mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,307
- 6,514
Tyranny of the majority ni nadharia ya upepo mbaya wa kidemokrasia. Kwamba watu wengi wanasombwa na upepo kuhusu mtu fulani kutokana na ushawishi batili.
Upepo huo mbaya, unaweza kusababishwa na kiongozi anayetumia uelewa mdogo wa watu kujijenga kisiasa na kijamii, akizusha mambo au kusingizia watu.
Nadharia ya kiongozi kujipatia umaarufu kwa njia zisizofaa inaitwa demagogue.
Vyama na hata mamlaka za nchi mbalimbali huamua kudhibiti tyranny of the majority kwa kutoruhusu wapigakura kuchagua moja kwa moja.
Mfano Marekani, wananchi hawapigi kura ya moja kwa moja kuchagua Rais. Isipokuwa wajumbe 538 wa kura za majimbo (Electoral College), ndiyo huchagua Rais.
CCM NA TYRANNY OF THE MAJORITY
Tyranny of the majority, vilevile huitwa tyranny of the masses. Hii ndiyo ambayo CCM ikiongozwa na Dk Jakaya Kikwete walipambana nayo dhidi ya Edward Lowassa.
Lowassa alikuwa mtu pendwa sana ndani ya CCM. Kama angeachwa agombee na wajumbe wapige kura za kidemokrasia, hakuna ambaye angemzuia kupata tiketi ya kuwa mgombea urais wa CCM 2015.
Viongozi wa juu CCM waliitumia kamati ya maadili kumkata Lowassa kabla hajafika Kamati Kuu. Hivyo, wajumbe CCM walitakiwa kuchagua kati ya waliokubalika na viongozi.
DEMOKRASIA
Kudhibiti tyranny of the masses ni kuzuia sauti za wengi. Hivyo, huwezi kufanikisha hilo bila watu kulalamika na wengine kupinga.
Kupingana ndani ya chama ni demokrasia. Kutaka watu wanyamaze na wasiseme hisia zao ni kujenga chama kibaya.
Sophia Simba, Adam Kimbisa na Emmanuel Nchimbi, walipinga Lowassa kukatwa. Ilikuwa haki yao kidemokrasia.
Wajumbe wa Nec CCM wengi wao waliimba "tunaimani na Lowassa", wimbo huu ulimuudhi na unaendelea kumkera Rais Magufuli.
Hata hivyo, Rais wetu atambue kuwa hiyo ndiyo gharama ya demokrasia. Lazima upingwe na watu.
MAPOKEO
Kama waliofukuzwa, walioondolewa uongozi na walioonywa sababu ni kumtaka Lowassa ni ukatili wa demokrasia.
Ikiwa watu hao hata baada ya chama kupitisha jina la mgombea urais, waliasi na kusaliti kwa kukipiga vita chama kishindwe na Lowassa aliyegombea urais kwa tiketi ya Chadema, hapo ni halali kufukuzwa.
Nchimbi, Simba na Kimbisa walibaki CCM na walimfanyia kampeni Rais Magufuli. Kufukuzwa, kupewa onyo, na Kimbisa kusamehewa, ni kutaka ionekane kupinga ndani ya chama ni uasi.
Hivyo, waliofukuzwa ingetolewa maelezo jinsi walivyokihujumu chama, na kusaidia ushindi kwa wapinzani, maana hilo ni kosa la kutosha kufukuzwa uanachama.
Endapo ni yaleyale ya 2015, kilichotokea ni uonevu, na ukandamizaji wa demokrasia.
Ndimi Luqman MALOTO