VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,006
Mimi, nilipokuwa mtoto mdogo kule Songea Ruvuma, nililelewa na shangazi yangu aliyeitwa Mwajuma. Shangazi Mwajuma alikuwa na demokrasia fulanifulani ya kiini macho. Wakati ule sikuwa na uelewa wa kutosha kuhusu demokrasia yake. Ya kwake haikuhusisha kupigwa kwa kura. Yake ilikuwa demokrasia ya kukisia na kependelea. Ilikuwa ya kulenga kupendelea mtoto fulani.
Kulenga mshindi au mfaidika hata kabla ya kutekelezwa kwa jambo. Hasa wakati wa kula. Kwa shangazi Mwajuma tulikuwa watoto watatu. Wawili wa kwake na mimi. Mimi nilikuwa wa katikati kiumri. Wote tulikuwa wavulana. Mkubwa kabisa na mdogo kabisa walikuwa wa kwake. Basi, Shangazi Mwajuma alikuwa akiwapendelea watoto wake kwa umahiri na kupokezana.
Mimi nilibaki kushangaa na kupitwa na demokrasia-kandamizi hiyo. Demokrasia iliyokuwa-kama hii ya CCM-ya kiini macho. Siwezi kumsahau Shangazi Mwajuma. Kuna siku, kukiwa na nyama, anadai kuwa mtoto wa kwanza achukue anazotaka kutoka kwenye bakuli ili kuonesha kuwa yeye ndye mkubwa wetu. Siku nyingine nafasi ya upendeleo hupewa mtoto wa mwisho (kiziwanda/kitindamimba). Kwa namna hiyo hiyo.
Ukubwani ndiyo nayaona yale ya Shangazi Mwajuma kupitia CCM. CCM imejaa demokrasia bandia na ya karata-tatu. Mlengwa hujitokeza tangu mwanzo hata kama hubezwabezwa. Kitendo cha leo cha wagombea wawili wa Uspika (Dr. Tulia Ackson na Bwana Abdullah Mwinyi) kujitoa na kumuacha pekee Bwana Job Yustino Ndugai kuwa mgombea wa Uspika kimenikumbusha Shangazi Mwajuma na demokrasia bandia yake.
Kulikuwa na haja gani wengine kuchukua fomu na hata kupitishwa na CC na NEC? Wabunge wa CCM wana nafasi gani tena kumchagua mgombea wa Uspika ikiwa mgombea amechaguliwa na Kamati Kuu ambayo ndiyo iliyochuja na kuacha majina matatu mwanzoni. CCM inacopy na kupaste demokrasia ya Shangazi Mwajuma!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)