CCM na Serikali tutaendelea kuwavumilia wakosoaji wetu lakini si wanaovuruga amani yetu

Fukua

JF-Expert Member
Jun 1, 2022
546
479
Wavuruga amani ni:

Wale wanaokosoa kwa matusi, wanaotugawa utanzania wetu kikabila, kikanda,kidini, huyu ni mzanzibar na huyu ni mtanganyika n.k.

Wanaopinga Kila jambo jema kwa nchi yetu mfano huu mkataba wa Tz na DP World kuhusu bandari zetu.

Wanaoshambulia hoja wasizozipenda kwa matusi makubwa hadharani na huku mitandaoni.

Wanaokashfu na kuibagaza serikali na raisi wetu kwa uongo na ulaghai, maana wanahatarisha usalama wa nchi kwa kuzua taharuki kwa wananchi.

Na wengine wafananao na hao.

Nchi yetu ni huru na Ina uhuru wa kutosha kabisa Sasa kama uhuru wetu unatupelekea kukosa heshima na ustaarabu basi ni uhuru usiofaa hata kidogo.

Ni waombe watanzania hasa wa kwenye mitandao tujadiliane hoja kwa hoja na kistaarabu. Maana unapotukana watu hovyo kwenye mitandao siku sheria zikichukuliwa dhidi Yako utabaki peke yako

Nina ipongeza CCM na viongozi wake kwa uvumili mkubwa kwa baadhi ya watz wapenda matusi, vurugu na ujinga ujinga wa kutosha. Miaka zaidi ya 60 SI mchezo.

CCM oyee

Mama anaupiga mwingi na nchi imefunguka.
 
Kwa hiyo sasa ndo unataka iweje?

CCM wanaowakejeli na kuwadharau Watanzania kuwa hawana akili nao wanadumisha amani?


Hangaya ameshaprove kufeli. Je hapo unasemaje
Ccm inawahesimu na kuwajali watanzania wote kwani ndio waliyoiweka madarakani. Na hili huwalinathibitishwa kwenye chaguzi ambazo ccm hupewa kura nyingi za kishondo
 
Umeshindwa kujua hata Amani huwa inavurugwa namna gani,umeandika mistari kibao alafu hujui unaongea nn.very poor.
Nimetumia lugha rahisi Ili nieleweke lkn pia hapa tunajadili hoja kama una maoni Yako kuhusu mambo yanavunja amani tuwekee hapa Kuna watu wengi watachanganua na kujifunza mkuu usiishie kubaki na maarifa Yako tu hapa Kuna wasomaji wengi tofauti tofauti SI CCMna CHADEMA tu
 
Nimetumia lugha rahisi Ili nieleweke lkn pia hapa tunajadili hoja kama una maoni Yako kuhusu mambo yanavunja amani tuwekee hapa Kuna watu wengi watachanganua na kujifunza mkuu usiishie kubaki na maarifa Yako tu hapa Kuna wasomaji wengi tofauti tofauti SI CCMna CHADEMA tu
Pale ulipo ww ss tulishatoa mguu zamani kaka.Watanzania wana Akili sana ndio maana unaona wanahoji mambo ya msingi kwa Taifa lao.Wamebaki wachache wasioelewa.
 
Back
Top Bottom