VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Mwaka 2006,Mfadhili wa Chuo cha Sayansi ya Uuguzi cha Bugando-Mwanza,Cornell Weill alitoa pendekezo. Kwamba,alidhamiria kuwalipia ada yote wanafunzi wote waliokuwa wakisoma Stashahada na masomo mengineyo. Pendekezo lake hilo alilipitishia kwa Mkuu wa Chuo hicho. Nakala ya Pendekezo hilo ilitumwa Wizara ya Afya pamoja na Wizara ya Elimu.
Nakala ilipopokelewa Serikalini,likawakera wengi. Ikasemwa kuwa kuwalipia wanafunzi wote ada zote ni kuwafanya wanafunzi hao wasisome. Kwamba wangebweteka na kujisahau. Mikakati kabambe ikapangwa ili kuzima Pendekezo la Weill. Wakati huo,wanafunzi wote wa Bugando walikuwa wakila bure vyakula bora kabisa. Nalo hilo likakwaza Serikali. Ikawa nongwa.
Ujumbe ulionijumuisha mimi ulitumwa Bugando haraka haraka ili kuzima endekezo hilo. Ujumbe huo ulibeba mikwara yote ya Serikali iliyoelekezwa kwa Mkuu wa Chuo na hata Bwana Weill ambaye kwa wakati huo alikuwapo Tanzania kusubiria jibu la Pendekezo lake hilo. Tukafika Mwanza na kuelekea Bugando.
Kwakuwa Mkuu wa Chuo alikuwa na taarifa za Ujumbe wetu,haraka kama radi akaitisha kikao baina yetu,uongozi wa Chuo na Weill aliyeambatana na Wasaidizi wake. Tukafikisha ujumbe wetu bila ya kupepesa macho wala kuona haya. Tukatema cheche kuwa Pendekezo hilo halikubaliki kwakuwa 'lingeathiri' elimu pale Bugando na nchini kwa ujumla. Lingezalisha wanafunzi na wazazi wavivu kwakuwa wangekuwa wamelipiwa ada yote na kula bure chuoni!
Lakini,Weill(Mmarekani aliyekuwa akisikiliza kwa makini sana) aliruhusiwa kulipia sehemu tu ya ada za wanachuo. Akasitishwa pia 'kuwalisha bure' wanachuo. Weill hakupinga. Akakubali na kuahidi kuendelea kuisaidia Bugando kadiri ya uwezo wake na kadiri atakavyoruhusiwa na Serikali. Kikao kikafungwa na ujumbe huo.
Sisi tukarejea Dar es Salaam kuendelea na kazi za kichama na kiserikali. Mnaonaje hapa wakuu? Si ni Serikali hii hii inayowasomesha wanafunzi vyuoni tena kwa asilimia 100 kwa baadhi yao? Watoto wa maskini wa Bugando wakapishana na bahati hii ya ufadhili wa jumla toka kwa Weill. Hatahivyo,bado Weill anaisadia Bugando kwa namna moja au nyingine.
'Dhambi' hii inanitesa hadi leo. Hiyo ndiyo CCM na Serikali yake!
VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba Dar es Salaam (sasa Dodoma)

Last edited by a moderator: