUNGE letu TUKUFU.

Hili ndilo la msingi sana.KUB alifaa aitishe kikao cha dharura cha Baraza la Mawaziri vifuli na siku ya leo baada ya Bunge hili kuvunjika na baada ya yeye kutoka ndani ya Kamati ya Maadili ambayo na amini yumo na mara baaada ya Bazara kivuli kufanya kikao cha dharura walifaa waitishe Kikao cha wa Bunge wa UKAWA na mwisho watoke na Taarifa kwenda kwa Umma kuna nini nyuma ya hizi miswada.

CC Kurugenzi ya Habari Tumaini Makene.
 
Last edited by a moderator:
huo ni mpango endelevu wa kifisadi ndani ya vichwa vya wabunge wa maccm haiwezekani
 
Hawa ndorobo ndiyo wanazidi kujimaliza na kutupatia hoja za kuwashawishi wananchi kwa nini ni hasara kuwa na wabunge wengi wa ccm, wenyewe wanafikri wanawakomoa ukawa kumbe ndiyo wanawapa nondo za kuwachapia, asanteni sana mafisi wa kijani toka lumumba.
 
Back
Top Bottom