CCM na CHADEMA sasa turudi kujadili solutions za issues muhimu kwa taifa letu!


Mlachake hapo pekundu unamtisha, Willy anayajua haya na nina uhakika anaongea na msure wake hali halisi ya chama chao, well kuitetea au kuisemea CCM kwa sasa lazima uwe na uwezo wa kumeza mfupa bila kutafuna, au kama ile sentesi ya kulisemea baba wa taifa kuhusu kulisemea Azimio la arusha....

Kujivua magamba kungeanza kipindi kile kile marehemu Kolimba (RIP) aliposema CCM sasa haina dira wala mwelekeo, sasa kadri siku zilivyopita ndiyo magamba yamekomaa na hayavuliki tena, chama kimebalidilshwa na kuwa cha matajiri na si wakulima na wafanyakazi.

CCM wana kazi kubwa mno, na kwa aina hii ya kasi ya kina NAPE sijui kabisa kama watakiokoa chama, naogopa kusema chama kinaweza kuwafika watu mikononi, bora wewe Malecela Jr unayeandika toka ughaibuni - yaani your safe.
 
CHADEMA wanafanya kazi ya siasa, CCM ndiyo wenye serikali wanatakiwa kutekeleza ahadi!! CHADEMA wao wanatekeleza kazi yao kama chama cha siasa!! achana na hizo Malecela.
 
angalia hii mpya ya mukama huko musoma, hivi ccm hoja zimeshawaishia? mbunge aibe madawati apeleke wapi? ayauze ? hahahaha h ah aha !!!!!
 

Willy huko uliko wewe unafurahia maisha na kula kuku kwa mrija
Njoo uone maisha halisi ya mtanzania na uingie kwenye siasa tupambane maana unapoongelea ukiwa mbali hakuna anayekusikia
Njoo kwenye uhalisia wa maisha ya kitanzania na uyaone maisha halisi ya kitanzania
Hayo ya kuongea katiba, utawala bora na mengineyo yanaongeleka kama wananchi wanajua mkate wao unatoka wapi maana kwenda kumuongelea katiba mpya au utawala bora mtu aliye na njaa ni kama kumtukana
 
CHADEMA wanafanya kazi ya siasa, CCM ndiyo wenye serikali wanatakiwa kutekeleza ahadi!! CHADEMA wao wanatekeleza kazi yao kama chama cha siasa!! achana na hizo Malecela.

umesema vyema Dullo ! Ccm waache porojo , watimize ahadi , CDM kazi yake nikuwasimamia ipasavyo mpaka kielewe.
 
watanzania wamegeuzwa omba-omba. Mzee mzima kaacha familia yake kwenda kuomba-omba khanga na vitenge kwa mgeni wa kijiji nape. Na amewaagiza wanafamilia wamuombee kwa mungu apate khanga, kitenge, kofia au fulana.

mzee wa ban,
maneno yako sawa na kusema hakuna jambo jema laweza kutokea nazarethi.......
 
- Easy now, not that fast!, tuheshimu uamuzi wa wananchi waliopiga kura!

William @ NYC, USA.

Kama ni kuheshimu waliopiga kura, kwanza Kikwete na serekali yake wakubali kuwa walichakachua kura kwa makusudi au kwa mfumo uliopo. Na waseme ukweli kuhusu yaliyotokea kwenye uchaguzi uliopita.
Hatuwezi kun'gang'ania eti tuheshimu waliopiga kura wakati matokeo haya represent kile kilichokuwa kwenye box za Kura....huu utakuwa ni ukandamizaji.
Nadhani wakitaka kuheshimiwa kwanza waweke ukweli wote hadharani, ndio heshima itarudi.

And when we need change hakuna taratibu mana watu wanaendelea kufa kwa kukosa huduma za afya, watoto hawasomi, na uchumi unadorora...fast track is the only solution....we just need to overhaul the system then mazungumzo ni huko baadae....
tumeona mazungumzo mengi sana lakini hakuta tija.
 

Mkuu William; heshima mbele. Nina hakika kuwa wewe una mtazamo chanya kuhusu chama chako kwa kuwa unauchungu nacho. Na huenda huwa hujiulizi CCM ikufanyie nini bali unajiuliza wewe uifanyie nini CCM?. Kwa ujumla ni kwamba CCM ilianza kujimaliza yenyewe kwa kuacha malignant members wenye desire ya kukitumia chama kwa manufaa binafsi kujipenyeza mpaka kwenye mishipa ya damu ya CCM kwa kisingizio cha ufadhili wa chama. Hawa kwao CCM ni mradi wa kuweka viongozi wanaowataka kuongoza taifa ili wawatumie katika kuhujumu uchumi kisha kutumia pesa hizo hizo kukifadhili chama. Hawa wao issues are nothing kama kuna mtu atakuwa anatishia ustawi wao wa kupata madili yote ya kibiashara ya serikali na kutumia hila kuchota hazina ya nchi kwa mikataba feki. Watamuandama kummaliza ili aonekane useless mbele ya jamii. Thanks to Wazalendo wa kweli kwa kuianza kuwaamsha watanzania ili wajue haki zao.

Mara nyingi CCM imekuwa mabavu ya dola kuzuia upinzani kuelimisha umma kwa hofu kuwa watu wakijua haki zao itakuwa ngumu kuwadhibiti kwa uonevu, na kutumia intelijensia za uongo kufanikisha azma hiyo, vyombo vya dola navyo vimekuwa ni Toilet tissues za CCM kwa muda mrefu kiasi cha kujikuta hawaaminiki tena na wananchi. CCM inahitaji miaka mingine 50 ili kurudisha imani kwa umma. JK hawezi kufanya chochote kwani naye ni victim wa mfumo mzima wa kuingia madarakani kwa rushwa. Akimwaga mboga wao watamwaga ugali. Ila anaweza kuiokoa nchi kwa kuiacha ijitengenezee katiba mpya iliyohuru bila ya ku-infect mchakato mzima, hilo likifanyika na Tanzania ikawa nchi ya demokrasia iliyo huru na haki, tutashuhudia wananchi wakiwaweka viongozi wao madarakani na siyo Mafisadi kuwawekea viongozi, na hilo likifanyika, basi CCM itaanza kujadili issues na siyo watu.
 
pata washauri na kabla hujaongea fikiria kidogo wewe nape! Zile siku tisini za magamba ni aje? Na ile kauli ya wachagga na chadema hujasikika ukikanusha, kwa maana hiyo bado ina simama!

hoja zote mbili nimeshazijibu vyakutosha bahati mbaya sina private email yako ningekutumia majibu mwenyewe maana hii ya kusema naona we haikufikii
 
nguvumali,
ahadi zipi uzisemazo na porojo zipi tuziache?
Tukumbushane ahadi za JK

1.Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
2.Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
3.Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
4.Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
5.Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
6.Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
7.Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
8.Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
9.Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
10.Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
11.Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12.Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
13.Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
14.Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
15.Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
16.Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
17.Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18.Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
19.Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
20.Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
21.Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
22.Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
23.Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
24.Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
25.Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26.Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
27.Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
28.Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
29.Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
30.Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
31.Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
32.Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
33.Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
34.Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
35.Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
36.Kulinda haki za walemavu - Makete
37.Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
38.Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
39.Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40.Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
41.Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
42.Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
43.Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45.Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
46.Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
47.Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
48.Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
49.Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
50.Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
51.Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
52.Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
53.Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
54.Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
55.Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
56.Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
57.Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
58.Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
59.Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
60.Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
61.Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
62.Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
63.kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
64.Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
65.Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
66.Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
67.Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
68.Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
69.Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
70. Barabara za angani (fly overs. )
 
nguvumali,
ahadi zipi uzisemazo na porojo zipi tuziache?

Nape kumbe unaongoza jahazi na hujui kuwa mnatakiwa mtimize vitu mlivyoahidi? au wewe huhusiki na hukumbuki aliyezitoa?
 
hoja zote mbili nimeshazijibu vyakutosha bahati mbaya sina private email yako ningekutumia majibu mwenyewe maana hii ya kusema naona we haikufikii

Wewe umejibu lini, hebu weka hapa au nirushie kimokole@jamiiforums.com nikusaidie kuweka wengine waone
 
hoja zote mbili nimeshazijibu vyakutosha bahati mbaya sina private email yako ningekutumia majibu mwenyewe maana hii ya kusema naona we haikufikii
ndio hizi?
 

Nape hebu tupe majibu maana mwaka wa Jk unakatika huo na ahadi ni karibu 70 bado miaka minne tuu je zitatimizwa au ilikuw ani mbinu ya kupata kura
 
nguvumali,
ahadi zipi uzisemazo na porojo zipi tuziache?

Nape kaka yangu,so unataka kutuaminisha kuwa AHADI zote za Chama cha Mapinduzi zishatekelezwa..wacha nijaribu kukumbuka chache

  • siku 90 kutibua mafisdi,
  • kujenga barabara za lami kuzunguka mlima kilimanjaro,
  • viwanja vya ndege vya kimataifa,

Aaaah wacha nisiumize kichwa changu kukumbuka vitu vinavyoniumiza ilihali nilisha ambiwa na sura ya Msemaji kuwa haiwezekani bali naongea tu sababu siasa ni kuzungumza,eti hamna siasa za mkono mtupu
 
ndo mana nikamuuliza nae anataka kuja kutuongoza kama watoto wa waliokuwa viongozi wengine? Maana naona juhudi zake utadhani Tz ina watu 20 tu, hv mtaacha lini huo ufalme wenu, mnadhani mnabusara kuliko watanzania wote! Tumechoka na majina yenu ala!

hilo nipo na wewe bw wiliam lakini naomba ulijibu hili.
je viongozi walioiba hela za uma wakaenda kuficha ulaya na marekani na baba yako akiwa ni mtuhumiwa wewe unasemaje?

Humo nilikoBOLD umekuona lakini W. J. Malecela?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…