CCM na mkakati wa kuharibu katiba

CCM na mkakati wa kuharibu katiba

MLONDWE

Member
Joined
Mar 18, 2013
Posts
30
Reaction score
12
Leo tumechapisha katika gazeti hili habari ya kusikitisha kwamba Waraka wa CCM kwa wanachama wake kushinikiza watetee matakwa ya chama hicho wakati wakitoa maoni yao katika Mabaraza ya Katiba, umezua mtafaruku mkoani Iringa, baada ya Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Said El-Maamry kumzuia mmoja wa wajumbe wa Mabaraza hayo kutumia waraka huo kutoa maoni.

Mjumbe huyo wa Tume alimzuia mmoja wa wajumbe waliokuwa wakichangia maoni kwenye mapendekezo ya Rasimu ya Kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kubaini kwamba alichokuwa akichangia kilitokana na maelekezo ya CCM kama yalivyo katika Waraka uliotokana na kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho iliyokutana mjini Dodoma, Juni 10, mwaka huu.

Tunasema habari hizo ni za kusikitisha kwa sababu mbili kubwa. Kwanza, mjumbe huyo wa Tume alikuwa anatimiza wajibu wake kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa kuhusiana na uendeshaji wa Mabaraza hayo, lakini hatua yake hiyo ilizua tafrani kubwa, kwani baada ya mjumbe huyo wa Baraza la Katiba kutoridhishwa na hatua ya kuzuiwa kutoa maoni kwa kukariri Waraka wa CCM, alishinikiza wajumbe wa mkutano huo wamfukuze Mjumbe huyo wa Tume sio tu kwa kile alichoeleza kwamba anapingana na maelekezo ya Tume ya kuwaacha wananchi watoe mawazo yao kwa uhuru, bali pia kwamba wajumbe wenzake hawakuwa na imani naye.

Pili, habari hizo zinasikitisha kwa sababu chanzo cha mtafaruku huo ni CCM, ambacho ndicho chama tawala kilichounda Serikali iliyo madarakani. Kimsingi, Serikali ya chama hicho ndio iliyoamua nchi yetu ipate Katiba mpya na ilihakikisha sheria husika inatungwa na kupitishwa na Bunge. Hivyo, chama hicho kingetegemewa kiwe mfano bora kwa kuheshimu na kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa katika mchakato mzima wa kupata Katiba mpya.

Hivyo, lilikuwa jambo la kushangaza kuona chama hicho kikitoa Waraka wa kuwaelekeza wanachama wake nini cha kusema na vifungu gani vya Rasimu hiyo wavikubali na vipi wavikatae. Waraka huo wa kurasa 32 hakika unabeba matakwa na masilahi ya viongozi wa chama hicho, mbali na kuwapora wanachama wake haki na uhuru wa kuamua nini kiingizwe katika Katiba mpya na nini kiachwe.

Sasa tunaelewa kwa nini baadhi ya watu wanakuwa kama kasuku wanapotoa mapendekezo na pia kwa nini baadhi yao walitoa rushwa na kutumia udini ili wachaguliwe kuingia katika Mabaraza hayo ya Katiba. Kumbe walitegemea kwamba wingi wa kura za wajumbe wa itikadi moja katika mabaraza hayo ndio ungeamua hatima na mwelekeo wa Katiba mpya.

Vitimbwi tunavyoendelea kushuhudia, kikiwamo hiki cha CCM kuandaa Waraka wa kuwalazimisha wanachama wake kutoa maoni kwa kuzingatia matakwa ya viongozi wake vinatia wasiwasi kama kweli mwishowe itapatikana Katiba iliyoridhiwa na wananchi au Katiba ya viongozi kama zile zilizotangulia.

Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliagiza na kuonya kwamba wananchi waachwe watoe maoni yao kuhusu Katiba wanayoitaka pasipo kuingiliwa au kushawishiwa na mtu au chombo chochote. Tume pia ilisema wingi wa kura za watu wenye itikadi moja katika Mabaraza hayo hakitakuwa kigezo katika kuandika Katiba mpya. Tunakubaliana na Tume pale inaposisitiza kwamba itazingatia uzito wa hoja na sio wingi wa hoja.
 
kuna shida gani kutetea msimamo wa chama chake? kwani mtu maoni yake hawezi kuyasoma kwenye karatasi yake aliiyoiandika?
 
Hivi kumbe katiba ni ya chama?
 
kuna shida gani kutetea msimamo wa chama chake? kwani mtu maoni yake hawezi kuyasoma kwenye karatasi yake aliiyoiandika?

Kwani katiba inaundwa ya chama hapa au ya nchi nzima? Si wakatoe mapendekezo ya kuandika katiba yao ya CCM
 
mbona walemavu, vijana na dini wanatoa misimamo yao kwani katiba ni ya walemavu au vijana au dini?

kuna shida gani kutetea msimamo wa chama chake? kwani mtu maoni yake hawezi kuyasoma kwenye karatasi yake aliiyoiandika?

Katiba sio matakwa ya chama bali yenye maslahi kwa watu wote wa nchi hii.
 
Wameshindwa kuandika upya katiba ya chama chao, halafu wanajifanya wajuaji.
 
Ukwaju Chama hiki ni hatari sana kina jivunia wingi wa wajumbe wake
 
Last edited by a moderator:
Siasa za busara CCM hawaziwezi,dawa ni kuwatoa kwa mtutu
 
kuna shida gani kutetea msimamo wa chama chake? kwani mtu maoni yake hawezi kuyasoma kwenye karatasi yake aliiyoiandika?
Akatetee msimamo wa chama chake kwenye kuunda katiba ya chama, si ya nchi... Inavyooneka, CCM wapo tayari kuleta katiba ya chama chao iwe ndo rasimu.... Sasa kama kila mtu akiletetea msimamo wa chama chake, unadhani mwisho wake ni nini...???
 
Leo tumechapisha katika gazeti hili habari ya kusikitisha kwamba Waraka wa CCM kwa wanachama wake kushinikiza watetee matakwa ya chama hicho wakati wakitoa maoni yao katika Mabaraza ya Katiba, umezua mtafaruku mkoani Iringa, baada ya Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Said El-Maamry kumzuia mmoja wa wajumbe wa Mabaraza hayo kutumia waraka huo kutoa maoni.

Mjumbe huyo wa Tume alimzuia mmoja wa wajumbe waliokuwa wakichangia maoni kwenye mapendekezo ya Rasimu ya Kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kubaini kwamba alichokuwa akichangia kilitokana na maelekezo ya CCM kama yalivyo katika Waraka uliotokana na kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho iliyokutana mjini Dodoma, Juni 10, mwaka huu.

Tunasema habari hizo ni za kusikitisha kwa sababu mbili kubwa. Kwanza, mjumbe huyo wa Tume alikuwa anatimiza wajibu wake kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa kuhusiana na uendeshaji wa Mabaraza hayo, lakini hatua yake hiyo ilizua tafrani kubwa, kwani baada ya mjumbe huyo wa Baraza la Katiba kutoridhishwa na hatua ya kuzuiwa kutoa maoni kwa kukariri Waraka wa CCM, alishinikiza wajumbe wa mkutano huo wamfukuze Mjumbe huyo wa Tume sio tu kwa kile alichoeleza kwamba anapingana na maelekezo ya Tume ya kuwaacha wananchi watoe mawazo yao kwa uhuru, bali pia kwamba wajumbe wenzake hawakuwa na imani naye.

Pili, habari hizo zinasikitisha kwa sababu chanzo cha mtafaruku huo ni CCM, ambacho ndicho chama tawala kilichounda Serikali iliyo madarakani. Kimsingi, Serikali ya chama hicho ndio iliyoamua nchi yetu ipate Katiba mpya na ilihakikisha sheria husika inatungwa na kupitishwa na Bunge. Hivyo, chama hicho kingetegemewa kiwe mfano bora kwa kuheshimu na kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa katika mchakato mzima wa kupata Katiba mpya.

Hivyo, lilikuwa jambo la kushangaza kuona chama hicho kikitoa Waraka wa kuwaelekeza wanachama wake nini cha kusema na vifungu gani vya Rasimu hiyo wavikubali na vipi wavikatae. Waraka huo wa kurasa 32 hakika unabeba matakwa na masilahi ya viongozi wa chama hicho, mbali na kuwapora wanachama wake haki na uhuru wa kuamua nini kiingizwe katika Katiba mpya na nini kiachwe.

Sasa tunaelewa kwa nini baadhi ya watu wanakuwa kama kasuku wanapotoa mapendekezo na pia kwa nini baadhi yao walitoa rushwa na kutumia udini ili wachaguliwe kuingia katika Mabaraza hayo ya Katiba. Kumbe walitegemea kwamba wingi wa kura za wajumbe wa itikadi moja katika mabaraza hayo ndio ungeamua hatima na mwelekeo wa Katiba mpya.

Vitimbwi tunavyoendelea kushuhudia, kikiwamo hiki cha CCM kuandaa Waraka wa kuwalazimisha wanachama wake kutoa maoni kwa kuzingatia matakwa ya viongozi wake vinatia wasiwasi kama kweli mwishowe itapatikana Katiba iliyoridhiwa na wananchi au Katiba ya viongozi kama zile zilizotangulia.

Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliagiza na kuonya kwamba wananchi waachwe watoe maoni yao kuhusu Katiba wanayoitaka pasipo kuingiliwa au kushawishiwa na mtu au chombo chochote. Tume pia ilisema wingi wa kura za watu wenye itikadi moja katika Mabaraza hayo hakitakuwa kigezo katika kuandika Katiba mpya. Tunakubaliana na Tume pale inaposisitiza kwamba itazingatia uzito wa hoja na sio wingi wa hoja.

taifa ni muhimu zaidi kuliko chama na maslahi binafsi.ila nashangaa kuna wapumbavu wengine wako tayari kutumika kutetea chama kuliko taifa.wanajali vijisenti viwili wanavyopewa bila kujali watakufa njaa kwa miaka mingi zaidi baada ya kutetea upumbavu wao huo.kuna wakati naamini kuna watu wengine ni misukule.mfanomwaka 2011 katikati nilibahatika kufika eneo linaloitwa pongwe-msungura kwa uelekeo wa chalinze kwenye training moja hivi kuhusu xplosions,kuanzia chalinze njia nzima ukimuona mwanamke kajifunga kanga au kilembe kichwani basi ni cha kijani chenye maneno "chagua ccm,chagua kikwete"nilijiuliza sana kwanini hawa watu wote wamevaa hivi,mara ya kwanza nilidhani ni ushabiki wa kichama lakini wakati wa kurudi baada kusimama kununua vijizawadi vidogo vidogo kwa ajili ya familia ilibidi niulize wenyeji....jibu nililopewa nilichoka sana....hawana cha kuvaa zaidi ya hivyo vikanga,vilemba na vitisheti walivyonunuliwa navyo wakati wa uchaguzi.niliwahurumia sana kwani kijikanga cha buku 5 kinamfanya agawe maisha kwa miaka 5.baada ya hapo anaanza kulia umaskini,hela hamna,karo za shule,dawa hamna hospitali etc etc.sasa na ndo baadhi ya wapumbavu flani ambao wanajua kutetea maslai ambayo hata wao hawata faidika nayo.bora hata wa huko chalinze tunaweza kusema hawana elimu ya kutosha ya kujitambua
 
Hi ni another poor...very poor move from ccm....huwezi kuwa agaist wananchi kwa miaka ya sasa....utapata maumivu....poor stratergy from ccm......Nauliza swali tena HAKUNA MTU MWENYE AKILI TIMAMU HUKO CCM KWA SASA...??
 
kuna shida gani kutetea msimamo wa chama chake? kwani mtu maoni yake hawezi kuyasoma kwenye karatasi yake aliiyoiandika?

Hapo unakua unatetea chama au watanzania? Acha ukilaza, fikiri nje ya box!Matakwa ya CCM na CDM si matakwa ya Watanzania. CCM wanataka kutawala nchi siku zote na kulinda maslahi ya viongozi wabadhirifu baada ya uongozi wao! Ni suala la kutetea hilo? Macho ka goroli za mchina!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
mbona walemavu, vijana na dini wanatoa misimamo yao kwani katiba ni ya walemavu au vijana au dini?

Wewe unatetea nini na utimamu wako? Unataka ushikiwe akili pia? Katiba ni kwa maslahi ya taifa zima ndugu. Hii nafasi ikichezewa hutaipata tena maisha yako yote. Akili za kuambiwa changanya na za kwako. Huo usemi nadhani sijakosea.
 
Tunahitaji chama cha kutuletea mfumo bora,tukiwa na mfumo bora mambo yote yatakaa sawa hata wananchi watakuwa na maisha bora,lakini kama mfumo utaendelea kuwa huu uliokuwepo basi nchi tutaendelea kuwa wapumbavu,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom