Ninadhani sifa kuu ya wana CCM ni kulinda maslahi ya chama chao kwa nguvu zote. Hii inatokana na maamuzi ya CC-CCM ya hivi majuzi kuwashughulikia viongozi wa Jumuiya ya Wazazi na Katibu wa CCM wa Mkoa wa Singida. Leo hii nimeshangaa kuona news hii kwamba UWT nako moto unawaka kisa MKATABA wa ukodishaji wa kitega uchumi chao. Kinachoshangaza hao hao vigogo wa UWT na CC-CCM (wengi wao wamo Bungeni na baadhi ni viongozi waandamizi ndani ya serikali) ukiwaomba mikataba ya serikali ichunguzwe wanakuwa wakali kama nyuki. Hivi hii double standard inatupeleka wapi nchi hii? Hivi kitendo cha serikali kuwa na msimamo wa kugoma kuchunguzwa mikataba na ubadhirifu wa mambo mbali mbali ambayo yameongelewa sana, haioni kwamba inapoteza credibility yake kwenye macho ya wananchi? Iweje leo fedha za CCM ziwe muhimu sana kiasi cha kufukuzana/kusimamishana uongozi ilihali waliotafuna hela za umma tena mabilioni ya kumwaga wanaendelea kutesa mtaani na wako "comfortable" wala hawana pressure. Ina maana kula hela ya CCM ni dhambi kubwa sana na kula hela ya serikali siyo kosa? JK anatupeleka wapi na CCM yake? Afadhali hizo habari za ndani ya CCM zingebaki kuwa siri yao ili wananchi tusijue na tukabaki na imani kwamba labda awamu ya nne haioni kama kuna ufisadi iwe serikalini au kwenye chama chao. Hii ni aibu kubwa kwa uongozi wa CCM na aibu kwa viongozi wa serikali kwa kuwa JK ni president na cheamani wa CCM, akina EL na wengineo ni wajumbe wa CC-CCM na PM pia. Habari kamili hii hapa chini:
Kwa vingunge wa CCM maslahi ya chama ni muhimu sana kuliko maslahi ya nchi. Kweli tutafika?UWT kwawaka Baraza likijadili viongozi Dodoma
*Chanzo ni ukodishaji City Ambassador
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
SIKU chache baada ya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kusimamisha uongozi wa juu wa Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho kwa tuhuma za ubadhirifu, na kisha Kamati ya Utekelezaji ya jumuiya hiyo kujiuzulu, mambo si shwari ndani ya Umoja wa Wanawake Tanzania UWT, ambapo uongozi wa juu wa umoja huo uko matatani baada ya kusemekana kusaini mkataba usiozingatia maslahi yao.
Taarifa zilizopatikana jana mjini hapa zimeeleza na kuthibitishwa na baadhi ya viongozi wa umoja huo kuwa mmoja wa viongozi wa ngazi za juu huenda akasimishwa kutokana na tuhuma za kusaini mkataba wa ukodishaji wa jengo la kitega uchumi la UWT la City Ambassador, lililopo karibu na kona ya barabara za Kawawa na Ali Hassan Mwinyi.
Kutwa nzima ya jana, Baraza Kuu la UWT lilikuwa katika harakati za mkutano wa kulijadili suala hilo na mara kadhaa, mmoja wa viongozi wa umoja huo, alikuwa akitolewa nje wakati Baraza likimjadili. Pia alitolewa nje ya kamati ya utekelezaji ya umoja huo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, kikao cha baraza hilo kilitawaliwa na mvutano ambao msingi mkubwa ni kile kinachoonekana kutoshirikishwa na au kutozingatiwa kwa maslahi ya umoja huo pamoja na ya chama. Kikao kilendelea kwa muda mrefu hadi usiku.
Hivi karibuni Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiliusimamisha uongozi wa juu wa Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho kwa tuhuma za ubadhirifu. Miongoni mwa watu waliosimamishwa na Kamati Kuu (CC) ndani ya jumuiya hiyo kwa tuhuma za ubadhirifu ni pamoja na Mwenyekiti, Abihudi Maregesi, Makamu wake Ramadhani Suleiman Nzori na Katibu Mkuu, Cosmas Hinju.
Umoja wa Wanawake, Jumuiya ya wazazi na Umoja wa Vijana (U-CCM) ni mihimili muhimu ya CCM, ambayo nayo ni mhimili wa muhimu chama hicho.
Tangu kuundwa kwa CCM Februari 5, mwaka 1977, baada ya kuvunjwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shiraz (ASP), jumuiya hizo zimekuwa nguzo muhimu suala lolote linalozigusa jumuiya hizo ni suala la chama.