Zikomo Songea
JF-Expert Member
- May 15, 2016
- 670
- 582
Wakuu, salaam. Ni juzi tu, siku ya Alhamis, mkuu Allen Kilewela alipost thread iliyokuwa na kichwa cha habari "Ubunge wa Msigwa Waivurunga CCM Iringa Mjini" (mnaweza kuirejea).
Pamoja na mambo mengine, mtoa mada alijikita katika kuonyesha kuwa kitendo CCM kushindwa kumwondoa Msigwa kwenye kiti cha ubunge jimboni humo, licha ya juhudi za muda mrefu na mbinu mbalimbali, kinaelekea kudhoofisha chama hicho kikongwe cha siasa nchini. Katika mchango wangu nilieleza juu juu ugumu wa siasa za Iringa mjini.
Leo Mh. Peter Msigwa (Mb) amefanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mwembetogwa mjini. Kinyume kabisa na matarajio ya wengi, mkutano ulihudhuriwa na watu wengi sana, hali iliyonikumbusha kampeni za mwaka 2015. Najiuliza, hii inatoa ishara gani kwa CCM? Nashawishika kuamini kuwa CCM italazimika kusubiri "moshi mweupe" kwa muda mrefu zaidi ya uliotarajiwa. Karibuni kwa mjadala.