CCM na serikali yake wanapaswa kuwaomba radhi watanzania kwa kushiriki kuiba au kusaidia wezi

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,510
2,000
Tangu ile ripoti ya kwanza na hii ya leo, Kamati zote mbili zimewasaidia watanzania kubaini kuwa CCM si ya kuaminika, haifai kuongoza nchi, haina dhamira ya dhati ya kusaidia taifa hili, na viongozi wengi wa CCM ni wapiga dili.

Serikali ya CCM ndiyo iliyoileta kampuni ya Accacia nchini, wakaipa mgodi bila kusajiliwa BRELA, CCM ikatumia idadi kubwa ya wabunge wake bungeni kuruhusu wawekezaji wa madini (including Accacia) kuchukua 96% ya gross income na taifa kuambulia 4% tu.

Mambo haya yaliyoongelewa kwenye kamati leo na ile kamati ya kwanza, yamekua yakiongelewa na vyama vya upinzani kwa miaka mingi lakini CCM na wafuasi wake wakiwabeza wapinzani. Leo Kamati hizi zinaongea lugha ileile iliyoongelewa na upinzani kwa miaka mingi, wafuasi walewale wa CCM waliobeza ndio wako mstari wa mbele kushangilia. Upuuzi wa kiwango cha shahada ya uzamivu.!!

Labda niwaambie tu kuwa chanzo cha yote haya si makinikia, wala si Accacia kutokusajiliwa. Chanzo cha yote haya ni mikataba ya hovyo iliyopitishwa na wabunge wa CCM kwa wingi wao bungeni. Kwa hiyo kama tunataka kusaidia taifa hili dawa si kukenua meno kumsifia Rais, dawa ni kurudisha mikataba yote bungeni, ikafumuliwe na kusukwa upya kwa maslahi ya taifa. Vinginevyo tunapoteza muda kusikiliza vitu visivyotoa promising future.

[HASHTAG]#NiniKifanyike[/HASHTAG]:

1. CCM na serikali yake wanapaswa kuwaomba radhi watanzania kwa kushiriki kuiba au kusaidia wezi wa kimataifa kuiba rasilimali za nchi (madini ni kielelezo tu, lakini CCM wameuza rasilimali nyingi kuliko madini. Sekta ya utalii, uvuvi, gesi huko balaa ni kubwa zaidi).

2. Serikali ya CCM wakubali kubeba lawama zote zinazotokana na hasara hii kubwa kwa taifa.

3. Mikataba yote ya madini na mikataba mingine inayohusu rasilimali za taifa (kama utalii, gesi, vitalu vya uwindaji, Uvuvi, nishati etc) irudishwe bungeni ikafumuliwe na kusukwa upya kwa kulinda maslahi ya taifa.

4. Naibu Waziri wa Madini Dr.Medard Kalemani (ambaye alibakizwa baada ya Waziri Muhongo na Katibu Mkuu kuondolewa) nae aondolewe. Ikumbukwe Kalemani alikua wizara ya nishati na madini tangu mwaka 1999 akishika nafasi mbalimbali wizarani hapo. Amekuwa Afisa Mwandamizi wa Sheria (Seniour Legal Officer), Mkurugenzi wa sheria kwa nyakati tofauti. Maana yake ni kwamba alihusika kwa namna moja au nyingine na mikataba hii mibovu iliyotuingizia hasara kama taifa.

5. Mwaka 2020 CCM waamue wenyewe kuondoka madarakani kwa kutosimamisha mgombea Urais, maana wamepoteza uhalali wa kuendelea kuongoza. Vinginevyo wananchi wawaondoe madarakani kwa nguvu ya kura.!
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
27,593
2,000
Francis, Acacia wana kosa la kutosajiliwa. Waliambiwa kujisajili wakakanusha. Kama walikataa walichukuliwa hatua gani?
 
Apr 15, 2017
39
125
haya yako Tanzania tu ambapo mmoja ya wale walioshiriki kusema ndio na kusema mikataba ni siri anatuambia tena tumeibiwa mno ni mambo ya ajabu sana kwa mambo haya bora umeishi Burundi mambo yakajulikana najiuliza ivi ile gesi mtwara kichapo nilikuwa cha nn kwa wazawa na ile mikataba inayopelekwa bungeni kwa dharura basi bwana tutaona mengi
 
Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,510
2,000
Francis, Acacia wana kosa la kutosajiliwa. Waliambiwa kujisajili wakakanusha. Kama walikataa walichukuliwa hatua gani?
Acacia haina Certificate of Compliance! Na imekuwa ikifanya uchimbaji muda wote? How? Yaani mpaka Tume iundwe ndio hili lijulikane? [HASHTAG]#Ulofa[/HASHTAG]
CCM tuliamua kujisahisha na ndio maana tulisema mabadiliko ya kweli 2015 mchagueni JPM.. JPM for Changes

Ameshachoka mpaka anajuta.
'Kuna muda natamani ningekuwa namaliza muda wangu, hii kazi ni ngumu. huwa namuuliza Mungu, kwanini alinipa mimi' JPM
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
27,593
2,000
Acacia haina Certificate of Compliance! Na imekuwa ikifanya uchimbaji muda wote? How? Yaani mpaka Tume iundwe ndio hili lijulikane? [HASHTAG]#Ulofa[/HASHTAG]

Ameshachoka mpaka anajuta.
'Kuna muda natamani ningekuwa namaliza muda wangu, hii kazi ni ngumu. huwa namuuliza Mungu, kwanini alinipa mimi' JPM
Ok, haya ni mambo ya sheria, sasa nani anazitoa hizo certificate
 
Nyalutubwi

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
573
225
Ndugu yangu unajua dunia nzima na hata nchi ambazo hazina hadhi ya kutushangaa wanajiuliza maswali ya inakuaje nchi yenye raslimali kama Tanzania inatawaliwa na viongozi wanaoweza kutoa maamuzi ya ajabu hivi katiaka kusimamia raslimali zake?.Haiingii akilini eti leo baada ya miaka zaidi ya 18 ndiyo tugundue rasilimali zetu zinaibiwa.Tatizo kama ulivyosema ni sisi wenyewe kutojitambua kama wasimamizi wakuu wa raslimali zaTaifa kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Tuna matatizo ya msingi ambayo nadhani ni matokeo ya kuwa na Katiba ambayo haionyeshi wajibu kwa viongozi wetu.
Hakuna la ajabu kwenye hii ripoti kwani ni Mtanzania gani asiyejua jina la Chenge,Ngereja,Daniel na wengine wengi ni jinsi gani wameshiriki katika kuiingiza nchi hii katika matatizo hayo kwa ajili ya matakwa yao binafsi na ya Kichama?.
 
engine rock

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,198
2,000
Tangu ile ripoti ya kwanza na hii ya leo, Kamati zote mbili zimewasaidia watanzania kubaini kuwa CCM si ya kuaminika, haifai kuongoza nchi, haina dhamira ya dhati ya kusaidia taifa hili, na viongozi wengi wa CCM ni wapiga dili.

Serikali ya CCM ndiyo iliyoileta kampuni ya Accacia nchini, wakaipa mgodi bila kusajiliwa BRELA, CCM ikatumia idadi kubwa ya wabunge wake bungeni kuruhusu wawekezaji wa madini (including Accacia) kuchukua 96% ya gross income na taifa kuambulia 4% tu.

Mambo haya yaliyoongelewa kwenye kamati leo na ile kamati ya kwanza, yamekua yakiongelewa na vyama vya upinzani kwa miaka mingi lakini CCM na wafuasi wake wakiwabeza wapinzani. Leo Kamati hizi zinaongea lugha ileile iliyoongelewa na upinzani kwa miaka mingi, wafuasi walewale wa CCM waliobeza ndio wako mstari wa mbele kushangilia. Upuuzi wa kiwango cha shahada ya uzamivu.!!

Labda niwaambie tu kuwa chanzo cha yote haya si makinikia, wala si Accacia kutokusajiliwa. Chanzo cha yote haya ni mikataba ya hovyo iliyopitishwa na wabunge wa CCM kwa wingi wao bungeni. Kwa hiyo kama tunataka kusaidia taifa hili dawa si kukenua meno kumsifia Rais, dawa ni kurudisha mikataba yote bungeni, ikafumuliwe na kusukwa upya kwa maslahi ya taifa. Vinginevyo tunapoteza muda kusikiliza vitu visivyotoa promising future.

[HASHTAG]#NiniKifanyike[/HASHTAG]:

1. CCM na serikali yake wanapaswa kuwaomba radhi watanzania kwa kushiriki kuiba au kusaidia wezi wa kimataifa kuiba rasilimali za nchi (madini ni kielelezo tu, lakini CCM wameuza rasilimali nyingi kuliko madini. Sekta ya utalii, uvuvi, gesi huko balaa ni kubwa zaidi).

2. Serikali ya CCM wakubali kubeba lawama zote zinazotokana na hasara hii kubwa kwa taifa.

3. Mikataba yote ya madini na mikataba mingine inayohusu rasilimali za taifa (kama utalii, gesi, vitalu vya uwindaji, Uvuvi, nishati etc) irudishwe bungeni ikafumuliwe na kusukwa upya kwa kulinda maslahi ya taifa.

4. Naibu Waziri wa Madini Dr.Medard Kalemani (ambaye alibakizwa baada ya Waziri Muhongo na Katibu Mkuu kuondolewa) nae aondolewe. Ikumbukwe Kalemani alikua wizara ya nishati na madini tangu mwaka 1999 akishika nafasi mbalimbali wizarani hapo. Amekuwa Afisa Mwandamizi wa Sheria (Seniour Legal Officer), Mkurugenzi wa sheria kwa nyakati tofauti. Maana yake ni kwamba alihusika kwa namna moja au nyingine na mikataba hii mibovu iliyotuingizia hasara kama taifa.

5. Mwaka 2020 CCM waamue wenyewe kuondoka madarakani kwa kutosimamisha mgombea Urais, maana wamepoteza uhalali wa kuendelea kuongoza. Vinginevyo wananchi wawaondoe madarakani kwa nguvu ya kura.!
Watakuelewa kweli?
 
fattys

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
669
500
I second you brother. Although it is too late. Baada ya kutapapata kwa muda mrefu Rais Magufuli amesema ukweli na Mikataba yote ya Uchimbaji wa Madini sasa itakuwa wazi na itapelekwa Bunguni kujadiliwa. Amsema hata ikibidi Bunge kuongeza muda wa Kikao chake wafanye hivyo ili Mikataba hiyo irekebishwe
 
samora10

JF-Expert Member
Jul 21, 2010
7,558
2,000
Naona Kinara wa huu wizi ndio anaongoza muhimili wa Tatu leo! CCM ni janga la kitaifa tusijidanganye
 
Mlandula Jr

JF-Expert Member
Jan 3, 2016
1,718
2,000
Tangu ile ripoti ya kwanza na hii ya leo, Kamati zote mbili zimewasaidia watanzania kubaini kuwa CCM si ya kuaminika, haifai kuongoza nchi, haina dhamira ya dhati ya kusaidia taifa hili, na viongozi wengi wa CCM ni wapiga dili.

Serikali ya CCM ndiyo iliyoileta kampuni ya Accacia nchini, wakaipa mgodi bila kusajiliwa BRELA, CCM ikatumia idadi kubwa ya wabunge wake bungeni kuruhusu wawekezaji wa madini (including Accacia) kuchukua 96% ya gross income na taifa kuambulia 4% tu.

Mambo haya yaliyoongelewa kwenye kamati leo na ile kamati ya kwanza, yamekua yakiongelewa na vyama vya upinzani kwa miaka mingi lakini CCM na wafuasi wake wakiwabeza wapinzani. Leo Kamati hizi zinaongea lugha ileile iliyoongelewa na upinzani kwa miaka mingi, wafuasi walewale wa CCM waliobeza ndio wako mstari wa mbele kushangilia. Upuuzi wa kiwango cha shahada ya uzamivu.!!

Labda niwaambie tu kuwa chanzo cha yote haya si makinikia, wala si Accacia kutokusajiliwa. Chanzo cha yote haya ni mikataba ya hovyo iliyopitishwa na wabunge wa CCM kwa wingi wao bungeni. Kwa hiyo kama tunataka kusaidia taifa hili dawa si kukenua meno kumsifia Rais, dawa ni kurudisha mikataba yote bungeni, ikafumuliwe na kusukwa upya kwa maslahi ya taifa. Vinginevyo tunapoteza muda kusikiliza vitu visivyotoa promising future.

[HASHTAG]#NiniKifanyike[/HASHTAG]:

1. CCM na serikali yake wanapaswa kuwaomba radhi watanzania kwa kushiriki kuiba au kusaidia wezi wa kimataifa kuiba rasilimali za nchi (madini ni kielelezo tu, lakini CCM wameuza rasilimali nyingi kuliko madini. Sekta ya utalii, uvuvi, gesi huko balaa ni kubwa zaidi).

2. Serikali ya CCM wakubali kubeba lawama zote zinazotokana na hasara hii kubwa kwa taifa.

3. Mikataba yote ya madini na mikataba mingine inayohusu rasilimali za taifa (kama utalii, gesi, vitalu vya uwindaji, Uvuvi, nishati etc) irudishwe bungeni ikafumuliwe na kusukwa upya kwa kulinda maslahi ya taifa.

4. Naibu Waziri wa Madini Dr.Medard Kalemani (ambaye alibakizwa baada ya Waziri Muhongo na Katibu Mkuu kuondolewa) nae aondolewe. Ikumbukwe Kalemani alikua wizara ya nishati na madini tangu mwaka 1999 akishika nafasi mbalimbali wizarani hapo. Amekuwa Afisa Mwandamizi wa Sheria (Seniour Legal Officer), Mkurugenzi wa sheria kwa nyakati tofauti. Maana yake ni kwamba alihusika kwa namna moja au nyingine na mikataba hii mibovu iliyotuingizia hasara kama taifa.

5. Mwaka 2020 CCM waamue wenyewe kuondoka madarakani kwa kutosimamisha mgombea Urais, maana wamepoteza uhalali wa kuendelea kuongoza. Vinginevyo wananchi wawaondoe madarakani kwa nguvu ya kura.!
Mimi nakubaliana na wewe katikahili asilimia mia moja.
 
Malo Robi

JF-Expert Member
May 16, 2017
306
500
Naona shetani kazeeka sasa anaelekea kwenye umalaika.
Maajabu ya CCM ni pale unapomkuta mwanaccm anahudhunika as if kipindi cha bunge alikuwa siyo yeye. Rais, Makamu wake, Waziri mkuu na spika woote wanajua nguvu wanayotumiaga kupitisha na kuhalalisha uozo bungeni. Tusilete hisia zisizo na msingi eti tumeibiwa mno. Mimi nakataa hatujaibiwa ila tumegawa kwa moyo wetu mweupe. Sheria na mikataba ccm ndo waasisi. Ni mjinga pekee atakaye simama na kumsifia Rais eti kafanya jambo ajabu. Hilo ni jukumu lake kama Rais kulinda rasilimali zetu ndo maana tunamlipa malupulupu na mshahara mnono. Wameharibu kupitia mikataba na sheria mbovu afu leo wanataka kutumia obovu huo kujiweka mstari wa mbele kuwa na uchungu na mali za taifa. Ni upumbavu wa hali ya juu ambayo haijawahi tokea. CCM atangazwe kama ADUI namba moja wa taifa letu na wasijikoshe kwa Ripoti zao za kipumbafu wakati kipindi wanaweka hii mikataba na sheria mbovu kuna watu walipiga kelele wakafukuzwa bungeni na adhabu kadhaa kisa wanaingilia hii mtaji wa ccm. Rais asijikoshe kuwa na uchungu wakati alionao pembeni pamoja na yeye mwenywe ndo adui wa taifa.
Nimesikitika sana leo Rais anaagiza Spika wa bunge mbumbumbu asiyejielewa ndugai kumpa agizo la kuruhusu kufanyiwa kwa amendment za sheria za madini huku akimpa na jukumu la kuwaziba mdomo na kuwashughulikia wapinzani watakao ongea bungeni kwamba awaondoe na wakiongea nje Rais atawashugulikia! Hapo ndo ninapoona hii kitu si uzalendo bali ni kick kwa pikipiki!
Hivi kuna mbunge gani wa ccm mwenye uwezo wa hata robo ya michango adhimu kama ya tundu lisu, lema na wengine wadogo wenye udhubutu wa kukosoa hadharani? Msukuma, Mlinga au prof wa mil 20 za mboga????
Tuzinduke kama taifa kupinga kwa nguvu zote utawala wa CCM maana ni janga na watesaji wakubwa wa watanzania.
 
Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
13,409
2,000
Siyo kuomba radhi wafungwe wote.
Ukisema hivyo ni pamoja na rais maana naye pamoja na kuonesha uchungu alikuwepo yeye mwenyewe huwa anasema kwa miaka 20 yumo ndani ya serikali na huwa anasema aliyafahamu haya!
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
42,803
2,000
Ukisema hivyo ni pamoja na rais maana naye pamoja na kuonesha uchungu alikuwepo yeye mwenyewe huwa anasema kwa miaka 20 yumo ndani ya serikali na huwa anasema aliyafahamu haya!
Uliza alichowafanyia Halmashauri ya Chatto ndiyo utajua una Rais wa aina gani.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom