CCM na Fikra Tegemezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM na Fikra Tegemezi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Worshiper, Oct 13, 2012.

 1. T

  The Worshiper JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 301
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  “Ni afadhari kuumbwa mwili wote kuwa mgongo kuliko kuwa tegemezi kifikra na kimawazo kwani kwako ubongo hauna maana”.Ndivyo unavyoweza kuutumia msemo huu kuelezea hali ilivyo ndani ya CCM,viongozi wa CCM ile kazi na majukumu yanayofanywa na kichwa(ubongo) katika kufikiri na kuwaza wameyatelekeza na kuwa tegemezi katika kubeba fikra na mawazo ya watu wengine.Kwao majukumu ya ubongo na kichwa si kitu cha msingi sana kwasasa kwa maana hawakishughulishi na hawakitumii katika kujenga fikra na mawazo yao wenyewe isipokuwa kubeba ya wengine (upinzani).CCM imebadilisha matumizi ya kichwa na ubongo na kuwa kama ya mgongo kubeba fikra na mawazo ya vyama vingine.Hapa ubongo na mgongo wa CCM vinafanya kazi zinazofanana(kubeba).

  Mambo mengi CCM imekuwa ikiigiza kutoka vyama vya upinzani,mara nyingi wamekuwa wakisubiri upinzani wamefanya nini na wao ndiyo wafanye.Uwezo wao wa ubunifu (Creativity) na kufikiri (Thinking capacity)umekuwa ukishuka kwa kasi siku hadi siku.Hali hiyo imevamia hata hapa bungeni Dodoma huku wengi wa wabunge wao (CCM) wakionyesha udhaifu mkubwa wakiwa hawana jipya wakisubiri hoja zozote zinazoletwa na upinzani kwa kutumia wingi wao na kiti cha spika wazipinge na kuziunga mkono zile wasizozijua.

  Fikra na mawazo yao (CCM) ni yaleyale (mgando) yanayochosha miaka nenda rudi huku wakiwa wameshindwa kabisa kuzifanyia kazi sera zao chakavu.CCM inafahamu kwasasa uwezo na upeo wao katika kuendesha na kushughulikia mambo mbalimbali umeshuka(uko chini sana) lakini chakushangaza bado wanajifanya kuamini katika kushinda wakati mawazo na fikra zao zimeshashindwa tayari “You can never believe in POSITIVES while you think in NEGATIVES”.


  Naomba kuwasilisha!!!
   
 2. p

  politiki JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  That is a classic example of too much corrupt, kosa ambalo watanzania tutajilaumu CCM ikiondoka madarakani ni
  uharibifu watakaokuwa wamesababisha tutajiuliza why did we wait for so long to get rid of them ???
   
 3. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
Loading...