CCM na CHADEMA sasa turudi kujadili solutions za issues muhimu kwa taifa letu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM na CHADEMA sasa turudi kujadili solutions za issues muhimu kwa taifa letu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, May 23, 2011.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  @ Facebook:by William Malecela on Monday, May 23, 2011 at 4:11am

  - Mjadala wa suala la Ukabila na udini ni mjadala ambao umeshapittwa na wakati. Sioni sababu kwanini baadhi ya viongozi wa CCM bado wanatumia karata hiyo linapokuja suala la Chadema. Hatari yake ni kuwa jambo hili litafanya chama chetu kionekane kinawagawa Watanzania kwa misingi ya dini, kabila na hata rangi vitu ambavyo ni vigeni kabisa ndani ya CCM.

  CCM ni chama ambacho kinahitaji wakati huu kuliko wakati mwingine wowote ule kuonesha uongozi katika kujadili issue na siyo watu. Kwa kuanza kujadili watu CCM kimejiingiza kwenye mtego ambao ni vigumu sana kutoka na ni mtego ambao mwisho tutajikuta tunanasa sisi wenyewe. Sasa turudi kwenye issue muhimu za taifa.

  - Kuna masuala mengi ambayo Watanzania tunataka kuona tofauti katika maisha yetu na yanayohitaji majibu kutoka Chama Tawala. Tulienda kwenye uchaguzi na kuomba kura za Watanzania ili tuwaongoze kwa miaka mitano ijayo na hilo ndilo tunatakiwa kufanya siyo kujitetea kila kukicha au kulalamikia upinzani. Kama tutawapatia Watanzania uongozi wakati huu basi hoja nyingi za upinzani zitakufa zenyewe. Lakini tukisikia tena mambo ya Chadema chama cha Wachagga au cha Wakristu kutoka viongozi wa CCM tutakuwa tunakaribisha mgawanyiko mkubwa kati ya wananchi. CCM iachane na hoja hizi za udini na ukabila na iwe mwepesi kujitenga nazo wala isizilee au kuhusishwa nazo kabisa. Siasa za udini na ukabila zimepitwa na wakati twende kwenye siasa za issue:


  Yapo masuala ya:

  Utawala bora
  Elimu
  Utawala wa Sheria
  Nishati
  Katiba Mpya
  n.k

  - Viongozi wetu wa CCM na CHADEMA, mtaanza lini kuzungumzia haya badala ya kuhangaika na mambo ya CCJ na siasa za chama cha Wachagga? Hebu turudi sasa kwenye issues muhimu kwa taifa letu, kama hamuwezi jivueni magamba tuanze upya!


  MUNGU IBARIKI TANZANIA!


  William Malecela.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu WJM,

  Agenda kubwa ni kuitoa CCM madarakani ambayo imeshindwa kuongoza na kuleta maendeleo. Miaka karibu ya 50 sasa tangia tumepata uhuru, ajabu hatuna cha kujivunia Kama taifa. CHADEMA wanafanya Kila kiwezekanacho wanainchi wajue uraia. Porojo za amani na utulivu wakati serikali haiweki miundo mbinu hazina nafasi tena. Ufisadi na wizi wa Mali ya umma ufikie mwisho. adui nambari moja wa Watanzania ni CCM ambacho mtaji wake ni ujinga wa Watanzania wenyewe.
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280

  nilidhani na leo ummjibu kama juzi...''Nepotism''..

  ki u ukweli chaedema inazungumzia kila siku suluhisho la taifa hili lakini ccm hawasemi kitu kazi kusingiziana na kupigana vijembe....kwa miaka 50 hatuna maemdela ya ukweli....sasa hivi nchi nzima imejaa magofu tupu.....magofu kwenye kilimo...magofu kwenye miondo mbinu...magofu kwenye elimu nk.......na yote hii ni sababu ya ccm maana kila mtu ana mipango yake lakini hawaisimamii kazi kuja na misamiati mipya tu.tuko hatua za mwisho......mchakato unaendelea.......jitihaza za serikali ziko wali.........nk

  malecela william ccm hawana nia ya dhanti ya kumaliza matatizo ya nchi hii au kuja na mbadala wa matatizo hayo.....
   
 4. m

  malimamalima Member

  #4
  May 23, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  safi sana william...umenigusa sana...ccm imekuwa ni chama cha kulalamika badala ya kuanza kutekeleza ahadi lukuki...
   
 5. R

  Renegade JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,761
  Likes Received: 1,062
  Trophy Points: 280
  CCM Iachane na mawazo mgando na yaliyopitwa na wakati ya watendaji wake wengi.
  CCM Imefanya mengi katika Tanzania, Yapo Mazuri yanayopaswa kuendelezwa lakini yapo mengine mabaya yaliyolifikisha Taifa hapa tulipo.Kinachotakiwa ni kitu kimoja nacho ni kufanya mabadiliko ya kweli ndani ya CCM kATIKA NGAZI ZOTE, Na mabadiliko haya yawe na lengo la kukijenga chama kwa maslahi ya Watanzania, na siyo ya kupanga safu za mtandao wa kuwania ulaji kwa mwaka 2015.
  CHADEMA hapo ilipo ina mwelekeo mzuri japo yapo mambo ambayo yanatakuwa kufanyika, Chadema ifungue matawi vijijini kote Tanzania,Viongozi Wanapopitia Vijini wahakikishe kuwa wana mtandao wa kutosha kufanikisha team ya ushindi 2015. Tunataka ushindani wa kweli, Yeyote atakayeshinda ni kwa maslahi ya Taifa, na si kuwa na uoga kwamba akiingia fulani Hataivuruga nchi. No way nchi inahitaji mabadiliko, Ushindani wa vyama vya siasa ni kwa maslahi ya Taifa.Lazima kuwa na uwanja ulio sawa kwa washindani woooote. Tume huru ya uchaguzi ni muhimu, kama serikali imeweza kufikisha TAKUKURU isiyo na kazi sehemu zote tanzania kwanini ishindwe kufikisha TUME YA UCHAGUZI KOTE TANZANIA?
   
 6. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #6
  May 23, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Comrade Willium,

  Kudos! Nimekuwa nikisizitiza sana kuhusu hili.To be honest with you after careful thought ,I have come to the conclusion that we are doing exactly what our corrupt leaders want us to do: hate each other based on tribe.
  I think we need to stop this our obsession with the Ethnic sentiments.What we need to do not is what the Americans did in the USA to elect OBAMA.We the youths of Tanzania should work together and come up with ideas as well as strategies to kick out the corrupt leaders in our government. Even a certain tribe,Religion or political party lead or take control of the power in the land or seccede and form another nation based on religion or Tribe,there is no guarantee that there will be no corruption or power hungry politicians in the new formed countries. We should not give up on Tanzania

  Tanzania is still a salvable country ,but our elders are clearly not going to do it for us ,we the energetic youngsters especially the ones in Tanzania are the ones who are going to free themselves.

  Trust me if all Tanzanians can down tools and refuse to go to work ,to school and protest on the streets of Tanzania collectively from the west to the south to the east to the north. Corrupt and weak leaders will relinquish power. We have a big population ,the army can start shooting everybody on the road because of the people demonstrating are relative of the armed forces personnel. If we can do this for a month ,they will have no choice but to surrender to the will of the people.

  We can free ourselves from this “Nightmare” ,instead of coming here and trading insults ,let us work together and stand as one ,that way the government and political parties will fear us ,how can a few hundred people hold 45 million people to ransom? My people please think and think deep ,let us leave cheap political propaganda alone and build a better Tanzania.Jamii Forums(JF) have southands of members and counting ,we can start from here using all kind of social media like youtube ,blog and other social networks to generate support. There are a lot of intellectuals on JF and their contribution to making this a reality is crucial.We can generate ideas on how to impart pro-change spirit n rural dwellers.

  Let us Unite,Tanzania ni yetu sote.

  May God Bless Tanzania,
  God bless JF members!
   
 7. T

  T.K JF-Expert Member

  #7
  May 23, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 345
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  William, alichosema mchungaji hapa ndio ukweli wenyewe....hizo kelele za ukabira na udini ni hoja za kuficha watu wasiutambue ukweli huu
   
 8. m

  mob JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 509
  Trophy Points: 280
  nakushukuru we kwa kuliona hili nimejaribu kuangalia na kusoma katiba inapinga hivi vitu ili inaniwia vigumu kuwaelewa viongozi wetu kama ninavyosikia wanaleta hizi siasa na wakati wao ndo wangetakiwa wawe mahiri katika kutetea haya maswala yasiibuke tena. hebu tusome hay yaliyomo katika katiba....................
  (4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au
  mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria
  yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya
  Mamlaka ya Nchi.
  (5) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii
  neno "kubagua" maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji
  mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao,
  kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini,
  jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina
  fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na
  kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa
  aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida
  iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima, isipokuwa kwamba neno
  "kubagua" halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia Serikali
  kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha
  matatizo katika jamii.........................................​
  .
   
 9. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #9
  May 23, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - Mchungaji sisi Wa-Tanzania sio wajinga wala mabwege tena, tungekuwa Chadema wasingekuwepo the fact kwamba wapo kwa mujibu wa katiba ya jamhuri na tunawalipa kodi yetu kwa ajili ya ruzuku kila mwezi ni ukweli ulio wazi kwamba Wa-Tanzania sio wajinga tena!

  William @ NYC, USA.
   
 10. T

  T.K JF-Expert Member

  #10
  May 23, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 345
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  William, alichosema mchungaji hapa ndio ukweli wenyewe....hizo kelele za ukabila na udini ni hoja za kuficha watu wasiutambue ukweli huu
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  May 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  naona umemchana Nape live
   
 12. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #12
  May 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe kama mwana-ccm, hoja kwamba chadema ni cha kikabila, wachagga na mengineyo unazionaje? ni za kweli? ni uzushi?
   
 13. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #13
  May 23, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hatimaye William umerudi kundini. Na hiki ndicho tunachokitarajia kutoka kwa kijana yeyote mpenda nchi. Unafiki sasa ufike mwisho, tuseme ule ukweli juu ya CCM hata kama ukweli unauma. Wakati wa unafiki umepita. Sasa ni wakati mzuri wa kila mtanzania kuyageukia maslahi ya taifa na kukemea kwa nguvu zote wale wote wanaoonyesha kuzorotesha na kuchelewesha maendeleo ya nchi yetu. Thanks William kwa kuliona hili na kulisema hadharani.
   
 14. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #14
  May 23, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  Hilo umeliona wewe lakini Mwenyekiti wako pamoja na Katibu wako wa uenezi hawalioni hilo na hawaelewi kabisa.
  Jibu ni rahisi, perfomance ya CCM haipo sawa na expectations za wapiga kura, nguvu ya Chadema ilivyo sasa hakuna yeyote anayeweza kuizuia.
  Sio kwamba jambo hili litafanya, limeshafanya lionekane CCM ipo ili iwagawe watanzania. Imeshatugawa kwa misingi ya aliyenacho na asiyenacho na sasa iko bize kutugawa kwa misingi ya kidini na kikabila. Hapo penye red, nahisi huijui vizuri CCM, kama unaijua vizuri rejea kauli ya Kolimba iliyofanya afukuzwe uongozi CCM na linganisha na haya ambayo CCM inayafanya.
  its too late, badala yake CCM inahitaji wakati huu kuratibu kuiba sana raslimali za watanzania,
  Kujadili watu ni culture ya CCM, kumbuka walivyomfanya Dk Salim na Sumaye 2005, kumbuka walivyomfanya Slaa 2010, kumbuka UVCCM walivyomfanya Sumaye 2011, kumbukawalivyomzushia mzee Malecela kuwa alibadili dini ili akipata urais aingize OIC Tanzania.

  Hapa sasa umeongea point, nimekukubali lakini ni vigumu kwa CCM ya sasa ya JK, Ridhwani, Chiligati na wengineo wanaweza kuleta mapinduzi mazito namna hiyo. Tuwapishe Chadema tu mkuu, thats the only solution
   
 15. I

  Iga Senior Member

  #15
  May 23, 2011
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  William Malecela ninakubalina na wewe mia kwa mia. Migogoro sio tatizo. Tatizo ni watu wanaojifanya tu machinoo. Hawashauriki. Hawawezi kufanya kazi na upinzani. Eti wapinzani paka nyau na matusi mengine ndiyo hoja zao. Badala ya kusema sisi sote ni Watanzania na dawa ya umaskini, ujinga na maradhi yetu hawezi kupewa tu BABU mmoja kama yule wa Loliondo inataka tukutanishe na kugonganisha vichwa vyetu. TUNAHITAJI TAASISI MAALUM KUSHUGHULIKIA CONFLICT -Political or economic or otherwise MANAGEMENT AND RESOLUTION kwa faida ya wote na sio kelele za mbwa-mwitu lakini tukitoka nje hatumuoni!!!!

  ALOO Lema, Slaa na Mbowe babangu nilifikri eti mkokoro ni tatizo kumbe ndio njia ya kuamsha waliolala kweli na hasa serikali inapousa madini yetu na kisha kuruhusu 'kaburu. mpya kutuchinja eti. Hivi hao wanasiasa wanafikiri Mara pamoja na hao korokoroni wao ni sawa na mikoa mingine kweli ???Waamke na wajisahihishe haraka au tutalizana kilio cha chura asubuhi kweupe ndugu!!!


  MSIACHE KUISOMA HII NI YA MWAKA KAMA SIO YA KARNE:

  Maendeleo huja kwa Kuchochea migogoro chanya

  MIGOGORO kwa kiasi kikubwa husaidia kila upande kuweka wazi bila unafiki mahitaji na maslahi yake mbele. Wananchi wanapofanya kazi kwa ushirikiano au ushindani migogoro hujidhihirisha kwa baadhi yao kukata tamaa, kejeli, jazba, mazungumzo, majadiliano na mabishano. Hususan, katika ushindani ambamo watu huwa na malengo tofauti au wanakuwa na misheni zilizofanana, ambamo ni mmoja tu kati yao anayeweza kuibuka na ushindi.

  Uweledi, uzoefu, ustadi na ujuzi wa kugeuza migogoro kuwa kitu chanya ndipo hapo inapohitajika. Hatima ya yote hapa ni kuwa na lengo moja na kuongeza faida au manufaa kwa pande zote husika.

  Migogoro chanya ni njia pekee inayomaliza kiini cha matatizo mengi. Kwa tulio wengi tunakubali matatizo na kuyaacha matatizo kuwa matatizo hadi wale yanayowasumbua wanakufa. Na jumla ya matatizo ya wananchi na hasira yao, ndiyo yanayogeuka migogoro mikubwa baadaye.

  Migogoro huwa na faida pale viongozi wanapokuwa wakweli, safi, wachapakazi, bora na waliodhamiria kuleta mabdailiko ya kimsingi katika jamii husika.

  Kinyume chake udikteta katika kuwatawala watu na ubwanaukubwa wowote ule uwe wa mtu au wa kikundi fulani huzusha utitiri wa migogoro hasi.

  Kuanzisha na kuchochea migogoro chanya kubadili hali ovyo, duni na mbaya waliyonayo wananchi na kutafuta hali ya neema kwa kasi na ari zaidi na bora kuliko waliyonayo.

  Fursa za kimaendeleo kwa wananchi zinakuwa ni mambo pacha na matatizo yao ya kila siku na sio tena kitu cha siri bali ni mazungumzo na matukio ya kila siku. Maana usiri ni chanzo kikubwa sana cha migogoro katika jamii husika.

  Tulionesha pia kwamba watu au jamii isiyo na migogoro hunyauka na kufa kimaendeleo kama jamii.

  Hali hii inaonekana katika baadhi ya vijiji na mikoa nchini ambayo inabaki sana nyuma kimaendeleo ikifananishwa na mingine.

  Migogoro kila siku isiyodhibitiwa huwa uwanja wa vita visivyokwisha kama hali ilivyo Somalia leo.

  Ni dhahiri basi upo umuhimu wa kuchochea migogoro chanya katika jamii ili kuwazindua wale walioko usingizini na kutumia kuwa macho kwao kuumua mabadiliko na maendeleo endelevu katika jamii husika.

  Nitajaribu kutumia mifano kadhaa ili kulithibitisha hili. Kwanza, tuanze na bunge letu tukufu. Bunge hilo lilipokuwa na wabunge wengi kutoka chama tawala halikuwa limechangamka kama lilivyochangamka leo. Baadhi ya wabunge walikuwa wakilala badala ya kutoa michango inayowasilisha dhiki na uhitaji wa wale wanaowawakilisha. Swali ni je, gogoro la kibunge ni chanya au hasi. Uchanya wake utatokana na pande zote mbili kujua tabia na mwenendo stahilifu ambao wabunge wanatakiwa kuufuata ili nchi ipate maendeleo kwa kutanguliza mbele Utanzania badala ya uchama, ukubwa na umimi.

  Migogoro itakuwa hasi kama wabunge watalifanya bunge ni mahala pa kukashidiana, kudhihakiana, kudharauliana badala ya kuheshimu michango ya watu na nguvu ya hoja badala ya nguvu za kisiasa na kimamlaka.

  Mfano wa pili ni wa vita dhidi ya umaskini, ujinga na maradhi. Hii ni migogoro ya muda mrefu ambayo inafikia hata wakati mwingine tunaisahau na kuiona ni sehemu yetu ya maisha.

  Mfano mwingine ni wa katiba mpya. Huu ni mgogoro kwa sababu kuna wale walioko madarakani leo ambao katiba ya zamani imewafaa, itawafaa na inaelekea itaendelea kuwabakisha madarakani kwa muda fulani lakini sio milele na wale ambao wanaoona katiba iliyopo inawanyima mengi wanayostahili na wakati umefika wa kuibadili ile ya zamani.

  Upande mmoja kuna serikali na chama tawala (sio wote) na kwa upande mwingine kuna wapinzani na Watanzania wasio na chama (sio wote) na kazi iliyoko mbele yake ni kugeuza mgogoro huu wa katiba uwe mgogoro chanya kwa faida ya Watanzania wa leo na wa kesho. Na kazi ya kuandika katiba mpya bila shaka itakuwa rahisi kama wote tutaelewa na kulikubali hili.

  Mgogoro yenye manufaa itaifanya serikali na chama tawala kwa upande mmoja na wapinzani na wananchi wengine kwa upande mwingine, waweze wote kwa pamoja kuibuka washindi katika ujenzi wa nchi.

  Ipo tofauti kubwa sana kati ya maisha vijijini na maisha ya mjini. Kuna wanaothubutu kusema kwamba maisha vijijini yangelikuwa bora kwa robo tu ya yale ya mjini basi wasingeliishi mijini. Ipo haja basi ya kuchochea maendeleo ya vijijini angalau vijiji vifanane fanane na mijini na hivyo tukawa tunatenda haki kwa wote. Sio kosa kwa mtu yeyote yule kwenda vijijini na kuwaambia hamna maji, umeme, barabara, hospitali safi, shule bora kwa sababu viongozi wameshindwa kazi yao. Mgogoro chanya ndio njia pekee ya kupunguza tofauti kati ya vijiji na miji.

  Mgogoro mwingine ni ule wa upatikanaji huduma na mahitaji ya msingi kwa wananchi. Hili kwa mujibu wa Machiavelli ni jukumu la kwanza la uongozi wowote ule. Maana wananchi wengi wakipata chakula cha kutosha, wakalala mahala pazuri na wakawa huru kuzifuata ndoto zao huwa hawana habari na siasa na utawala.

  Bila maji, umeme, barabara, madaraja, shule na hospitali nafuu na taratibu za kunusuru masikini kwa huduma twaibu na upatikanaji mahitaji yote ya msingi, migogoro itakuwa hasi zaidi kuliko chanya. Na ukweli huu budi ujulikane na kila mtu.

  Katika mikoa kuna maeneo ambayo ina vyuo au vyuo vikuu viwili hadi kumi wakati kuna mikoa haina hata chuo kikuu kimoja. Katika hali kama hii bila shaka kwenye katiba iliyopo, ibara ya 9 kifungu (d) kinachosema: "kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja," hakijazingatiwa. Na hili ni swali la nini huzuka kwanza, yai au kuku ? Ndivyo ilivyo pia kwa viwanda na miradi mingine mikubwa-hakuna usawa kinchi!

  Hakuna asiyejua kilichotokea huko Yugolsavia hata tukisema Mungu aepushilie mbali! Maana kinachoonekana sasa ni kuwa ni pale tu mkoa unapokuwa na Waziri mkuu au Waziri wa elimu utakapoweza nao kupata chuo achilia mbali Chuo Kikuu. Kwa maoni yangu, badala ya kujenga vyuo vikuu vikubwa tunavyoshindwa kuvitawala na kuviendesha vyema ni bora kila mkoa kwa sababu za haki na usawa kila mkoa uwe na Chuo Kikuu chake ili kuchochea maendeleo ya elimu ya juu, utafiti na uchumi kwa jamii husika.

  Watanzania wote walichangia kwa kodi yao uanzishaji wa makampuni ya umma. Yalipotaifishwa hakuna Mtanzania wa kawaida aliyenufaika kitu moja kwa moja. Hiki ni chanzo kizuri cha mgogoro kama tutauliza kama tuliweza kuanzisha makampuni yaliyomilikiwa na serikali kwanini tunashindwa kuanzisha makampuni yatakayomilikiwa na wananchi au wanajamii wenyewe moja kwa moja ?

  Pengine mikoa inazorota kimichezo na kisanaa kutokana na serikali na chama tawala kuhodhi baadhi ya viwanja vya michezo. Je, upo mgogoro chanya utarudisha viwanja hivyo mikononi mwa wananchi na kuchochea bora zaidi kujengwa ?

  Katika kila eneo la maisha, imani/dini, kazi, elimu, uwekezaji, kujiajiri, huduma, biashara na kadhalika kuna tofauti na kasoro nyingi tu. Hii ni migogoro. Kazi yetu sio kuifukia chini bali kuiweka wazi na kuishughulikia iwe migogoro chanya kwa faida ya nchi na watu wetu!

  Kwanini Barricks wapewe migodi mingi hali hawajali maisha ya Watananzia wanaoteketea huko Mara, Bulyahunlu na kwingineko?
  Na kwanini kodi zao ziwe chini kiasi cha kuishtua IMF? Huu si mgogoro? Na kwanini hatukuwapa Wachina au Wakorea au Warussi au Wajapani baadhi ya migodi ili
  tunufaike zaidi.

  Madrasa za kiislamu, shule, vyuo,vyuo vikuu, hospitali na taasisi zingine kama vinaendeshwa ovyoovyo na kimasikini, je ni vibaya kuuondoa siasa na ukiritimba uliopo katika dini hiyo ili kuleta migogoro chanya na hatimaye taasisi hizo ziendeshwe vyema kwa faida ya wote ?

  Migogoro chanya hufanya kazi yake vizuri kama watu wanaheshimiwa, wanaelimishwa, wanafunguliwa macho na wahamasisha kuikataa hali mbaya iliyo na kudai hali nzuri ambayo wanaelezewa au kuiona katika picha au sinema.Wachochezi wakifanya kazi yao vizuri wanaweza kubainisha mabilioni ya kodi yanayokusanywa kila mwezi kuwa yanaweza kabisa kufanya kazi hiyo na nyinginezo nyingi na kurahisisha kuharakisha mapambano yetu ya kutafuta maendeleo.

  Uongozi safi na bora hauwezi kupatikana hadi pale wananchi watakapoamka na kutambua kuwa wao ndioi 'matajiri' na mabwana au wamiliki wa katiba, mamlaka na madaraka yote ya nchi hii na viongozi ni vibarua wao. Wana uwezo wa kuwapa kazi na kuwafuta kazi pindi watakapotaka kufanya hivyo. Umma ukishirikiana na wanasiasa wakweli, watendaji waadilifu na vyombo vya habari visivyotumiwa kwa maslahi ya watu binafsi kufuatilia kazi na nyendo zote za watumishi wao ili nchi ipate kitu chenye thamani sawa na kile inachowalipa wale walioko madarkani.

  http://www.blogger.com
  Posted by KWETU KUPENDWE KWANZA at 11:10 PM
   
 16. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #16
  May 23, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280


  - Easy now, not that fast!, tuheshimu uamuzi wa wananchi waliopiga kura!

  William @ NYC, USA.
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  sipingani na wewe ila asilimia kubwa ya watanzania juwezi kusema kuwa wameshaufuta ujinga
  kama unabisha angalia hii picha hapa huyo ni Nape ndugu yako, tutafika kweli?
  [​IMG]
   
 18. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #18
  May 23, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  W. J. Malecela unatarajia kugombe uongozi TZ?
   
 19. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #19
  May 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,982
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Katika ukweli mzima watu wenye uelewa wanajua swala la ukabila halipo kabisa na linakuzwa kwa maslahi ya watawala.
   
 20. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #20
  May 23, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  Uamuzi upi mkuu? Mi nadhani waasisi wa ufedhuli huu wa kutoheshimu maamuzi ya wananchi ni CCM
   
Loading...